Hip Hop inanguzo tano; emceeing, graffiti, breakdancing, beatboxing na deejying na japo kua mashabiki wengi wa Hip Hop wanaifahamu sana nguzo ya emceeing au kughani hizo nguzo zingine hua wanazisahau au hata hawajui kama zipo!
Nikiwa natafuta wakumhoji ili niweze kuandika makala yanayo ongelea nguzo ya graffiti/art au sanaa kwa Hip Hop Seth Odhiambo alisogezwa kwangu na wimbi la kisulisuli la mtandao wa kijamii Facebook. Kazi yake nilipoiona pale Facebook na Instagram moja kwa moja nikaona lazima nimkaribishe kwenye jukwaa letu ili tumfahamu vizuri pamoja na kazi yake nzuri ya digital art.
Sanaa ya Seth Odhiambo “Skchr” imejikita sana kwenye mziki wa Hip Hop ambao ni kama chakula chake cha kila siku. Nawa mikono usogee tunapokula nae kwenye sinia lililo jaa mapochocho kibao ya Hip Hop na sanaa.
GURU(RIP) na DJ Premier wakiunda kundi la Gang Starr
Kaka, karibu sana Micshariki Africa. Tueleze historia yako kwa ufupi, jina lako rasmi na unajishughulisha na nini kimaisha?
Shukran sana. Jina langu rasmi ni Seth Odhiambo. Nashughulika na uchoraji wa vibonzo ikiwemo vibonzo vya wasanii wa hiphop, graffiti, nembo (logo), uchoraji wa majalada ya albamu(album covers), michoro ya kuchapisha kwa t-shirt, michoro ya vitabu na kadhalika. Kazi ya ualimu pia nafanya lakini si ya kufunza uchoraji ni masomo mengine katika shule ya msingi.
Nilizaliwa na kulelewa Changamwe mjini Mombasa, Kenya na kusomea shule ya msingi na upili ya St. Lwanga hadi kidato cha pili ambapo tukahamia nyumbani Kisumu wakati babangu mzazi alipostaafu kwa kazi yake aliyokuwa anaifanya.
Ulianzaje uchoraji?
Uchoraji nilianza nikiwa shule ya upili na nakumbuka tukiwa vijana watatu katika darasa letu ambao tulikuwa tumejaliwa na vipaji vya uchoraji ila wenzangu hawakuvikuza vipaji hivi kama nilivyofanya mimi. Kipaji changu nilikikuza polepole kadri nilivyo zidi kukua.
Kule shule ya upili ndipo nilianza kuvutiwa na uchoraji wa vibonzo na katuni wanaohusika na Hiphop. Nilikuwa nachora kila pahali si nyuma ya vitabu si kwa madawati na ilifika wakati uchoraji wangu ulianza kufanya nizorote kimasomo ikabidi nitulie kwanza nishughulike na masomo ili nifaulu mitihani yangu.
Baada ya kumaliza masomo ya shule ya upili mwaka wa 2001 ndipo nilirudia uchoraji tena nikipanga vile maisha yangu ya baadaye yangekuwa.
Jina lako la uchoraji Seth Skchr ulilipataje na lina maana gani?
Jina la Seth Sketcher lilikuja kutokana na mapenzi yangu ya kuchorachora kila mara. Nilipokutana na Bankslave mara ya kwanza katika hali ya kupiga gumzo aliniuliza jina langu (tag) as a graffiti artist nikamwambia ni Sketcher hapo ndipo aliniuliza "Huoni kuwa ni hilo jina ni refu?" Wakati huo sikulifikiria sana swala hili lakini baada ya siku kadhaa ndio wazo la kufupisha jina toka Sketcher hadi kuwa Skchr likanijia. Kwa hivyo hilo ndilo lkawa jina langu la usanii hadi leo na sioni nikilibadilisha.
Kwa nini uliamua kuwa graphics designer/digital art designer?
Uamuzi wangu wa kuwa designer ulikuja kutokana na mvuto wa michoro ya Hip Hop niliyoiona. Mimi ni mpenzi wa Hip Hop tangu zamani. Chochote kilichohusika na Hip Hop halafu kina michoro fulani kilinivutia iwe ni nembo za vikundi kama vile Bad Boy Records, Luniz, Def Squad, ni baadhi ya michoro iliyonivutia.
Kuna tofauti gani kati ya digital art na kazi za michoro ya mikono?
Sioni tofauti kubwa na michoro mingine ila tu katika digital art ni rahisi kuwasilisha kazi kwa mteja.
Ofisi yako ya kazi ipoje? Huwa una bonge la studio au ni laptop tu?
Hehehe, hamna ni mimi na laptop au tablet yangu tu! Kuwa msanii wa digital ni msanii tu ila vyombo muhimu ninavyovitumia ni kama tarakilishi au Ipad au tablet yoyote ile halafu pamoja na software za uchoraji kama vile ProCreate, Sketchbook Pro, Adobe Illustrator, Photoshop, Medibang na kadhalika.
Kwenye shughuli hii ya graphics designing ni kipi kimekugusa sana kwenye ujuzi wako waku kubuni?
Katika shughuli zangu za ubunifu kile kinachonigusa sana ni kuwa ubunifu huu hunilisha mimi na familia yangu, yaani nafurahi sana kuwa naweza kutumia kipaji nilichojaliwa na Mwenyezi Mungu kujikimu kimaisha.
Kazi yako hunuia kusema nini ?
Kazi zangu hunuia kuonyesha mapenzi yangu ya dhati kwa Hip Hop.
Kazi yako inatoa maoni gani juu ya maswala ya sasa ya kijamii au kisiasa?
Huwa sipendi mambo ya siasa kwa hivyo utakuta kazi zangu hazilengi huko na sio kwamba sioni yanayoendelea nchini kwangu la hasha, ila sipendi tu kujishughulisha nayo. Ni Hip Hop naipa muda kwani ndiyo hunilisha na kunivisha!
Je ni nani alikuvutia sana kwa mambo ya designing na kukupa hamasa ya kuwa graphics designer? Pia ni nini hukupa hamasa na motisha ya kubuni?
Hamasa na motisha ya kubuni michoro yangu hutokana sana na muziki wa hiphop. Naweza sikiliza ngoma flani halafu mstari flani au punchline flani hivi yaweza nipa wazo nitengeneze mchoro unaohusiana nao. Si hayo tu...siku zinaposonga pia mawazo mapya huja.
Tueleze kidogo kuhusu kazi yako, ni nini unahitajika kuwa nacho ili uweze kufanya kazi hii vizuri?
Ili mtu aweze kuifanya kazi hii vyema kwanza kabisa anapaswa kupenda uchoraji. Pili, usiifanye shughuli hii ukitarajia utatajirika, wakati mwingine chombo huenda mrama, waeza kosa wateja uone ni kama wapoteza muda wako! Cha tatu, chukua maoni ya wakosoaji wako positively (kwa njia chanya), ukiweka kazi yako mtandaoni na mtu asipo Like au asiponena jambo, wewe songa mbele na uendelee kubuni tu, wacha kazi yako inene yenyewe. Mwisho naweza sema usiilalie bahati ya mwenzio, usitake kuwa kama mtu mwengine, ng'ang'ana uwe wewe na mtindo wako na zidi kuboresha kazi zako kila siku iitwayo leo na pia usijiinue, usiwe na kiburi wala kujifanya mjuaji! Nyenyekea, wacha kazi yako ikuinue.
Umekuzaje kipaji hiki hadi kimekupa ajira?
Imenichukua miaka mingi ili kazi hii iweze kunipa ajira. Sikuwa na uwezo wa kununua vyombo vya kufanya kazi za digital art mwanzoni. Nilikuwa nachora kwa penseli na kwa karatasi tu na watu waliipenda michoro yangu kama Ilivyo. Na jambo hili lilinipa nguvu za kutaka kujiendeleza zaidi Hadi kuna wakati rafiki yangu aliponipa graphic tablet niitumie. Wakati huo pia nilipata tarakilishi yangu binafsi. Nikaanza kujifunza kuitumia polepole tu na miaka nenda miaka rudi nimejikuta mahali nilipo kwa sasa.
Je unapataje fursa za kazi?
Ili nipate fursa ya kazi, kama nilivyosema hapo nyuma ni kazi yangu kwanza ndio inanena. Msanii akieneza kazi yangu mtandaoni wengine wanaiona na ndivyo taarifa kuhusu kazi zangu zinaposambaa halafu wale wanaonijua na pia wanao ona kazi zangu wakisikia mwenzao Ana uhitaji wa kazi za uchoraji wanampa mawasiliano na ndivyo ninavyozidi kupenya kila pembe.
Pia social media ama mitandao ya kijamii imezidi kuniwezesha kuwafikia wasanii wengi wa Hip Hop. Mtandao wa Instagram umeniwezesha pakubwa sana kwenye hii kazi kwani kupitia njia hii nimeweza kufanya kazi na ma emcee kama vile kundi la Snowgoons toka Marekani.
Ilikuwaje hadi kufikia kufanya kazi na ma emcee wa Hip Hop? Umeshawafanyia kazi akina nani nje na ndani ya Kenya?
Wasanii wengi japo si wote nitakaowataja ambao nimefanya nao kazi ni kwa mfano SoulMate na Ace Tha Don toka Kenya ilhali nje ya Kenya ni kama vile Gillateen (majalada yake manne ya albamu zake nilimfanyia (shoutout kwake)) na bado tunapanga kufanya kazi nae hivi karibuni.
Pia kuna Planet Asia, Ghost of The Machine na Dj Proof, albamu ya DLP & Denzil Porter kutoka Bronx, albamu ya DLP & iNTeLL (2nd Generation Wu) ambaye ni mwana wa U-God (mmoja wapo wa kikundi maarufu cha Wu-Tang Clan), albamu ya Quantum Physics, albamu ya Supreme Celebral, albamu ya Ant Milli. Wote hawa wapo America.
Kuongezea pia kuna wasanii wengine nimewachorea majadala ya singles pekee hasa Dj Proof, Mack C, King Gems The Artist, King Magnetic, Vioxii Dedee (toka Kenya), na kadhalika.
Pia siwezi kumsahau Moe Hendrix (America) ambaye amenipa kazi nyingi sana huyu na itakuwa kufuru mimi kutomtaja.

Cafu Da Truth(toka Kenya) ulipataje fursa ya kufanya naye kazi kwenye mradi wake Mambo Kavu EP?
Cafu naye tulipatana kwa njia ya Facebook na WhatsApp.
Seth aliunda jalada la EP ya Cafu Da Truth, Mambo Kavu EP
Je ulishakaa pengine kule America na nchi za ughaibuni? kwani unaonekana umefanya kazi nyingi sana na ma emcee toka huko
La hasha! Sina na sijawahi hata kumiliki passport sembuse kuishi America (akicheka)!
Kazi zako hupatikana kwa bei gani?
Kwa upande wa bei sina bei ya maalum kwa sababu mtu anaweza taka kazi ambayo ni ndogo na ndani ya dakika thelathini nishaimaliza, hapo siwezi kumwambia atoe elfu ishirini za Kenya. Kwa hivyo mimi huweka bei kulingana na inayoihiaji mteja. Ikiwa ni kazi itakayonifanya nijikune kichwa sana nikiwaza na kuwazua cha kufanya bei lazma itakuwa juu kidogo.
Pia Kwa upande wa bei kuna jambo fulani ningependa kulizungumzia, Huwa nina bei tofauti kwa ajili ya wateja wangu toka Kenya na wa nchi za nje, sababu? Uchumi wetu si kama wa nje.
Kuna wakati nilifanya kazi na DJ flani wa majuu akafurahishwa sana na kazi yangu hadi yeye mwenyewe akaniambia hiyo bei nilimpa ni ya chini sana. Kwa hivyo aliniongeza pesa mwenyewe. Kazi niliyomwambia anipe dola hamsini alinipa mia moja na hamsini. Kwa hivyo nikaona kuwa wateja wa marekani na nchi nyinginezo bei zao zipo tofauti ndipo nikaamua bei za huko ziwe tofauti na nyumbani.
Kwa Kenya mi huchaji Ksh. 3500 tu na akitaka kuongeza sitokataa (akicheka)!
Hawa walio majuu/mamtoni hukulipa kwa kupitia njia zipi?
Wa nchi za mbali hulipa kwa kutumia PayPal ama MoneyGram.
Shughuli ya kumchorea mteja hukuchukua muda gani mpaka umalize?
Inategemeana na concept au wazo ninalolifanyia kazi. Kama ni kazi kubwa ninaweza kuchukua siku kadhaa ila kama mchoro ni wa mtu Peke yake na sina shughuli nyingine huwa ni kazi ya siku moja au mbili.
Wewe hupenda kuskiliza mziki gani unapofanya kazi zako?
Wasanii ninaowasikiliza kwa sana ni wa Boombap au Underground Hip Hop wawe ni wa miaka ya tisini ama wa miaka ya juzi, bora tu ni emcee wa Boombap ngoma zake nazikaribisha sana masikioni mwangu!
We unadhani ma emcee wa Hip Hop waliopo handakini wanaweza fanya nini ili wazidi kuonekana na mziki uendelee kuwalipa kama ma emcee waliopo handakini kule America?
Muziki wao unapaswa kuwa na quality ya hali ya juu. Kwa mfano unaweza pata msanii ana mawazo mazuri katika wimbo wake ila vile anavyoyawakilisha mawazo hayo kwenye kinasa sio vizuri sana kwa msikilizaji na hapo anakosa soko.
Nimependa sana albamu ya Fikrah Teule(Azania Na Wanawe) na Kaa La Moto(KESI) kwani hizo albamu ni za viwango vya hali ya juu sana. Toka Tanzania ma emcee ambao wana kazi za viwango ni akina Nash MC, Dizasta Vina na kadhalika. Hawa niliyowataja miziki yao huwa ya viwango vya juu, asilimia mia moja!
Mchoro wa Kaa La Moto Kiumbe toka kwa Seth Sketcher
Je hakuna wabunifu kama wewe kule America wanaofanya kazi hii?
Wapo wengi mno na wanafanya kazi safi sana.
Changamoto za kazi zako ni zipi?
Nikiwa huku kuna vitendea kazi fulani bado sina ila nikivipata kazi itakuwa bora zaidi na bei itaongezeka. Pia wateja wengine wasumbufu wamenifanya huwa nadai kulipwa kwanza kabla ya kuanza kazi kisha nimtumie kazi yake kwa njia ya email.
Ni nini tofauti yako na wale ma designer waliopo America kinachowavutia hawa ma emcee wa mamtoni kutaka kufanya kazi na wewe?
Kazi zangu zanena zenyewe na pia mimi huhakikisha nimewasilisha kazi ndani ya muda na hata ikichukua muda mrefu huwa nasikilizana na mteja kabisa mapema. Sipendi scandals kwenye kazi zangu!
Una ushauri gani kwa digital artist anaeanza?
Yeyote anayeanza kazi hii aipende kwa moyo wake wote iwe inamlisha au la!
Mpate Seth "Sketcher" Odhiambo kupitia mitandao ya kijamii:
Facebook: Seth Skchr
Instagram:sethskchr