Beti Ya Kwanza
Jamani ee poleni kwa usumbufu/
Najua wengi mmechoka ila naombeni mniruhusu/
Nipeni dakika chache mnisikilize right now/
Nna mawili matatu ya kuitisha hichi kikao/
Sisi wote wapangaji wote tumepanga/
Kila mtu katoka alikotoka tumekutana/
Wapo tuliowakuta wapo waliotukuta/
Basi tuongee sio mambo ya kuzunguka/
Wengine hata majina hatuyajui hatusomani/
Tunapishana tu bafuni au bombani/
Ni salamu tu baada ya hapo buyu baya/
Mtu yuko next door ila hakunaga kujuana/
Humu ndani Ni watu wachache wanaivana/
tunajiongeza tukiskia wakati wanaitana/
Tunaweza kuona kuwa sio vitu vya lazima/
Ila ni vyema kufahamiana sio kutungiana majina/
Kwa kuwa nimewaita basi ngoja nianzishe/
Naitwa Shule, haya kila mmoja ajitambulishe/
Ama baada ya salamu, baada ya kujifaham/
Naomba niende kwenye mada bila Kumaliza time/
Beti Ya Pili
Kuhusu kodi hilo ni swala la landlord na wewe/
Si tuongee maswala yetu walipa kodi wenyewe/
Najua wazi kuwa hatufanani vipato/
Kila mtu na hali yake hatulingani michakato/
Wengine hohehahe wengine wana nafuu/
Wengine mboga nane wengine matawi ya juu/
Lakini bili hazijui, lazima kuwajibika/
La sivyo tutakaa giza au Maji kukatika/
Na kama mjuavyo hizo ni huduma muhim Na/
Tukasema mchango kila chumba kitalipa/
Sasa mbona wameibuka mabingwa wa kula chocho/
Siku wakibananishwa wanaita Watu wanoko/
Mtu unajua ni zam yako kununua umeme/
Unaondoka unarudi usiku ukishakuwa mnene/
Sometimes uko tungi na kauli za kishujaa/
Buku tatu ya nini tupambane na Mishumaa/
Mara ntalipaje sawa na siwashi vitu vingi/
Mara naoga mara mbili tu hata maji situmii/
Hata buku la taka mtu anakaza hatoi/
kufanya usafi utata ni kuchafu mpaka toi/
Beti Ya Tatu
Na kuna mambo mengine Sio shwari wandugu/
Sometimes hakujakucha ila tayari vurugu/
Mziki ka library, mpaka mabati yatubu/
Imagine unaamshwa na sukari ya zuchu/
Brother na woofer yako unavyofanya sivyo/
Kumbuka kuna watu wana sound kama disco/
Na sister pale sikufichi una maudhi/
Maana akitokea mtu Mkapishana kauli/
Ni nyimbo za Isha mashauzi/
Na Kisha Unazifuatisha kwa sauti/
Na nyie madogo wa chuo wa ile room ya kwenye kona/
Msijione mna akili au ni nyie tu mmesoma/
Kuzoea wanawake utadhani mademu zenu/
*Msipende kitonga kaeni mbali na wake zetu/
*Mi nliitwa mvutaji sasa nazimia mbali/
Na bado vijineno eti navutia ndani/
Hebu tuache chuki na kusemana vibaya/
Story za Uzushi na kuchorana si sawa/*
Tushirikiane Tupendane kama ndugu wa damu/
Kama ulikuwa hujui si ni ndugu Fahamu/
Zinatokeaga Shida za ghafla/
Iwe za kifedha au Shida za kiafya/
Pengine ni saa mbaya na ni shida za fasta/
Majirani ndo si wenyewe hizi shida zikitupata/
Outro:
Na yule mama wa chumba kile/
Siku yoyote akijaga tu mmwambie/
Si amewekwa kutuspy thats why halipi kodi/
Mwambieni Kiherehere hakimfanyi kuwa bosi/
Lugha chafu na kashfa, kupimana tunaishije/
Michezo ya kiswahili, na kuchawiana ife/