Lyrics

Verse 1:

Leo naomba tuulizane humu ndani/
Hivi kufuata utaratibu huwa kuna ugumu gani/
Maana kuwa watu sijui wameshindikana/
hawafuati Utaratibu kila wanapoingiaga/
kwenye sehemu za huduma za kijamii/
Za kwao ni kuvuruga wanapokuja hawaangalii/
Na huhitaji kuwa profesa ili kusoma mabango/
Jipange kwenye foleni mmoja mmoja ndio mpango/
Hawa raia wana muda wako hapa/
Sio kisa Umewakuta ndio ukajua Hawako fasta/
wala sio wajinga wala sio wavivu/
Watulivu japo mstari unakwenda taratibu/
Sasa ndugu yetu wewe unaingia saivi/
Na Unataka upitilize kwa spidi mia ishirini/
Acha habari zako acha janja ya nyani/
Rudi nafasi yako kisha panga mstari/

Chorus:

Yeah!! Iwe hospitali au tanesco.. Mstari/
Iwe dukani ama benki.. Mstari/
Iwe bombani hata central/
Ofisi za Serikali ama private sector.. Mstari/ X2

Verse 2:

Nyie ndo Mkifikaga mnatuliaga pembeni/
Mnapeana ishara mnatumiana meseji/
Haipiti dakika mnaitwa mnapita mbele/
Sasa leo mtakubali kupita ni kipengele/
Skia wewe, Tumekutana humu humu/
Hatujui kama wewe unajuana na muhudumu/
Haituhusu haijalishi hata kama nani yako/
We panga tu mstari ngoja mpaka zamu yako/
Hata mwalimu mwenyewe, hayati Mwalimu nyerere/
Alifuata foleni kwa mstari sembuse wewe/
We unakuja tu, na foleni unaivuruga mkuu/
Tunakwambia kwa uzuri, unatufanyia kiburi/
Ka maziwa yaliyochemka kwa gesi unakuja juu/
Haaa.. Kama unafura fura tu/
Mkuu.. Ila hapa utarudi nyuma/
La sivyo madirisha yafungwe Tukose huduma/

Chorus:

Yeah! Iwe hospitali au tanesco.. Mstari/
Iwe dukani ama benki.. Mstari/
Iwe bombani hata central/
Ofisi za Serikali ama private sector.. Mstari/ X2

Verse 3:

Yeah! Unaongea unabonga bonga/
Tukijisahau unachomekea ka boda boda/
Ma broda ngoja, tunasonga mmoja mmoja/
Acha kujikausha jishtukie ona noma/
We! Hebu Chapisha Upesi sana/
Wapo wenye haki ya kupita we simama/
Wajawazito walemavu na Wazee sana/
Hao ndio wanapishwa peke yao we hapana/
Labda na wagonjwa ambao hawajatengamaa/
We acha kujifanyisha Usituletee sanaa/
Hapa Kila mtu anataka kuhudumiwa/
Hapa kila mtu ana haraka ndugu tulia/
Jiulize ni nani anapaswa Kusubiria/
Kama Kila mtu anataka Kuhurumiwa/
Fuata foleni Hebu okoa muda mwana/
Kama una haraka ni poa ungekuja jana/