Beti Ya Kwanza
Mmenikuta kwenye vitu vyangu/
Hii kitu naipenda Ninatii kiu yangu/
What's up GQ this is my essential/
My number one na itabaki mpaka kesho/
Niwe nyumbani au mbali na maboda/
Lazima ntakuwa na chupa ziwe mbili ama moja/
Shule hujaona hata ma Drinks ma mzinga/?
Usifananishe maji na vitu vya kijinga/
maji kwanza Slogan ya kongwe/
Utasema nimezama navyogonga vikombe/
Natoa sumu na bacteria/
Takataka Nyingine na flush nakaa vyema/
Kukaa vyema Kwangu Mbona kitu simpo/
Sijaona Homa ya kunishona mfululizo/
Sio kinywaji tu kwangu mi ni tiba babii/
Wanaopelea kila dakika Fatigue/
I eat water I drink water you see/
Af nakaa kijanja, I be water Bruce lee/
Wengine wanakunywa juisi, maji ya matunda/
MI nakunywa hivi hivi nipe maji makubwa/
Kiitikio
Kunywa maji hii sio lugha ya picha/
Kunywa maji, gida kunywa kabisa/
Eight glasses a day, keep the doctors away/
Eight glasses a day, keep the doctors away/ X 2
Beti Ya Pili
Mimaji tena, Koo liwe laini/
Nayaongeza Niwe msoo niwe fine/
Natawala jukwaa natambaa na midundo/
Naambaa Bila kukamaaa kwa viungo/
Grease kwa vyuma ndo maji kwenye mifupa/
Yana Lubricate Na Ni Kilainishi kikubwa/
Hulinda uti wa mgongo na other sensitive tissues/
Watu wa matizi hapa hutuambii kitu/
Hurahisisha na mmeng'enyo wa chakula/
Huzuia kuvimbiwa na tumbo kuuma/
Yanarekebisha hadi harufu ya kinywa/
Amini man Nakufundisha mtu mzima/
Watu wa skin care kwa ngozi Safi yenye afya/
Huondoa makunyanzi huleta muonekano wa ujana/
We Kunywa Low fat au fat-free milk/
Kunywa lozi almond milk/
Na Mzee wa plain coffee Nakuona/
Uko sawa ila nakuapia maji ni bora/
Mi sitaki kujua ni wapi utayapata/
Ila hakikisha kuwa ni Safi na salama/
Kiitikio
Kunywa maji hii sio lugha ya picha/
Kunywa maji, gida kunywa kabisa/
Eight glasses a day, keep the doctors away/
Eight glasses a day, keep the doctors away/ X 2
Beti Ya Tatu
Maji muhimu acha kusema ya kazi gani/
Na je unahitaji Maji mengi wakati gani/
Ukitamani kwa sana vitu vyenye sukari/
Hamna issue Mwanetu kanywe tu maji/
Nakupa somo kidogo kidogo/
Kunywa maji Ukiona una mkojo kidogo/
Au Mkojo wenye rangi hebu fanya ujiwahi/
Upunguze risk za kupata UTI/
Kunywa maji mengi kama unaharisha na kutapika/
Zidisha! kama uko sick na una fever/
Zidisha! kama kuna Joto la kuzidi/
Unaposhughulisha mwili piga vikombe vya wingi/
Ukipakua Chakula, usisahau maji/
Ukipooza mitula, usisahau maji/
Saidia Figo Kwa kutosahau maji/
Fundisha na wengine kutodharau maji/
Unahitaji maji ya kutosha ufanye kazi/
Kabla ya kwenda kwa doctor kanywe maji/
Da Dada da dee mnashipata mazee/
Eight glasses a day, keep the doctors away/