Sajo MC

Penda Unachofanya mbali na kuwa jina la album ya Sajo MC huwa pia ni moja ya kauli mbiu zangu tangu nilipojinyakulia mradi huu.

Sajo MC ambaye ni mtu wa Mbeya, Tanzania alitoa mradi huu mwaka jana na baada ya kuuskiliza kwa mda niliona ni vyema nirudi kwake tena ila wakati huu nipige naye stori ili kuweza kumfahamu yeye na mishe zake za muziki.

Karibu sana kaka Sajo MC hapa Micshariki Africa. Kwanza kabisa tuanze kwa kukufahamu unaitwaje, unatokea wapi na unajishughulisha na nini?

Kwa jina kamili naitwa Lusajo Yusuph Kaganjo, natokea Mbeya na nje ya mziki najishughulisha na udereva.

Tueleze kidogo kuhusu historia yako ya nyuma ya mziki. Ulizaliwa wapi, masomo umefikia wapi na ulianzaje hizi mishe za mziki?

Mimi nimezaliwa Mbeya mwaka 1989, na kimasomo namiliki Degree moja Bachelor Of Accountancy (BAC) kutoka chuo cha Tanzania Institute of Accountancy. Kuanza kwangu mziki nimelelewa na K4S member (DAS J) pamoja na Mastiff ni brothers ambao nilipokua mdogo wao walikuwa wanachana sana pia walikuwa wanamiliki tapes nyingi za nje ambazo kadri ya nilivokua nasikiliza zikawa zinanipa vibe pia,tapes izo mfano ni za Das Efx ,Lost boyz,Dr. Dre ,Xzibit ,Nas na nyingine nyingi.

Tueleze kidogo kuhusu jina lako Sajo MC lilikujaje na linamaanisha nini?

Sajo ni jina linalotokea kwa jina langu halisi Lusajo,na MC nilipewa na watu wangu wa mtaa baada ya kuwa natembea na microphone kihakika.

Mpaka sasa una miradi mingapi, inaitwaje na imetoka lini?

Nina mradi mmoja Penda Unachofanya uliotoka mwaka 2021 na pia nisharekodi mixtape moja pamoja na album moja nyingine ambazo sijaziachia bado

Tueleze kidogo kuhusu mradi wa Penda Unachofanya. Mradi huu ulikujaje, watayarishaji waliohusika humu ni akina nani, ma emcee waalikwa pia kwenye mradi huu? Je maudhui ya mradi huu ni yepi?

Mradi wa Penda Unachofanya umetayarishwa na muandaaji Wise Geniuz chini ya studio za AMG Records. Maudhui ya huu mradi yaliangalia sana maisha halisi anayoishi mwanadamu wa aina yeyote na wasanii walioshirikishwa umo ni Janta Kawe, Zamkiller, Shaulin Seneta pamoja na Isanga Native.

Kwenye mradi huu ni ngoma gani unazipenda na ni kwa nini?

Kwenye mradi huu nazipenda ngoma zote ila Shtuka na Mashakani na Wasanii ni ngoma ninazozipenda zaidi kwa sababu nilivokua naziandika nilikuwa na vibe kali.

Kwenye mradi huu uliachia ngoma yoyote ya kutambulisha mradi? Je mradi huu unapatikana wapi? Hebu ongelea Mashakani, huu wimbo historia yake ni nini? Kwa nini uliamua kuuandika?

Katika mradi huu niliamua kuachia wimbo mmoja unaoitwa Shtuka ,na mradi huu unapatikana kwa njia ya WhatsApp  +255656117828. Wimbo wa Mashakani niliuandika kutokana na mazingira ya hiki kizazi kipya tunavoishi.

Mjumbe Zero ni nani, nani alikuwa analengwa hapa? Wimbo mzuka sana.

Iko wazi Mjumbe Zero niliyekua namzungumzia ni Mbeya Boy (Chuma) na wenzake baada ya wao kumdiss brother angu in culture Lugombo MaKaNTa.

Kando na mziki Sajo Emcee unajishughulisha na nini? Je unapiga chombo cha mziki?

Kando na mziki mimi ni dereva na katika mziki naweza kupiga ngoma na gitaa.

Unazungumziaje utayarishaji wa Wise Genius. Kwa nini uliamua kupiga naye kazi  kwenye mradi huu?

Wise Geniuz ni producer anayejiamini pia hana kwere na watu wa aina yeyote (anaweza kuishi na mtu wa kila aina)na midundo yake ina match na mitambao yangu.

Ma emcee chipukizi ungewashauri nini kuhusu mziki huu na utamaduni wa Hip Hop, wafanyeje ili waweze kuwa ma emcee wazuri?

Mcs chipukizi wote katika utamaduni wa Hip Hop nawashauri wasiigize harakati (wasi pretend kwa wanachokifanya)na wakazane kuandika jumbe zinazoishi.

Nini cha mwisho ungependa kutuambia ambacho sijakuuliza?

Nadhani mengi umeniuliza ila ningependa kutoa ushauri kwa ndugu na jamaa wote wanaokata tamaa kutokana na ugumu wa maisha, Sajo MC ni mtu anaye amini mafanikio yapo kwa kila mtu duniani.

Shukran sana kwa mda wako kaka Sajo MC.

Asante sana brother Mkombola kutoka Micshariki Afrika, tuko pamoja acha upendo utuongoze.

Mfuate Sajo MC kwenye mitandao ya kijamii;

Facebook: Xajo MC
Instagram: sajo.mc.tz

Kununua mradi huu kwa Tshs 10,0000.00 wasiliana na Sajo MC kwa njia ya WhatsApp: +255656117828.