Beti Ya Kwanza

Shida kidogo tu Murder kill kill/
Kweli Magonjwa ya akili ni real/
Unachinjaje mtu kisa kakukataa/
Sababu nyingine Unashindwa hata kushangaa/
Aaa Na hizi ndoa za kufosi/
Tunafosi sana mwisho Tunazoa Na Mikosi/
mtu ukimuoa bila yeye kupenda/
Ana asilimia kubwa kuwa na wenge la kwenda/
Kingine ni Tamaa ndogo ndogo/
Wife unaye bado unakaa kwa Dogo dogo/
Bronzo Ishirikishe akili/
Kama vipi muhalalishe mfanye mke wa pili/
Mara Wivu wa kimapenzi Unakuteka Unaongoka/
Hujui ka Unaumwa Unateswa na sonona/
Mwisho mapanga na tindikali/
Unamuua mwanamama kinyama hata hujali/
Huyu nimesomesha yule nimelea mimba/
Huyu nimempa mtaji yule nimejengea Nyumba/
Tuliza ndonga bro utaua wangapi/
Shusha Mkono Mambo hayo sasa basi/

Kiitikio

Shusha Mkono!! Acha Unyanyasaji!!
Shusha Mkono!! Huo sio ushababi!!!
Shusha Mkono!! Badilisha itikadi!!!
Shusha Mkono!! Zuia Mauaji!!

Beti Ya Pili

Kabla hatujauliza is it love or shillings/
Tukubaliane kwanza kwamba No more killings/
Kabla hatujatafuta chanzo ni bwana au bibi/
Tushushe mikono kwanza au vipi/
East Africa, mbona Unyanyasaji Unakithiri/
Kutwa Visa ka utitiri na Mauaji ya kikatili/
Hii miaka miwili Wanawake wanazidi kaa/
Yani Kenya pekee ni zaidi ya sitini na/
Bado bongo Uganda na nchi zilizobaki/
Story ni nyingi kuliko walizo publish/
Waliozeshwa mapema haijatosha/
Wengine walikeketwa haijatosha/
Walikuwa mpaka chombo cha starehe na haijatosha/
Wakanajisiwa kisa fedha haijatosha/
Saivi imekuwaga kifo ndo suluhu/
People are so evil unyama ndo umekubuhu/
Duuh! Na hii Mifumo dume/
Ndo inafanya tuone kwamba wanawake wakikosea wana haki ya kuchezea wanastahili hata wakufe/
tuiangalie kama sio Ivunjwe vunjwe/
Tucheki njia nyingine ila mikono ndio ishushwe/

Beti Ya Tatu

Licha ya kuwepo mashirika na Wadau mbalimbali/
Most of the time Haki za binadamu hazifuatwi/
sheria zimetungwa na hazina maana/
Msaada hautoki hata Kimahakama/
Utaskia Tunafanyia upepelezi/
Na Hawachukulii serious kufuatilia kesi/
Ndio maana wahanga hata polisi hawaendi/
Maana hawazingatiwi Wanakalishwa sana benchi/
Wakikumbuka kero na Kuombwa rushwa/
Wengi wanakataa tamaa na kuanza Kungoja kufa/
Oya wakubwa ambao bado hamjashtuka/
Kisa Bado Hamjakumbwa au Bado hamjaguswa/
Shit serious and not funny remember/
A next victim might be one of your family members/
Na watu wengine ambao wapuuzi sana/
Ni wenye dough, Viongozi wanao misuse power/
Upuzi sana Hizi groups bana/
Zapaswa kuwajibishwa kabla ya issues za karma/
Msiposhusha mikono mjue tu iko day/
Mtashikwa na mtahukumiwa, muwe condemned/..