Beti Ya Kwanza
Kuhusu Wanawake Na Elimu Siha/
Swala La Hedhi Huwezi Kuacha Kuligusia/
Na Maswala Kama Haya Kwenye Hii Dunia Tulipo/
Huwezi Kusema Kwamba Kuyazungumzia Ni Mwiko/
Yeah! Yapaswa Kujiuliza/
Ni Kipi Bora Zaidi Ya Afya Na Uzima/
Iwe Mashuleni Iwe Sehemu Za Kazi/
Wanawake Hupata Sana Changamoto Za Usafi/
Kwenye Midogo Na Vijiji/
Huko Ndiko, Kuna Changamoto Mara Mbili/
Na Hupelekea Kushindwa Kufanya Kikamilifu/
Kazi Na Masomo Ushiriki Unakuwa Hafifu/
Hivyo Pedi Ni Hitaji La Msingi/
Kila Mmoja Anapaswa Kujitahidi/
Naamini Kivyovyote Hatuwezi Kukwama/
Kumsaidia Mlengwa Kwenye Hedhi Salama/
Beti Ya Pili
Na Malengo Mnayoweka/
Msisahau Hoja Ya Upendo Peneza/
Mkitoa Elimu Bure Mzingatie Hii/
Kwenye Kila Shule Pedi Zigawiwe Free/
Sababu Hedhi Sio Kila Siku/
Hedhi Ni Siku Chache Kwa Mwezi So Sio Issue/
Ya Kuifanya Serikali Ishindwe Kugawa Bure/Na Kupelekea Wasichana Washindwe Kukaa Shule/
Ukifanya Hesabu Ya Haraka/
Utapata Ni Vipindi Mia Nne Kwa Mwaka/
Ambavyo Watavikosa Sababu Ya Shida Hiyo/
Na Mahudhurio Kupungua Ni Tatizo/
Itadumaza Ustawi Wa Elimu Ya Mwanamke/
Serikali Yangu Inabidi Mchangamke/
Najua Kuwa Mnajua Ila Nitarudia/
Ukimwelimisha Yeye Umeelimisha Dunia/
Beti Ya Tatu
Hata Wale Wanaobaki Na Kukaa Majumbani/
Bado Hali Zao Sio Salama Sio Shwari/
Vitu Wanavyotumia Kujisitiri Sio Uhakika/
Kuna Hatari Ya Kupata Maradhi Na Kudhurika/
Why Wakose Raha Na Kukumbatia Unyonge/
Ee, Wakati Hedhi Sio Ugonjwa/
Mimi Naona Kama Miyeyusho/
Yani Binti Asiwe Huru Kisa Uhaba Wa Taulo/
Na Haishindikani Pedi Kuwepo Kila Kona/
Haswa Kule Ndani Ndani Zipelekwe Za Kutosha/
Wanaozua Wapunguziwe Kodi Iwe Poa/
Bei Ishuke Na Bidhaa Ziwe Zenye Bora/
Salute Kwa Dada Flaviana/
Taasisi Yako Inafanya Makubwa Safi Sana/
Sisi Kwa Wingi Wetu Hatushindwi Kuchangishana/
Na Kufanya Pedi Ziwe Rahisi Kupatikana/