Pakua ngoma hii hapa! Download this track here!
Lyrics
Verse 1:
Mi naamini nyie ni wazima wa afya/
Mnaonaje tukiongea kuhusu Bima ya afya/
Kwa msiojua msiwe na shaka na hili/
Tuanzie hapo Bima ya afya ni nini/
Ni mfumo wa kujiunga kwa hiari au lazima/
Unaomuhakikishia mwanachama kugharamiwa/
gharama zote zinazojitokeza/
katika kupata huduma za kiafya anapokwenda/
Mfano kumwona dokta na kupimwa/
Au kupewa dawa pamoja na kutibiwa/
(Huu) ni kama mkataba unaoingiwa na pande mbili/
Anayetaka na mtoa huduma kupitia taasisi/
Au mifuko inayounganisha pande zote/
Sa mshanipata wote/
Mara nyingi Bima ya afya hujumuishwa kwenye makato/
Anayoyatoa mwajiri malipo yafanyikapo/
Kwa watu aliowaajiri au wafanyakazi/
Na kuna bima zile za watu binafsi/
wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine/
wenye mahitaji maalumu na wanafunzi vile vile/
Mdundo unapiga
Verse 2:
Watu huchagua hizi taasisi au mifuko kulingana/
Na aina, viwango au mwisho bima inapokava/
Maana hii mifuko inatofautiana/
Tanzania NHIF ndio inatumiwa sana/
Kuna STRATEGIS, AAR na METROPOLITAN/
Ni vyema Mwanachama angepata elimu ya kutosha/
Kuhusu huduma viwango na mipaka/
Kabla ya kujiunga na mfuko anaotaka/
Kiukweli kuna ulazima wa fasta/
Kila mwananchi kuwa na bima ya afya/
Kuna muda maradhi yanakukuta hauna pesa/
Lakini ukiwa na bima utatibiwa bila cash
Na/
hata wenye pesa inaweza isitoshe/
Ila wenye bima watacover vitu vyote/
Hutokatisha matibabu wala kungoja/
Utatibiwa bure mpaka utakapopona/
Tena kwa huduma bora hospitali za uhakika/
Bila hofu ya gharama ya vipimo na kadhalika/
watu wengi, hawana pesa ya dhahura/
Bima ndio mkombozi itawabeba wakiugua/
Mdundo unapiga
Verse 3:
Asante kwa vingi na vya msingi vile vile/
Hebu tuambie sasa nini kifanyike/
Watu wapewe elimu ya kutosha/
Wajue kwa nini bima sio kitu cha kukosa/
Kuanzia mijini hadi vijiji ndani ndani/
Zifanyike kampeni katika Uhamasishaji/
Na Mashirika ya bima yaweke bei rafiki/
Watu wa kila hali watokee kwa wingi/
Au bima zipangwe kwa madaraja/
Mtu akate kulingana na kipato anachopata/
Pia njia za malipo inabidi ziwe rahisi/
Na Wateja popote walipo wafikiwe kirahisi/
Na hospitali zinazopokea bima zifundishwe/
Sio akija mwenye hela mwenye bima asubirishwe/
Hii ipo sana na nimeshashuhudia/
Hudumieni wateja sawa na muache huo ujinga/