Beti Ya Kwanza

Kinachofikisha hii mitambao ni waya/
Mic na beat kali nkipita nayo ni fire/
Micshariki ndo mtandao wa kupata mawe ka haya/
Na Leo niko nao wanaotumia mitandao vibaya/
mshamba anajigamba utasanda shughuli yangu/
Ukijimix kwenye Moja na saba kumi zangu/
Mara sura kama nini Huna shughuli babu/
Nani kakupanga kwamba Ujanja ku bully watu/
kuna wapo wanaochafua wenzao/
Wazee wa matusi na picha chafu ndio kwao/
Wanaorekodi mabinti wakifanya nao ngono/
Na kuanza kuwa blackmail kutaka madau manono/
wanaounda ma parody kujifanya madem/
story zao kutwa Kukojozana Kwa game/
Kwa hiyo wazee, huwa mnawish kuparamika/
Aponzwa na likes hivo ndio tweet zitaandikwa/
Na wengine wanatapeli watu/
Mkifaulu kukamatwa ndo mtajua mnafeli wapi/
vitu vya kipuuzi ndo vinapigiwa shangwe/
Hii mitandao mzee, utakuja kuumia One day/
Na Keyboard warriors wajeshi wa baobonye/
ni waoga we Kutana nao uone/
Wanakujaza uende mbele ukigeuka utawaona wapi/
Wamejiloki kwenye Mageti Kwao masaki/
Usifuate mkumbo, utapotezwa na uzushi/
Pia kumbuka.. sio kila agenda ni ya kupush/
Usisambaze maudhui mabaya kuna sheria/
Siku ikikugharimu lazima tu Utalipia/

Kiitikio

Nenda pole pole sana Mister/
Nenda pole pole sana sister/
Ni kubaya kabisa, huko kote unakopita/
Sio mdomo tu hata vidole huponza kichwa/
Tulia fasta Acha mambo ya kihuni/
Tumia sasa Mitandao vizuri/
Mitandao ina faida ikitumika Inavyofaa/
Na itakufaa ukiitumia Kimanufaa/

Beti Ya Pili

Ukiwa na busara Hautoyumba asilani/
Utaepusha misala hutojikuta hatiani/
Kama unataka umaarufu kupitia/
Chagua njia zisizohusu Kujutia/
Unaweza eleweka bila Kutumia nguvu sana/
Unaweza kukosoa bila ya kutukana/
Unaweza kuheshimika bila ya kudanganya/
Kuwa kawaida inawezekana nini inakuchanganya/
Hii mitandao tu, tena ipo tangu na tangu/
Isikupeleke mbio ufanye mambo ya ajabu/
Unakutana na wengi kumbuka kuwa So smart/
Usije pata shida kuna maisha ukisha Log out/
Sisemi uwe nyumbu au mtakatifu/
Nasema uji control usije ukaharibu/
Hata kama umejiunga ili kuja kufurahi/
Usikwaze wengine hiyo huwa haifai/
Hata wamiliki, wanaelekeza kila wakati/
Na sio wajinga kuweka vigezo na masharti/

Kiitikio

Nenda pole pole sana Mister/
Nenda pole pole sana sister/
Ni kubaya kabisa, huko kote unakopita/
Sio mdomo tu hata vidole huponza kichwa/
Tulia fasta Acha mambo ya kihuni/
Tumia sasa Mitandao vizuri/
Mitandao ina faida ikitumika Inavyofaa/
Na itakufaa ukiitumia Kimanufaa/

Beti Ya Tatu

Mitandao ina faida ikitumika Inavyofaa/
Na itakufaa ukiitumia Kimanufaa/
Watu kibao wameitumia wakatoboa/
Wameifanya njia wakatulia sa wako poa/
Mtandaoni biashara kibao zimekua/
Mtandaoni maujanja kibao unachukua/
Mtandaoni.. nako kuna Elimu chungu nzima/
Pay attention ka huwezi basi jaribu Ujinga/
Usisubiri mpaka iwe kinyume ndo upate akili/
Muda ndio huu wa kuhamia upande wa pili/
Tafuta connection unda network/
Rasilimali watu watumie in a right way/
Mtu ni anachokula acha msosi au matunda/
Akili itakuwaje ka Ubongo umeshiba pumba/
Smart phones smart people digilatika Kijanja/
Ushaambiwa dunia ipo kwenye kiganja/..!