Beti
Watoto Bwana Inabidi Wacheze/
Wabembee, Ukuti Kwa Wingi Na Rede/
Maigizo, Hali Kadhalika Mdako/
Mpira Wa Makaratasi Utotoni Tuliita Taso/
Waruke Kamba, Waimbe Nyimbo Na Ngonjera/
Kioo, Uringo Bayoyo Kombolela/
Baba Mdogo, Kula Mbakshie Baba/
Waruke Wakimbie Wote Waskie Raha/
Michezo Ya Watoto Ile Michezo Sahihi/
Huimarisha Afya Na Uwezo Wa Kufikiri/
Inajenga Umoja Na Mshikamano/
Vitu Kama Chuki Na Woga Vitapita Kando/
Pia Inasaidia Kugundua Vipaji/
Kujua Tabia Kwenye Hatua Za Ukuaji/
Swali Kwa Mzazi Mlezi Mr Na Mrs/
Mtoto Atapataje Hayo Akishika Ma Ps/
Akifungiwa Geti Na Kuchezea Ma Toy/
Akiongea Mwenyewe Au Akipewa Smartphone/
Hiyo Ndio Unaita Michezo/
Hebu Acha Kubwetesha Hilo Taifa La Kesho/
Kuendekeza Uzungu We Mwenzetu Unawezaje/
Fungua Geti Mtoto Acheze Na Wenzake/
Na Kama Huchezi Nao, Usicheze Mbali/
Ili Uweze Kuzuia Ikitokeza Hatari/
Maana Watoto Wanaweza Kuumizana/
Na Kingine Michezo Migumu Hapana/
Basi Mchezo Ufanane, Na Umri Wa Mtoto/
Na Kujichanganya Huja Na Changamoto/
Wakataze, Wasiharibu Za Mali Za Jamii/
Wasiige Tabia Mbaya, Na Maradhi Yasiwafikie/
Na Kumbuka Kuwaingiza Michezoni Mapema/
Ili Wasizubae Wasiwe Wagumu Wa Kuelewa/
Wasishindwe Kujiamini, Na Kujiheshimu/
Kujiongoza Hiyo Ni Kitu Muhimu/
Malezi Mema Mama Junior, Na Baba Babu/
Muache Watoto Wacheze Ila Too Much Is Harmful/...