Unao
Sina Muda, Dah Niko Bize!
Ina Sound Poa Ee? Nimeona Nikuulize/
Unaambiwa Ndo Mambo Yalivyo Siku Hizi/
Ila Amini Kwamba Hilo Jibu Ni Tricky/
Wataalam Japo Sijui Wa Taaluma Gani Ila Ndio Wanavyoitwa/
Wanakwambia Inategemeana Na Nani Kauliza/
Au Ameuliza Saa Ngapi Na Ni Sehemu Gani Alipouliza/
Kama Umemuita Mtu Na Akakwambia Hana Muda Inawezekana Kwamba Amekutosa/
Bila Sababuuu Au Ana Vitu Vya Muhimu Zaidi Na Hivyo Ulivyomuitia Sio Muhimu Yani They Are Not Important/
And Vice Versa Is True/
Ila Ukweli Unabaki Constant Kama Nyeupe Ni Nyeupe Na Blue Ni Blue/
Jibu Ni Jibu Bwana/
Na Kama Ulitaka Jibu Si Umejibiwa Ama? /
I Wish Ningekuwa Mwingi Zaidi/
Maana Mambo Ni Mengi Muda Mchache Sijui Nini Na Nini/
Samahani, Ni Kweli Hauna? Really? Hivi Huoni Mkuu?/
Kwamba Siku Yako Ina Masaa Kumi Na Mbili Maana Inaishia Jioni Tu?/
Na Ulikubali Kwamba Siku Ina Saa 24/
Mi Sitaki Kuingia Sana Huko Kwenye Kwa Nini Saa 24, Au Nani Aliweka Hizo Saa 24/
Ni We Mwenyewe Unasemaga Kuwa Likishachwea Ndo Siku Imeisha/
Vipi Hayo Masaa Kumi Na Mbili Ambayo Unakuwa Umeyabakisha?/
Ni Kweli Huwezi Kufanya Kitu Chochote Productive Usiku? /
Au Ndio Binadamu Anatakiwa Alale Walau Masaa Nane Kwa Siku? /
Na Hapo Hapooo, Je, Hiyo Time Ndo Unaingia Kitandani Kulala? Jibu No.. /
Au Unakuwa Umetulia Ukitafakari Na Kuwaza? Jibu No.. /
Aisee!! Sasa Saa Hiyo Unakuwa Wapi?? Tiktok!!!/
Eeeh Haya Bwana Ila Hapo Ulipo Kumbuka Kuwa Saa Nayo Ina Tick tock.../
Ujue Unaposema Hupotezi Muda Kizembe Zembe Hiyo Haipingiki Man/
Ila at The Same time Kukaa Bure Tu Eti Unangoja Muda Uende Ende Mmmh Hiyo Haingii Kichwani/
Sikatai Kauli Yako Kuwa Hii Mitandao Isingekuwa Na Maana Basi Isingekuwepo/
Nakubaliii Ingia Mtandaoni Ingia Sana Kama Una Viporo Si Utavifanya Kesho/?
Puuza Wahenga Waliosema Liwezekanalo Leo Lisingoje Kesho/
Au Wakati Ni Ukuta Ukipigana Nao Utaumia Chukulia Kama Msemo, Au Ikiwezekana Uone Ni Kama Kichekesho/
Saa Zingine Unaacha Kupewa Madili Au Mambo Mengi Ya Msingi/
Kwa Sababu Gani? We Mwenyewe Huwa Unasema Una Mambo Mengi Ya Msingi/
Mfano, Hujawahi Kuskia Au Kuambiwa, Kuna Mishe Ya Hela Ilijitokeza/
Nikawaza Nikucheki Maana Ungeiweza/
Ila Nikasema Sidhani Maana We Binafsi Una Mambo Mengi Kwa Hivyo Kivyovyote Hutoweza Kutokea/
Ikabidi Niangalie Nani Ambaye Yuko Chap Akaja Akakomesha/
We Hauna Muda Sio...Je Yule Ambaye Anaona Siku Nzima Haimtoshi?/
Kwa Sababu Ana Vitu Mlima, Mpaka Anaamua Kucheki Watu Wengine Na Kuwaomba? /
Wampe Muda Wao Ili Wamfanyie Mambo Yake Ambayo Hajayamaliza? /
Tena Anaingia Gharama Na Kuwalipa, Kwa Lugha Rahisi Wanaita Ajira?/
Na We Uliyeajiriwa Mfanyakazi Ambaye Unalipwa Hizo Noti/
Ambaye Ukishalipwa Ukija Mtaani Sisi Ma jobless Tunakuita Boss/
Huko ofisini Kwako Si Ndio Unajifanya Huna Muda Ili Usipewe Kazi Nyingine/
Unajichelewesha chelewesha Kwa Kigezo Cha Kufanya Kazi Kiumakini/
Na Kazi Yenyewe Haufanyi Kihivyo Wala Nini Budah../
Zaidi Zaidi Unalalamika Tu Na Kutumia Muda Mwingi Kusema Hauna Muda/
Hata Upande Wa Pili, We Uliyejiari Unaweza Ukawa Una Vitega Uchumi/
Ni Kweli, Sababu Unaingiza Chochote Kitu Ila Kiuhalisia Ni Kwamba Unavitega Na Hauchumi/
Cheki, Labda We Ni Mjasiriamali/
Una Duka Lako Mahali/
Umejiwekea Ratiba Kuwa Mwisho Wa Kuuza Ni Saa Flani/
Na Hiyo Saa Ikifika, Hata Wateja Wakija, Unawaambia Muda Umekwisha/
Huwahudumii Unarudishia Unakipa/
Na Unapita Mitaa Flani/
Huenda Sio Mbali Na Duka Lako Ni Km Mita Flani/
Unawaona Wateja Hao Hao Wanahudumiwa Wanalipa/
Kumbe Jamaa Hafungi Duka Muda ukifika, Ye Anafunga Wateja Wakiisha/
Sijamaanisha Kuwa Hautakiwi Kupumzika/
Ila Inafikirisha Kama Mapumziko Yako Yatakuwa Chanzo Cha Hasara Na Sio Faida/
Sina Muda.. Hii Kauli Inaweza Kuwa Inazuia Sana Maendeleo/
Na Kama Tafsiri Yake Ndio Kama Hizo Hapo Juu Tutazidi Kufeli Kama Itaendelea/
Maana Inakuwa Haijabeba Kitu Chanya Zaidi Ni Kuharibu/
Kuna Jamaa Yangu Aliniambia Sisi Ni Maskini Kwa Sababu Tunastahili Kuwa Hivyo/
Kitu Kidogo Tu Utaskia Muda Uliniishia/
Au Kuna Vitu Viliingilia, Nikajikuta Nimepitiwa/
Waafrika Tumekuwa Watu Wa Sababu Nyingi Kupita Uhalisia/
Wote Tumepewa Muda Sawa/
Ila Shida Inakuja Unapofika Muda Wa Kuugawa/
Na Ndio Hapa Yanapotokea Matabaka Mbalimbali/
Ma Gap Ya Kiuchumi, Kipato Na Maswala Kama Hayo/
Kuna Watu Watautumia Vile Na Wengine Watautumia Hivi/
Tupo Tutakaouchezea Na Wapo Watakaoutumia Kiusahihi/
Na Hawa Ndio Tulikuwa Tunawatania Wametumwa Na Kijiji/
Tunajikuta Ma Born Town Halafu Wenyewe Wana Kijiji/
Kipindi Tuko Chuo Au Sekondari/
Tulikuwa Tunaenda Zetu Party/
Huku Wenyewe Wanasoma Kiusongo/
Si Tunachoma Na Kuzinywa Si Kitoto/
Hatuna Muda, Tunawaka Na Kuzima Chocho/
Halafu Pepa Zikija Tunaanza Kuzima Moto/
Halafu Kwenye Chumba Cha Mtihani, Ndo Tunakumbwa Na Mtihani/
Tunacheza Na Mikakati/
Formation Za Kudesa Na Kutembeza Vikaratasi/
Achana Na Hiyo,
We Hujawahi Kuskia Mtu Anakwambia Saivi Bado Asubuhi/
Au Ntafanya ABC Ikifika Juma Ngapi Sijui/
Yani Kana Kwamba Ye Ni Noma Na Muda Unamngoja/
Hajui Kwamba Mipango Aliyopanga Inaweza Hata Ikavurugwa Na Ugonjwa/
Na Matatizo Huwa Yanashtukiza/
Hayana Simile Wala Hayana Kusubirishwa/
Sina Muda.. Imepoteza Fursa Kibao Kubwa Na Ndogo/
Imeua Matumaini Imeua Na Ndoto/
Sina Muda, Rahisi Kuitamka Ila Kuimaanisha Ndio Kazi/
Niko Sure Imevunja Mahusiano Shazi/
Na Ukisema Uko Bize Au Hauna Muda Na Mimi Au Yule Tukakataa/
Usinitafsiri Au Kututafsiri Vibaya, Kusema Labda Tumekudharau/
La! Point Ya Msingi Ni Kwamba Wewe Muda Unao/
Ila Kuna Uwezekano mkubwa Kuwa Bwana Mkubwa Unautumia Muda Vibaya/
Ndio Maana Sio Wote Ambao Utawaambia Huna Muda Na Wakakuona Kama Mshkaji Mwamba, Au Mshkaji Mjanja/
Kuna Wengine Wataona Kwamba Mshkaji Anakwama, Au Mshkaji Hajajipanga/
Usipanic!!! Sikiliza, Unautumia Vipi Muda Wako/
Yani Unakipa Kipi Na Unampa Yupi Muda Wako/
Isije Kuwa Unautumia Kwa Watu Ambao Wanakucheki Kwenye Free Time Yao/
Halafu Wewe Ili Uwacheki Una Free Time Yako/
Na Tatizo Linakuja Pale Unapohoji/.....
Kwamba Wanastahili Yani Do They Really Worth It/?
Sasa, Ukiwa Mwenyewe Au Ukiwa Peke Yako/
Chunguza Sana Hivyo Vipaumbele Vyako/
Nasema Hivi Sababu Muda Utakuja/
Ambao Kweli Utakuwa Hauna Huo Muda/