Beti ya kwanza:

Jambo Woteee...Jambo Woteee.. Jambo Wote..Jambo Wote

Jambo Wote, Mtu Mzima Nshawasili/
Na Leo Ntaongelea Tiba Za Asili/
Vuteni Viti Kwanza, Shikeni Biki Kwanza/
Andikeni Tiba Hii Inahusisha Mitishamba/
Yani Mimea Inayotumika Kama Dawa/
Iwe Majani Mizizi, Maua Mbegu Na Maganda/
Nafaka Na Gundi Na Kadhalika/
Pia Mpaka Matunda Yanahusika/
Vilevile Makundi Ya Vyakula Mbalimbali/
Hii Tiba Haihusu Dawa Zenye Kemikali/
Mbali Na Kukutibu Au Kukuweka Fiti/
Hufanya Na Kazi Ya Kujenga Mwili/
Na Inafanya Vyote Hivi Kwa Wakati Mmoja/
Hii Ndo Tiba Mama Tiba Nambari Moja/
Asilimia Sabini Ya Waafrika Waliitegemea/
Mapinduzi Ya Kisayansi Yalipofika Ikalegea/

Beti ya pili:

Ukiangalia Gharama Ni Ndogo Au Hata Bure/
Kachume, Kachimbe Kunywa Na Utafune/
Na Wala Hazidhuru Ukiyafuata Masharti/
Sasa Kimbembe Ni Kwenye Dawa Za Hospitali/
Mzee... Hizi Dawa Zina Bei/
Yani Utateseka Sana Bila Pay/
Mwili Ukizizoea Unakuwa Sugu Kwa Dawa/
Na Ukipona Ugonjwa Inabaki Sumu Ya Dawa/
Kwa Hiyo Inakubidi Ku Recover Mara Mbili/
Kaa Kijanja Ndugu Kaa Kwa Akili/
Chunguza Kipi Kina Madhara Makubwa/
Upunguze Maafa Na Hasara Zitazokuja/
Watafute Wajuzi Wa Tiba Hizi/
Sio Ushamba Jitafute We Mswahili/
Usishikiwe Akili Nature Imetubariki/
Imetupa Chakula, Mimea Yenye Tiba Nyingi/

Beti ya tatu:

Wazee Wetu Walituambia Kwamba Asili Imetimia/
Wao Walijifunza Na Kuitunza Miti Hiyo/
Ikawatunza Pia, Wakajitibia Magonjwa/
Umwa Chochote Dawa Unayopatiwa Unapona/
Tuwaombe Watujuze Na Sisi/
Tujifunze Kwa Wingi, Vyakula Na Miti/
(Yeah) Tuache Majivuno Na Ubishi/
(Kingine) Tubadilishe Na Mifumo Ya Kuishi/
Miti Mingi Tuko Nayo Mitaani/
(Mingi) Na Mingine Wala Haiko Mbali/
Muhimu Kuwa Na Mashamba Na Bustani/
Ili Isipotee Inatupasa Kuhifadhi/
Saivi Kila Kitu Dili, Naomba Nikuhabarishe/
Kuna Watu Wanatuibia Kwa Mgongo Wa U Herbalist/
Epuka Wizi Huu Kwa Kusaka Maarifa/
Hakikisha Na Kizazi Chako Kinarithishwa/