Uchambuzi Wa Album: Penda Unachofanya
Emcee: Sajo MC
Tarehe iliyotoka: 02.07.2021
Nyimbo: 15
Mtayarishaji, Mixing & Mastering: Wise Genius
Studio: AMG Records
Nyimbo Nilizozipenda: Mjumbe Zero, Combination Party, Lengo, Maisha, Mashakani, Ndio Hivyo, Sisi, Somo, Wasanii, Shtuka, Nduta

Sajo MC
Kama kawaida yangu mimi hupenda kuchukua risk na kununua miradi ya wasanii ambao sijawai waskia kabisa kando na kununua miradi yao kabisia ili kuweza kuskia miradi ya wasanii ambao siwafahamu kabisa.
Kufanya hivi kuna uzuri wake na ubaya wake; ubaya ni pale ununue mradi alafu ukute ni mbovu na hela imeshaenda na uzuri wake ni umenunua mradi uliojaa madini mwanzo mwisho. Ila kiukweli ni kua kwa mimi ambae ni mwandishi yote freshi kwani inakua ni fursa ya kuchambua miradi yote na kuwapatia wasanii mrejesho.
Mwaka jana nilinunua miradi kibao kwa style hii na moja ya miradi hii ni Penda Unachofanya ya Sajo MC. Mradi huu ambao umesimamiwa kwa asilimia mia na mtayishaji Wise Genius toka AMG Records Mbeya haukuniangusha. Kama kawaida yake WG hujitahidi kupatia watu anaopiga nao kazi midundo mizuri ila ma emcee pia waweze kujielea vizuri.
Na kujieleza vizuri kwa mashairi ndio kitu alichokifanya Sajo MC toka ngoma ya kwanza Somo akiwa na Isanga Native hadi wimbo wa mwisho Mashakani akiwa Janta Kawe. Ngoma iliyotambulisha mradi Shtuka ni wimbo chanya sana unaokuhamasha kuwa macho mda wote na kutobweteka.
Uwezo wa Sajo unauona vizuri kwenye nyimbo kadhaa kama vile Lengo. Kwenye mdundo mzuka sana na akiwa na ma emcee wenzake Zam Killer na Big Dreams, Sajo anatuhamasisha tuishi maisha yetu tukiwa na malengo. Nyimbo zingine ambazo emcee huyu amepita freshi kabisa ni kama Maisha na Mashakani akiwa na Janta Kawe. Mashakani unasimulia unapiga tofauti maana unasimulia story za maisha za vijana flani walioendekeza maisha ya anasa na mwishowe wakajikuta kwenye matatizo. Nduta pia inapigwa ki story pia na ipo freshi sana.
Wimbo mwingine chanya unatufungua macho kuhusu vile watu wapo tofauti na lazima tujue kuishe nao nakujisachi pia ni Ndio Hivyo. Anasema Sajo MC kwenye beti ya kwanza,
“Hizi mipango nauliza ziko vipi/
Wale wengine bata wengine na dhiki/
Wengine mikwanja wengine hawalipwi/
Wengine makosa wengine ndio tiki/
Wengine wapo real wengine wanafiki/
Wengine jua kali wengine wana mali/
Wengine wame sleep wengine hawalali/
Na yule anajidai kisa babae ana gari/
Atasemaje asie na baba/
Wengine wamechili wengine kahaba/
Wengine wameshiba wengine labda/
Mtaa wana hustle wengine wana kaba/
Yule anatake wakati yule analia/
Wengine wanatupa wengine wanatamania/
Wale wanatenda wengine wanafikiria/
Wengine wa kusini wengine ma baharia/”
Mjumbe Zero Part II ni muendelezo wa beef kati ya Lugombo na Mbeya Boy. Lugombo alitoa Mjumbe Zero (Mbeya Gay Chuma Diss) hapo awali na Sajo MC akaamua kushindilia msumari kwenye jeneza. Kwenye wimbo huu pia Sajo MC anatema nyongo dhidi ya Mbeya Boy pia kwa utaratibu na uwasilishaji mzuri akisema kwa ucheshi kwenye beti ya pili,
“Mjumbe Zero naona kama unazingua/
Maisha ya uswazi unajikuta wakishua/
Age kama yako unaona kama hujakua/
Huna hata mipango unawaza kutusua/
Mitandao inadanganya ila wewe tunakujua/
Sijui utakwenda wapi jamii yote ikikuchoka/
Na kwenu umewadanganya wee ni mkali wakufoka/
Na kuchoma kama kaya kweli hauna ubaya/
Achana na ujinga jaribu soma riwaya/
Ikikushinda zaidi kajiunge na kwaya/
Acha kwenda resi maisha ndio haya haya/
Bila kujitambua mwisho wake mbaya/
Maneno mengi eeh mdomo mali yako/
Ongea mengi ila anza na ya kwako/
Sio ng’eng’e ng’eng’e nyingi kwenye harakati za wenzako/”
Sajo MC kupitia mradi wake wa katuonesha kua uki Penda Unachofanya tutaona na kukubali kazi yako kama tulivyoikubali kazi yake.
Mfuate Sajo MC kwenye mitandao ya kijamii;
Facebook: Xajo MC
Instagram: sajo.mc.tz
Kununua mradi huu kwa Tshs 10,0000.00 wasiliana na Sajo MC kwa njia ya WhatsApp: +255656117828.