Maarifa - "Haikuwa Rahisi"

Msanii: Maarifa ft. Dudy Sound
Wimbo: Haikuwa Rahisi
Album: Single

Uandishi na kurekodi

Uandishi wiki 1…….Kurekodi Miezi 4.

Kama jinale linavyosadifu,haikuwa rahisi kurekodi “Haikuwa Rahisi” kweli.

Mchakato wa kurekodi wimbo huo haukuwa rahisi kwani ulikumbana na changamoto kadha wa kadha. 

Asilimia kubwa ya wimbo imetayarishwa na Pallah (Midundo), ambaye ameandaa mdundo na pia amefanya mixing ya wimbo huo, Isam kwa upande wake amepiga vinanda na Abby Mp amesimamia uingizaji wa sauti. Kifupi ni kwamba, kama sio ubize bila shaka mpango mzima ungekamilishwa na Palla, lakini changamoto ya kwanza ilikuwa kwa Palla kutokuwa na studio rasmi ya kufanyia kazi na hata pale Studio ilipopatikana bado muda ukakosekana.

Saa, siku, wiki na hatimaye miezi ikakatika, Palla hakuwa na muda wa kutosha kuweza kukamilisha wimbo huo. Mara kadhaa ratiba za kurekodi zilivurugika au kuingiliwa na ratiba za kazi zake nyingine. Mbali na uandaaji wa muziki Palla ni muajiriwa, hivyo kuna muda haikuwa rahisi kwake kujigawa hasa alipobanwa sana na ratiba za ofisini.

Maarifa akaona sasa ni vyema mtayarishaji mwingine ahusike, akamuomba Palla na baada ya kupewa baraka kiroho safi mzigo ukasongeshwa kwa Abby kuingizwa sauti na mwishoni ukarejeshwa kwa Palla kufanyiwa mixing, hatimaye wimbo ulioandikwa kwa wiki moja ukarekodiwa kwa miezi 4.   

Turudi nyuma kidogo, Mwaka 2014 Maarifa alikuwa ameshaandika nyimbo kadhaa, moja ya nyimbo hizo aliita jina la “Safari” wimbo ambao baadae ndio ukaja kufahamika kama “Haikuwa Rahisi.”

Toka “Safari”, “Acha Story Iendelee” mpaka “Haikuwa Rahisi”

Haikuwa rahisi ni wimbo wa pili kutoka kwa Maarifa, wimbo wake wa kwanza ni “Maarifa Ya Maarifa”. Changamoto katika kufanikisha kibao hicho cha Maarifa ya Maarifa zilikuwa zinakatisha sana tamaa lakini alifanikiwa na ndipo changamoto zote alizokutana nazo aliziandika katika “Simulizi Ya Ukweli”. Simulizi hiyo Maarifa aliipa jina la“Haikuwa Rahisi” jina ambalo baadae sasa ndio likavikwa wimbo wa 

“Safari”

Kubadilika kwa jina toka Safari mpaka Haikuwa Rahisi kulienda sambamba na kubadilisha baadhi ya mashairi na hii ni kwa sababu, simulizi ya“Safari" ilimuelezea yeye binafsi kipindi anaandaa wimbo wa “Maarifa Ya Maarifa” lakini wimbo wa “Haikuwa Rahisi” unaelezea changamoto za jamii nzima. Kwa maana hiyo unaweza kusema Haikuwa Rahisi ni matokeo ya ujumbe kuhusu safari ya binadamu katika kutafuta ustawi wa maisha yake, ujumbe ambao ulisimuliwa na simulizi ya kweli iliyoelezea changamoto alizokutana nazo msanii huyo kipindi anaanda wimbo wa Maarifa Ya Maarifa.

Ndivyo ilivyokuwa,Haikuwa Rahisi lilionekana jina zuri kwa ujumbe husika kuliko jina la Safari na labda pia kuliko hata jina la “Acha Story Iendelee” jina ambalo nalo kuna muda lilipendekezwa katika mashairi hayo ya Safari.

Sasaaaaa mambo yakawa mambo, Maarifa akakamilisha kuingiza mistari so ikabaki kazi tu kwa Belle 9 kuja kurekodi chorus kama yalivyokuwa makubaliano.

30/07/2016 ndio siku hii track ya Haikuwa Rahisi iliachiwa rasmi kumbuka tarehe 30 June ya 2017 ndipo ikatoka Tupilia Kule, ikiwa ni wastani wa kutoa ngoma moja kwa mwaka

Wimbo wa Haikuwa Rahisi msingi wake ulikuwa ni changamoto ambazo msanii huyo amekutana nazo kipindi hicho anaandaa wimbo wa Maarifa ya Maarifa lakini cha ajabu wimbo wenyewe wa Haikuwa Rahisi nao haukuwa rahisi vilevile nao ukaleta changamoto zake kiasi naona nao unahitaji kutungiwa haikuwa rahisi yake.

Mgoma ukawa unasubiri chorus, Belle 9 akawa bize bize na ikumbukwe hadi hapa ilishafika miezi 4 ya usumbufu wa hapa na pale, ikawa hakuna namna tena ya kusubiria ikabidi achekiwe Soprano ili aje kushika chorus, bahati mbaya naye ratiba zake zilikuwa nyingi hapo sasa Producer Abby MP akamwambia DudySound kukamata chorus.

Upatikanaji wa Dudy ulikuwa rahisi tu vile ni msanii anayefanya kazi na Abby MP. 

Mapokeo ya wimbo kiujumla yalikuwa ni mazuri tu.vile kwa muda mfupi mgoma ulifikia watu wengi mno.

Haikuwa Rahisi ni wimbo ambao unahusu kila hatua ya Maarifa katika pilika zake za kimuziki lakini pia unamuhusu kila mwanadamu katika harakati zake za maisha na zaidi wimbo unachagiza kuhusu nidhamu, uvumilivu na kutokata tamaa pale tunapoelekea malengo yetu pia wimbo unachochea hali ya kujifunza na kuthubutu katika maisha yetu ya kila siku.

Mcheki Maarifa kupitia;

Facebook: Maarifa BigThinker
Instagram: maarifabigthinker

Pia mcheki Iddy Mwanaharamu mwandishi wa makala haya kupitia;

Facebook: Iddy Mwanaharamu