Beti Ya Kwanza
Kwenye mitaa hii tunayokaa ama ku settle/
Na kupitia maisha ya furaha na mateso/
Kuna watu,
tunawafaham hadi kesho/
Wanaficha vingi nyuma ya tabasamu na vicheko/
Mfano Wanandoa hawana noma wanachekeana/
Wako poa hata wakitoka na mikono wanashikana/
Hakuna tofauti yoyote wanaoneshana/
Ila nyuma ni usaliti na sivyo inavyoonekana/
Wanavyoishi utahisi hawajaweza kung'amua/
Ila ukweli ni kwamba Kuna mwenza kashajua/
Au mtu anajua ana ugonjwa /
Unammaliza taratibu anakufa anajiona/
Cha ajabu kanyamaza ana battle kimya kimya/
Na anatamani msaada anapaswa kusaidiwa/
Kuna mifano lukuki kaka/
Watu wanaficha mengi Moyo wa mtu kichaka/
Kinachosikitisha na kuchosha hadi saizi/
Kwa mambo ya kufikirika wanakosa usaidizi/
Chorus:
Usikae na kitu funguka/
Kunyamaza sio ishu funguka/
Bwana Hakuna shida funguka/
Bibi Vunja ukimya funguka/
Beti Ya Pili:
Pengine Kwa sababu ya kuogopa kutengwa/
Au Kwa sababu ya kuogopa kuchekwa/
Au hata kwa sababu ya kuogopa Kusemwa/
Unakuta Mtu ana tatizo na anaogopa kusema/
"Vipi nikisema na nikakosa msaada/
Naweza nikajieleza na nikaongeza msala/
Tatizo langu linaweza kuwa aibu/
Japo nalenga kujenga ila naweza Kuharibu/
Ukaribu, undugu mahusiano vile vile/
Vinaweza kuvunjika watu hawana simile/"
Badala kukata shauri amwambie flani na flani/
Anaamua kuchagua aumie ndani kwa ndani/
Coz Hakuna anayependa kuonekana ni weak na/
hakuna anayependa kuonekana mjinga/
Kwa Kifupi tumejijengeaga Utamaduni/
Kuwa Hakuna anayependa kuonekana tofauti/
Sio mbaya ni sawa kujifariji/
Ila ukweli utabaki ukweli hata kama ukijitahidi/
Kuficha vile ama kuficha hivi/
Ila haiwezi fanya hilo tatizo Kupita hivi/
Sanasana litazidi kukutafuna/
Litazidi kukuvuruga na kuzidi kuwa kubwa/
Chorus:
Usikae na kitu funguka/
Kunyamaza sio ishu funguka/
Bwana Hakuna shida funguka/
Bibi Vunja ukimya funguka/
Beti Ya Tatu:
Kama unaminya na kinywa hautafungua/kumbuka Mficha maradhi kifo humuumbua/
Mimi siwezi nikakuficha skia/
Kuna madhara makubwa Unapoficha hisia/
Na kupelekea vile unavyohofia kwa uchache/
Kuja kwa wingi na kukujalia We udate/
Asiye sawa hayuko sawa ataonekana/
Haijalishi mara ngapi anakazia yuko fine na/
Kama wanaokuamini inabidi Uwadanganye/
Vipi wakijua na wakakosa imani nawe/
(Na) stress unayozidisha kuficha na kadhalika/
Isipotibika Hukaribisha na washirika/
Yapo madhara ya kutolala vizuri/
Kiafya hapo majanga huja Asubuhi/
shinikizo la damu high blood pressure/
magonjwa ya moyo lazima yatakutesa/
Sukari nayo haiko mbali ni kugusa/
Au) kifo cha mapema haikatai ni kuvuta/
Kama Kufunguka ndio mwanzo wa kujitibu/
Ya nini kuvunga au kujitia uraibu/
Au kuwaza kujiua kwa sumu au kamba/
Kujining'iniza na kujitesa hadi kudanja/
Kabla hujafika huko kifikra hadi kimwili/
Acha kujiharakisha Subiri/
Magumu unayopitia haupitii alone/
Humu kwenye dunia hakuna kipya homie/
Najua ni ngumu kwa jamii inayokuzunguka/
Jipe muda, kisha jiamini kufunguka/
Chagua unayemuamini na uliye huru kwake/
Iwe mtu, taasisi mtilie maguu mfuate/
Mweleze yote na usibakishe kitu/
Jiaminishe uaminike usijiwazishe kitu/
Unayepigana kuwa sawa kuwa full ni wewe/
Kuwa free, ukweli utakuweka huru milele/
... Chenye mwanzo kina mwisho yatakwisha/
Yamalize urudi utimize mipango Maisha/
Yalosibu yamesibu simama pambana nayo/
Ni ya muda utatulizana utaachana nayo/..