Beti Ya Kwanza – Genry UK+

Ulikuwa mtoto sasa ujana umesogea/
Siyo lazima vyote ufanye vingine unaangalia/
Ni maji ya moto yenye mengi machafuko/
Ujana giza la mchana itengeneze kesho yako/
Popote ulipo madawa siyo upande wako/
Yakulevya wako mwili hayana fair dhidi yako/
Nisha poteza wengi ambao niliwaaminia/
Sababu ya mihadarati ma cocaine kujitupia/
Wakuu usipo wasikia mbeleni unavunja mguu/
Hivyo thamini pumzi afya ni moja tuu/
Na inasongwa na vingi maradhi mpaka tama/
Usijihusishe madawa hayata kufaa/
Sioni sawa kusikia masela wameelemewa/
Na madawa ya kulevya hadi wanashindwa kujielewa/
Nguvu kazi inapungua kwenye kusonga tunakwama/
Umri unakwenda hakuna tunacho fanya/
Ni hatari kwa maisha oya zungu ebu kausha/
Kama nyingi umeisha uza mpaka sasa inatosha/
Unda mipango chanya lete mtaa tuishi nayo/
Siyo madawa ya kulevya hapa zikakuokoa mbio/

Kiitikio - Geovan

Make the world a better place/
Tuepuke mihadarati/
And this goes direct to our societies/
And trust me that’s simple/
Ukiweka nia thabiti tambua njia ipo/
Simple/
Ukitaka kuacha madawa ya kulevya/
Simple/
Niamini mimi kila kitu unaweza/

Beti Ya Pili - Pdaz

Kinacho wapoteza umarecani mwingi/
Wadosi wana waponza kwa shilling/
Vijana nguvu ya taifa/
Utajiri wa fasta wana kufa/
Kwa kuuza na kuvuta plama/
Biashara ya unga wigo mpana/
Madawa ya kulevya sio poa maze/
Yamefanya mchizi wa Ilala apotee/
Serikali inapiga vita mbele/
Wanao yaingiza nao wanapiga kelele/
Wana tupotezea maboya gizani/
Tusi mjue mchwani ni nani/
Madawa ni kisanga kabisa unapotea/
Wanapotea wana awajutii kutumia/
Wala ganja msitafute stim zaidi ya hizo/
Shisha mwanzo wa madawa ilo tatizo/
Mitaa aipendezi na mateja/
Pambana dhidi ya madawa ile ki soja/
Kwa hisani ya afya madawa sio mchongo/
Maamuzi ya kuiga yasifanye uache pengo/
Toka kusini juu Pdaz mwafrika pure/
Napinga madawa madhara sija hadithiwa/
Niko stable harakati 49/

Kiitikio - Geovan

Make the world a better place/
Tuepuke mihadarati/
And this goes direct to our societies/
And trust me that’s simple/
Ukiweka nia thabiti tambua njia ipo/
Simple/
Ukitaka kuacha madawa ya kulevya/
Simple/
Niamini mimi kila kitu unaweza/