Beti Ya Kwanza

Uwe Mtulivu Uwe Mjuaji Much Know/
Shika Elimu, Ongeza Elimu Kielimu Uweze Grow/
Usiache Kusoma Waarabu Wanasema Iqra/
Mambo Mbalimbali Fahamu Kwenye Maisha/
Usiache Dunia Inabadilika Kwa Kasi/
Huenda Unachojua Leo Kitashuka Thamani/
Usiishie Kukumbata Ulichojua Zamani/
Make sure Unaongeza Kitu Kipya Kichwani/
Na Hata Kama Ni Kimoja Kila Day/
Zingatia Hakikisha Hakitoki Kinastay/
Maana Elimu Ni Elimu Iwe Ndogo Ama Kubwa/
Na Kama Itakufaa Si Mzuka?/
Umepita Vidato Bandugu Hongera Sana/
Ukaipata Uliyopata Heko Vyema Sana/
Ila Hiyo Sio Tiketi Ya kusema Hapo Mwisho/
Usidharau Nyingine, Ukasema Umemaliza/

Beti Ya Pili

Sawa Una Vyeti Vizuri Tayari Umeelimika/
Lakini Hujamaliza Kubali Kuelimishwa/
Maana Elimu Yako Imeegemea Kwa Ulivyosoma/
Ulivyospecialize Ndo Sana Vingine Holla/
Elimu Ni Pana Mwingine Kasoma Kile/
Ambacho Akija Kwako Inakuwa Mambo Mengine/
Na Bado Hakimfanyi Kuwa Bora Kukuliko/
Maana Yake Ni kwamba Hatujatosha Kufundishwa/
Each One Teach One Twende Hivyo Maisha Haya/
Nijuze Nikujuze Hata Pasipo Kulipa Ada/
Elimu Ni Bahari Tuskume Chombo Pamoja/
Tuvuke Twende Mbali Tusonge Kwa Pamoja/
Kama Wewe Ni Intellectual Haipingwi/
Sema Ikipanda Kichwani Ni Upimbi/
Nenda Unapoenda Kasome Bukua Uchoke/
Ila Hata Uwe Nani Huwezi Kujua Vyote/

Beti Ya Tatu

Nipe Usikivu Dadaa, Nipe usikivu Jamaa/
Hivi Ushawahi Kusikia kuhusu Elimu Ya Mtaa/
Wapo Watu Hawajui Kitabu Kinafananaje/
Ila Wana Maujuzi Maujanja Ndo Mahala Pake/
Kushinda Hata Wasomi Ma Degree/
Elimu Ya Mtaa Wali pass Ma GED/
Na Maarifa Yao Yanawasaidia Kuishi/
Na Maisha Yao Wana Mafanikio Kuzidi/
Sikukatishi Sikukati Stim/
Huenda Njia Zao Zikawa Marking Scheme/
Kwako, Kuwa Humble Kwa Huyu Yule Hapa Kule/
Chunga Usiwe Mjinga Baada Ya Kuanza Shule/
Fika Mpaka Chuo Faulu Na Uvae Joho/
Ila Usiache Kujifunza Na usikatae Bro/
Shule Haiishii Kiwango Cha Madaraja/
Na Haiishii Kwenye Milango Ya Madarasa/

Yeah yeah
Elimu ni Popote Hujaelewa Rudia Tena/
Kuna Wengine sheria wameijulia Jela/