Beti

Mi Naianza Siku Niko Active/
Sijiskii Uvivu Niko Safi, Kabisa Niko Happy/
Ndo Maana Kwangu Kila Siku Ni Productive/
Raha Maradufu Furaha Na Uchangamfu/
Morale Morale Tele Nimejaa Yani Full Full/
Sahau Kuchoka Hovyo Hovyo/
Siugui Ugui Na Sipati Homa Ndogo Ndogo/
Nicheki Yo/
Nilivyo Mwepesi Nilivyo Flexible /
Very Strong, Singoji Ugonjwa Upenye/
Nishikiwe Mabango Au Dokta Aseme/
Najua Mazoezi Ni Afya/
Ni Faida Kufanya, Na Hasara Ya Kuyaacha/
Yamenijenga Body Na Fikra/
Yamenibadilisha Niko Tofauti Kabisa/
Nilikuwaga Mzembe Kama Wewe/
Siwezi Hata Kushika Jembe Kama Wewe/
Push Tatu Ni Kimbembe Kama Wewe/
Lakini Saivi Mwana Niko Shega Kwenda Mbele/
Jikaze Mwanzoni Kuwa Na Discipline/
Mwisho Utazoea Sababu Huwa Ni Addictive/
Sikushurutishi Nakuacha Peke Yako/
We Unayeogopa Ukitazama Age Yako/
Mazoezi Kama Elimu Tu, Hayana Mwisho/
Na Sio Lazima Gym, Au Sehemu Flani Official/
Kijana Unalala Afu Wazee Wanapasha/
Eti Hutaki Kuchorana Huwezi Kwenda Kwa Uwanja/
Ni Tatizo, Si Unapasha Hata Indoor/
Mazoezi Yako Mengi Mengine Kufanya Simpo/
Na Hii Story Ya Tajiri Ndo Apashe Kaleta Nani/
Zoezi Ni Kwa Wote Tunapaswa Tuwe Ngangari/
Mbarikiwe Nyie Ambao Mmetenga Muda/
Hata Dakika Tano Tu Zina Maana Kubwa/
Ambao Kila Asubuhi Tunapishana Rodi/
Au Mida Ya usiku Tunapofanya Jogging/
Big Up Sana Aminia Amanaya/
Tuendelee Mpaka Mwisho Kukazia Kama Kawa/

Kiitikio

Kama Unabeba Vyuma Kabebe/
Kama Unacheza Rhumba Kacheze/
Ukiona Kukimbia Hauwezi/
We Tembea! Hata Kutembea Ni Zoezi/
Wale Wa Basket Na Football/
Tiririkeni Kwa Viwanja Kwa Fujo/
Mazoezi Ya Viungo Kwa Sana/
Karukeni, Waruka Viunzi Na Kamba/
Wale Wa Kuogelea Ka Samaki/
Haina Kuremba Kata Maji/
Piga Ma Push Up Piga Ma Squat/
Wa martial Art Miksa Miksa Ma Karate/
Miksa Sarakasi, Ki Acrobatic/
Oya Haya Mazoezi Yako Shazi/