Beti ya kwanza
Aliskika Akilalama Mbona Anapungua Uzito/
Mwili Unamuuma Anachoka Anakuwa Mzito/
Kwenye Kila Kiungo Alisema Anaumia/
Anaumia, Hata Akimeza Pain Killa/
Siku Chache Badae Pasipo Mategemeo/
Ngozi Ikababuka Usoni Ikaunda Shape Ya Kipepeo/
Hana Nywele, Vidonda Akazidi Kudhoofu/
Wakasema Amelogwa Wenye Akili Potofu/
Wale Wa Kupima Kwa Macho Hawakurudia Mara Mbili/
Walidai Dalili Za Tb na Ukimwi/
Kila Mtu Lake Sio Sheikh Sio Shemasi/
Maabara Za Mtaa Vipimo Vyao Vyote Hasi/
Hospitali Ya Mkoa Haikujua Nini Haswaa/
Wakampa Referral Kiswahili Rufaa/
Muhimbili Dar, Hawakuchukua Muda/
Daktari Akamwambia Kuwa Anaugua Lupus/
Beti ya pili
Akauliza Ndio Ugonjwa Gani Na Wapi Ulipotokea/
Ameambukizwa Na Nani Ni Wapi Alipokosea/
Dokta Akamwambia Skiza/
Magonjwa Yapo Kibao Dunia Nzima/
Yapo Yenye Tiba Na Yapo Yasiyotibika/
Yapo Ya Kurithi Na Yapo Ya Kuambukizwa/
Lupus Haiambukizwi, Na Sio Ugonjwa Mpya/
Ni Wa Kurithi Upo Tangu 1600/
Labda Mmoja Wa Mababu Au Bibi Alikuwa Nao/
Mmoja Katika Uzao Na Ndio Maana Leo Unao/
Hii Ni Hitilafu Katika Kinga Ya Mwili/
Badala Ya Kinga Kuukinga Inashambulia Mwili/
Kwa Kuwa Haina Tiba, Basi Watatibu Dalili/
Na Watafubaza Kinga, Ili Isizidi Kuathiri/
Nenda Hospitali, Fanya zoezi, Kula Fresh/
Kubali Hali Haina Haja Ya Kuwa Na Stress/
Beti ya tatu
Baada Ya Kuelimishwa Na Dokta Kupewa Skuli/
Karudi Mtaa Akawa Balozi Mzuri/
Akishakunywa Dawa Zake Za Kutuliza Maumivu/
Anapaka Mafuta Ngozi Anaufungua Mwavuli/
Jua Lisimuathiri, Akienda Street Kuwapa Shule/
Aliwaamsha Kule Hapa Hapa Kule/
Lupus Sio Kansa, Sio Ukimwi, Sio Kulogwa/
Kutenga Kunyanyapaa, Sio Kuukabili Ugonjwa/
Lupus Haiambukizi Kama Alivyosema Dokta/
Jamii, Iwapokee Wenye Nayo Pia Wana Ndoto/
Mara Nyingi, Watu Wacheck Afya/
Ukiona Dalili Nenda Ka Test Fasta/
Hata We Muda Wote Unaeza funza Watu Mitaani/
Usingoje Tarehe 10 Mei Siku Ya Lupus Duniani/
Na Juhudi Za Serikali Juu Ya Magonjwa Ya Kuambukizwa/
Zisiyasahau Haya Magonjwa Yasiyoambukizwa/