Wimbo: Pesa
Toka kwa: Shilinde
Albam: Single
Tarehe iliyotoka: 14.02.2022
Muunda Mdundo/Mtayarishaji: Producer Baba, Prof. Ludigo
Studio: The African Dream

Beti Ya Kwanza

Jinsi unakuja, na jinsi unasepa/
Unaleta hisia kwa jinsi unateka/
Jinsi unatega hisia, watu wanaasi/
Katu hawataki wakukose, watu wana nafsi/
Wanasemezana vilivyo, kisha ni kasi/
Ya kukufuata kila ulipo, hatua ni ngazi/
Washuke wapande, wanakunyakua kwa chati/
Kuna majambazi, wakikichafua ni kazi/
Ukipatwa, visa mikasa, hawashibi wanasaza/
Wengine wakipata upenyo hawalipi wanakacha/
Unaleta tamaa, wengine huvuka mipaka/
Wanakuwa vibaka, wanaungua wakidakwa/
Unapendwa wewe, sio mtu na utu/
Popote upo, we ni noma, huko na huku/
Unathamani hata kama mfuko una buku/
Anazini kapuku, yea milupo anamudu/

Kiitikio

Money money
More money, more problems (Pesa)
More money, more problems
Money money
More money, more problems (Pesa)
More money, more problems x2

Beti Ya Pili

Mabinti wanajiajiri, mtaji ni mwili/
Sababu ni wewe, huh! ulaji ni siri/
Kula kulala gharama, mahitaji kabili/
Watoto wa mama unawafanya wawe makafiri/
Wanasaini kwa siri, ajili wapate utajiri/
Hawa watu, unawafanya wawe makatili/
Kufa kufaana, unawapa tafsiri, wanafanya madili/
Yakiwalipa hutupa maadili/
Kila kukicha ni msako hadi watabiri/
Wanafanya yao wakupate, unawapa akili/
Upo nje upo ndani, ya dini wahubiri/
Kuna sadaka, mwenye maswali subiri/
Mitini tumbili, huku ni wingi wa sifuri/
Mbele ya 1 mpaka 9, michongo huwasili/
Wengine wakisepa nawe husomwa albadiri/
Msako huanza mapema inapojiri alfajiri/

Kiitikio

Money money
More money, more problems (Pesa)
More money, more problems
Money money
More money, more problems (Pesa)
More money, more problems x2

Beti Ya Tatu

Unafichwa overseas offshore, Pandora Papers/
Unalimbikizwa hasa, kodi wanakwepa/
Una majina mengi, ushuru ni pesa/
Kufuru ni pesa, TBT njururu ni pesa/
Vipande vyako vilifanya Yesu akamatwe/
Vijana wengi, naskia unafanya wapakatwe/
Ubadhirifu unakuhusu, rushwa ni wewe/
Dada zangu wanahonga ngono kisa ni wewe/
Ukikata kabisa wapenzi husepa wenyewe/
Ukirudi wanarudi tena, nacheka mwenyewe/
Ukijiachia ni msala, ukikoswa kiwewe/
Ukipatwa hata kifaranga ukimuona ni mwewe/
Kamari imehalalishwa, sababu sio mimi/
Hamlali ajili ya pesa, watafutaji ndio nyinyi/
Kuzaliwa mpaka kufa, unahusika vilivyo/
Mwanzo mwisho tupo active kufa likizo/

Kiitikio

Money money
More money, more problems (Pesa)
More money, more problems
Money money
More money, more problems (Pesa)
More money, more problems x2