Pakua ngoma hii hapa! Download this track here!
Verse 1:
Kwa Utaratibu wa wengi ili kufanikisha jambo/
Njia mowajapo ni kuchangisha michango/
Michango iko mingi kuna ya shida na raha/
Tugusie inayohusisha furaha/
Harusi, tafrija, e tee chee/
Rika na jinsia zote yani me na ke/
... Na Kabla sijaendelea na mambo haya/
Naanza na kusema kwamba michango sio jambo baya/
Ili kuona mambo yanafana tuna enjoy/
Kwa usawa huu bila kuchangishana hatutoboi/
kuchanga sio shida. kwangu ni sawa/
Shida inakuja kwenye mchakato wa kukusanya/
Kuna njia zinatumika sio rafiki siziafiki/
Unashurutishaje na Unalazimisha vipi/
Tukumbushane hapa na kuridhia kabisa/
Kuwa kuchanga Ni muhimu ila sio lazima/
Unakuta mtu hamkuwa hata mkiwasiliana/
Hamkuwa karibu yapata miaka mingi sana/
Ila akitaka kuchangiwa utamskia umenitupa/
Nani? Usingekuwa na shida ungenitafuta/
Au Unaenda kulala no vurugu wala tabu/
Ukiamka Umeadiwa kwenye group la wasapu/
Mtu kutumia Common sense tu hapana/
Na Swala la hela ni swala sensitive sana/
*Mdundo unapiga *
Verse 2:
Na Michango ya siku hizi kiwango cha chini laki/
Na kwa mwaka sio mmoja au labda miwili basi/
Hata kufika tisa inaweza/
Kwa Sherehe tu kama mia tisa inakwenda/
Hapo kuna mingine inafuatana nyuma nyuma/
Imeachana sana Imepishana juma juma/
Unajikaza huku umetoa huku ahadi/
Ila wenye jambo lao hawawazi Ugumu wa hali/
wahamasishaji washavaa mabomu/
Michango sio vita kufatana mpaka home/
Mtu akiahidi kutoa ngoja tarehe/
Kukumbushana sio mbaya lakini ngoja na we/
Sio upige Simu zaidi ya moja per day/
Wachangishaji saa nyingine huwa wana nongwa mazee/
(Juzi) Walimvuruga mpaka dada angu Seche/
Akajikuta amewajibu hiyo michango vepe/
Hehee!! make hapo kwanza ncheke/
Mpaka kuwajibu hivyo walileta sana wenge/
Tunapenda kutoa tunapenda kushiriki/
Pole pole jama mnavyotupeleka hatumaindishi/
*Mdundo unapiga*
Verse 3:
Mi la kusema nasema Sijui mtalipokeaje/
Kuna Sherehe nyingine sio lazima wote waje/
Ni kuacha tu makuu kuyakataa majaribu/
Alika ndugu kadhaa na jamaa wa karibu/
Piga ka party flani na mziki kiasi/
Hakikisha watu wamekula na wasimiss vinywaji/
Hapo ndio uwezo wako umekomea sio kitoto/
Jiepushe na fedheha ndogo ndogo/
Kama mtu kashindwa kuchangia bahati mbaya/
Sio kuanza kumchukia na kumtakia mabaya/
Naskia mna majina flani flani hajachanga/
Siku akija kuomba mumkatae. washamba! /
Badala ya kuzidisha majungu mtulie tu/
Punguzeni sherehe bakisheni zile kuu/
Maana nimesikia wanalalama mtaani/
Kuwa Mkipata ka shughuli mnakafanya mtaji/
Sijui uongo au ukweli, mnajua nyie/
Mi Ninachosisitiza ni Pumzi Mtuachie/
Ustaarabu ni muhimu kila mchangishapo/
Na mbaki kwenye lengo kusudiwa la michango/
....