Beti

Haijalishi kwamba uko level gani ya kimasomo/
O level, advance au chuo flani unasoma/
Unajengwa kuajiriwa uje upate kazi nzuri/
Ni vizuri tena Soma kwa usongo na ukaze msuli/
Kila hatua piga mabanda na high marks/
Pepa zijae Pass kuwa mjanja like that/
Kimbiza ndoto zako za nataka kuwa nani/
Ila chkua mbili Tatu Kabla ya Kuja mtaani/
Nakupa moyo kuwa mitkasi itatiki/
ila siwezi kukudanganya kuhusu hali ya nchi/
Kwenye Sekta binafsi na serikali ni mtiti/
Michongo haionekaniki hiyo ndo Hali halisi/
That's why niko hapa Kuna kitu tushee/
Muhimu sana na Inabidi Nikugee/
Hicho kitu kinaitwa plan b/
Huenda wengi wanakijua ila hawakuambii/
Naamini mbali na Shule una talanta nyingini/
Uwezo wa Kufanya jambo swadakta ki umahiri/
Kiumahiri Hata kama sio talanta/...
... Ila unaweza kujifunza na uka masta/
Na ukaliboresha ukajikuta umelijua/
Na ukajua kwamba litakuinua ukiamua /
Anza kudeal nalo usingoje Shule iishe/
ongeza maarifa Jifunze jiivishe/
Mwambie mzazi kipi unaweza fanya/
Sema mapema Kitu unachopenda acha kukwama/
Niko sure.. hawezi kataa kukusapoti/
Kama lengo ni Kuishi poa na kushika Noti/
Ikitokea huna mashavu ya ajira/
Huwezi kuwa disappointed ghadhabu na hasira/
Nna hakika.. Huwezi kupoteza mitaji/
Zaidi ni kuwekeza kuendeleza kipaji/
Na kuendeleza si kazi, kazi kuanza moja/
Kujitafuta mpaka ujipate huwa ni noma/
Na Uchumi wa nyumbani wengi hatuna Pesa nyingi/
Unaweza kumtesa dingi mikopo na pressure nyingi/
Ndugu! Sasa Yote ya nini/
Wakati namna ipo Ukijenga msingi/
Badala ya kungoja ajira wakati muda unakwenda/
Au Kufanya kazi ambayo hata hujaipenda/
Au kuwa chini ya mtu na kumtumikia/
Utajiajiri na.... mwisho wa siku utafanikiwa/...
Start slow start small utagrow fast and bigger/
You just Trust the process huo wakati utafika/
Tafakari chukua hatua ka wasemavyo haki elimu/
Hii vita utaishinda ukikamata hizi mbinu/...