Beti Ya Kwanza

Hebu Fikiri Kuhusu Afya Ya Mwili/
Na Pili, Fikiri Kuhusu Afya Ya Akili/
Fikiri, Huna Ugonjwa Huna Hata Dalili/
Kamili, Yani Uko Fiti Kwenye Moja Na Mbili/
Kisha Fikiri Kinyume, Yani Turn Table/
Una Ugonjwa Unaumwa Yani You Not Stable/
Hata Kama Hujalazwa, Hujatundikiwa Dripu/
Lakini Hauko Sawa Unasumbuliwa Na Vitu/
Au Fikiri Kuhusu Amani Uliyonayo/
Umetulia Umeshiba Huna Njaa Hupigi Miayo/
Kisha waza Vita.. Na Migorogoro/
Hadi Kulala Unashindwa Hulitamani Godoro/
Na Vurugu Nyingine Tu Ama Usumbufu/
Hata Bila Mabomu Na Kushikiana Mitutu/
Fikiri Kuhusu Uhai Na Pumzi Unayovuta/
Kisha Wazia Ku Die Huna Pumzi Umekufa/

Kiitikio

Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/

Beti Ya Pili

Waza kuamka Salama Na Kufanya Mambo Yako/
Hakuna Kukwaruzana Kupigana Na Watu Wako/
Waza Mapungufu Yako Ambayo Bado Sio Kikwazo/
Cha Kuziba Njia Zako Unazopita Toka Mwanzo/
Iwazie Roho Yako, Kauli Na Matendo/
Afu Waza Unavyopata Kwa Hiyo Hali Na Mwenendo/
Fikiri Kwa Utulivu Kidogo/
Acha Vikubwa Fikiri Kuhusu Vitu Vidogo/
Vitu Kama Heshima Ama Kuaminika/
Au Kupewa Nafasi Ama Kutambulika/
...Kuwa Na Bega La Kuegemea/
Au Sikio Ambalo Unaweza Kulielezea/
Chochote.. Kile Ambacho Kinakusibu/
Kuwa Na Ndugu Wawe Wa Mbali Au Karibu/
Fikiri Na Vingine Ambavyo Sijasema Hapa/
Useme Why Unafikiri Kwamba Pesa Ndio Baraka/

Kiitikio

Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na Mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na Mali tu/

Beti Ya Tatu

Kwa Kuwa Hii Story Imenileta Kwako Leo/
Kuna Usemi Usemao Pesa Ni Matokeo/
Tunaujua Wote Wewe Na Mimi/
Ushajiulizaaa Pesa Ni Matokeo Ya Nini/?
Yani Umefanyaje Mpaka Ukashika Pesa/
Umeona? Baraka Ni Deeper Kuliko Fedha/
Haihitaji Hata Kuzama Kwenye Books/
Yeah, Rudi Nyuma Kwenye Roots/
Kisha Acha Kusema Hujabarikiwa/
Yule kabarikiwa, Na We Umebarikiwa/
Umebarikiwa Sana We Fikiri Yourself/
Usipime Kwa Noti Au Material Wealth/
Tena Kuwa Msaada Bariki Na Wengine/
Baraka Zako Zitazidi Mara Mbili/
Na Hichi Ndicho Mi Nilichobarikiwa/
Pokea Baraka Hii Aminia....
Baraka Tele...