Beti Ya Kwanza
Ewe mzazi Fundisha mtoto kusalimia/
Kuamkia vile vile kusema Habari pia/
Kila salam iwe asubuhi mchana usiku/
Hizo zote mtoto azijue kikamilifu/
Ni wajibu mzazi Acha kuona kazi/
Usishindwe kumfundisha hata kuomba radhi/
Aseme samahani aseme nimekosea/
Akiri kosa na kuahidi tena halitotokea/
Mfunze shukran na umuhimu wa asante/
Kwa vikubwa na vingi vifinyu na vichache/
Na Haipendezi mzazi akiwa bubu/
Kukalia kimya swala la Heshima kwa kila mtu/
Mfunze kuheshimu wakubwa pia wadogo/
Bila kujali Hali na pia kasoro/
Ndio unamjengea future na Uko bize kazi/
Ila Tenga time umfundishe nyumbani/
Kiitikio
Maadili mema yanafundishwa nyumbani/
Tabia njema zinafundishwa nyumbani/
Ni Wapi!! Nyumbani Ndo Shule Ya Maadili/
Na Nani!! Mzazi ndio Ticha wa maadili/
Maadili mema yanafundishwa nyumbani/
Tabia njema zinafundishwa nyumbani/
Ni Wapi!! Nyumbani Ndo Shule Ya Maadili/
Na Nani!! Mzazi ndio Ticha wa maadili/
Beti Ya Pili
Kemea vitabia vya kubagua bagua/
Mjenge ale kila msosi sio kuchagua chakula/
Na Mfundishe table manners akiwa mezani/
Asiwe mlafi, asiongee na chakula kinywani/
.... Na mfundishe kuhusu usafi wa mwili/
Akiwa nyumbani, akiwa mtaani ajue usafi wa mazingira/
Sema udokozi mbaya asichkue kisicho chake/
Mfunze kusaidia ndugu na Wazazi wake/
Usipuuze eti sababu hauko free/
Ni wewe wa kumfundisha juu ya adabu na utii/
Unaniskia? We Mfundishe Hauna budi/
Mkataze matusi na mfundishe lugha nzuri/
Mfundishe thamani ya vitu Mfundishe na uaminifu/
Mtahadharishe gharama inayoletwa Udanganyifu/
We Mfundishe hata anapoanza kuwa mkubwa/
Mkumbushe kujipanga na kuanza Kujali muda/
Kiitikio
Maadili mema yanafundishwa nyumbani/
Tabia njema zinafundishwa nyumbani/
Ni Wapi!! Nyumbani Ndo Shule Ya Maadili/
Na Nani!! Mzazi ndio Ticha wa maadili/
Maadili mema yanafundishwa nyumbani/
Tabia njema zinafundishwa nyumbani/
Ni Wapi!! Nyumbani Ndo Shule Ya Maadili/
Na Nani!! Mzazi ndio Ticha wa maadili/
Beti Ya Tatu
Nilisema nitasema na nitarudia tena/
Mfundishe mtoto wako kuhusu tabia njema/
Huo ni wajibu wa mzazi/
Kabla ya yoyote kabla Ya mwalimu na mfanyakazi/
Usilete visababu Usilete visingizio/
Kwenye Good morals wewe ndio ujenge misingi hiyo/
Hiyo ni kazi yako, ukiwa nyumbani kwako/
Na mtoto wako Usimuachie mwalimu wake/
Maana Kazi ya teacher ni kutilia mkazo/
Sasa atakazia nini kama hukumfundisha Mwanzo/
Mwalimu muachie hesabu na sayansi/
Haiba ya michezo lugha na stadi za kazi/
Muachie Jiografia muachie Baiolojia/
Muachie Sanaa muachie Saikolojia/
Muachie hayo ila Morals usimuachie Mtu/
Fundisha maadili for a better future/