Beti

Sanaa, Sanaa Ni Nini/
Sanaa Ni Muziki, Ni Uchoraji, Uchongaji, Uchezaji Na Kadhalika Yani Sanaa Ni Nyingi/
Kwa Kiingereza Inaitwa Art, ART/
Na Kama Unataka Kuujua Ukubwa Wa Hii/
Ntakwambia, Ina Ukubwa Wa Kutisha/
Kwa Sababu Ni Kubwa Kiasi Cha Kuyazunguka Maisha/
Na Haiishi Tu Kuyazunguka Na Kupita/
Japo Mikono Yake Haionekani Ila Huyagusa Kabisa/
Ni Deep Sana, Ila Mi Ntaiongelea Kwa Uchache/
Na Kabla Sijaendelea Ngoja Niishkuru Kwa Kuiambia Asante/ Asante...

Amini, Vitu Havinogi Bila Art/
Imagine Kila Kitu Kifanyike Ki Black N White/
Sio Kweli, Ili Kuwe Na Perfection Lazima Nakshi Nakshi/
Mfano Mdogo Tu Fikiria Ma Brotherman Bila Kushave Na Ku Shape Up/
Hehe! Au Masista Duu Bila Make up/
Bila Kutupia Dizain Mbalimbali Za Mavazi/
Au Bila Kunukia Kwa Harufu Flani Flani Za Marashi/
Serious..
Jiulize, Ingekuwaje Kama Stress Ingekuwa Haipungui Au Kuisha Kwenye Maisha Ya Mwanadamu/
Ungeambiwa Utaje Vitu Vifupi Sidhani Kama Ungeacha Kuitaja Life Span/
Bila Hii Basi Ingebaki Vurugu Chaos/
Nani Hana Sanaa Nyumbani Kwake Au Kwao/?
Haikwepeki/
Sababu Kama Haipo, Haiko Freshi/
Kaa Chini, Fikiria Corona Na Majanga Ka Hili/
Yanayopelekea Lockdown Na Kukatazwa Kusafiri/
Yanayozaa Curfew Na Kukaa Karantini/
Bila Kujifurahisha Au Kujiburudisha Wangapi Wangehimili/?
Na Usidhani Kuna Hilo Janga Tu Basi/
Kuna Watu Wana Majanga Binafsi/
Hapa Sanaa Inafariji, Inaondoa Baridi, Inaondoa Upweke/
Sanaa Inaondoa Woga, Inatibu, Inaondoa Depression/
Na Sio Perepeche Hata Sayansi Imethibitisha/
Kwamba Ku Appreciate Art Kunaboresha Maisha/
Dr Shelley Carson Alisema Ina Uwezo Wa Kuboresha Mood/
Inazidisha Kuzingatia Na Kutusogeza Kwenye Tatuzi/
Za Maswala Mbalimbali Kimaamuzi/
Sanaa Inaleta Ubunifu/
Inakidhi Haja Na Kuleta Hali Ya Kuridhika, Satisfaction Wanaita/...

Sana... Ipo Kila Mahali Ujue Au Usijue/
Na Kama Umeiona Picha Au Mchoro Wa Kuvutia Na Unajiuliza Ununue Au Usinunue/
Professor Semir Zeki Wa University College of London Uingereza/
Alisema, Ukiangalia Sanaa Nzuri Yenye Kustaajabisha Na Kupendeza/
Yani Sanaa Kali Iliyorembwa/
Husisimua Ubongo Wako Sawasawa Na Pale Unapopenda/
Yeah.. Pale Unapo Fall In Love/
Huo Msisimko Sasa Huoni Hilo Balaa/
Hiyo Ndo Sanaa/ Sanaa Noma Sanaa Hatari/
Nunua Hiyo! Wekeza Na Peleka Sanaa Nyumbani/
Kwanza Ni Urembo/
Na Kila Kazi Ya Sanaa Ina Hadithi Nyuma Yake Hakuna Iliyoundwa Bila Malengo/
Kwa Hiyo Hutuambia Msanii Aliwaza Nini/
Hii Ina Maana Tumeshawasiliana Kiakili/
Hii Ndio Inatufanya Tuzielewe Hisia Zetu Za Ndani Kabisa/
Yeah! Inatufanya Tujijue Kama Watu Yani Sisi Ni Kina Nani Hakika/
Inatupa Mawazo Mapya Na Uzoefu Mwingine Kabisa/
Inatusafirisha Mpk Kilomita Zisizofikika Pindi Tunaposafiri Kifikra/
Kazi Ya Sanaa, Inatufanya Tuheshimu Na Kushkuru Kwa Vitu Tulivyonavyo/
Kipindi Tunapo Connect Nayo Kimawazo/

Haswa Pale Tunapoangalia Au Kuskia Yaliyomo/
Na Kuyalinganisha Au Kufanya Tathmini Na Ya Upande Ambao Sisi Tuliopo/

Na Muunganiko Wa Fikra, Hisia, Mitazamo Na Uhalisia Wa Nje/
Ni Sehemu Ya Visababishi Vya Kufanya Maisha Yetu Yabadilike/
Sasa Kumbe Basi, Sanaa Inayapa Umuhimu Na Inayapa Thamani Maisha/
Aisee.. Sanaa Ni Maisha/
Huwa Najiuliza Kila Wakati/
Hivi Dunia Nzima Imetengeneza Ajira Ngapi/
Jibu Ni Ma Milioni Na Mamilioni Malaki Na Malaki/Sanaa Kazi/
Inatoa Nafasi Ya Kuonesha Jamaa Vipaji/
Na Anayefanya Sanaa Ni Msanii Kama Mi Na Nakiri Ka Abbas/
Bila Sanaa Ningekuwa Mkabaji Mitaa Ya Kati/
Basi, Kwa Maana Hiyo Ntakuwa Right Nikisema Sanaa Inatunza Amani/
Vile Vile Inasukuma Tutani/
Samanta Kaplan Alisema Sanaa Inatusaidia/Katika Kuujua Ulimwengu Na Watu Pia/
Na Alienda Chini Zaidi Na Zaidi Na Akatuambia/
Sanaa Ni Zawadi Kwenye Dunia/
Bila Ubishi Kumtenga Mtu Na Sanaa Ni Zaidi Ya Kumuondoa/
Mi Naona Isingekuwepo Dunia Ingekuwa Imepoa/
Na Ni Bora Kupoa, Dunia Ingekuwa Inaboa/
Ingekuwa Haipendezi, Ingekuwa Tupu, Ingekuwa Wazi, Ingekuwaaa Dah ... Ingekuwa Sio Poa/....