Shobi Mzawa

Msanii: Shobi Mzawa
Wimbo: Mke Dalali

Simulizi Ya Wimbo 'Mke Dalali' kutoka Kwa Shobi Mzawa

Mke Dalali ni wimbo wa kipekee sana, unahitajika kusikiliza kwa utaratibu ili kung'amua ujumbe kusudiwa wa wimbo huo. Ubunifu huu umefanya wimbo huu kuwa wa kipekee sana. Karibu usome mahojiano yangu na Shobi Mzawa kuhusiana na wimbo huo.

Karibu shobi mzawa kwa segment hii ya NYP na leo tutachagiza mawili matatu kuhusiana na wimbo wako wa Mke Dalali.

Ahsante sana brother.

Kabla ya yote ningependa kujua namna ulivyoipata idea ya Mke Dalali.

Wazo nililipata mwaka jana mwezi wa 12. (Mahojiano haya yalifanyika mwaka 2017 mwezi wa 7), Kikubwa kilichochochea kupatikana kwa wazo ni mzunguko wa pesa, lakini wazo halikuwa la moja kwa moja...!!

Uandishi wa wimbo huu ulitumia muda gani?

Nilitumia wiki 1, na niliandika kila jioni baadhi ya mistari. Nilipendelea mazingira ya utulivu sababu wimbo wenyewe umekaa kihisia.

Je, ni changamoto gani ulizokutana nazo katika utafutaji ndio zikaleta wimbo huu?

Mke Dalali sio simulizi ya kweli bali ni njia kuu ya kuifunza jamii kupitia taswira halisi.

Nani producer wa wimbo huu na ushiriki wake ulikuwaje katika kuijenga hii track?

Producer wa wimbo anafahamika kama Producer P, ndiye aliyetengeneza N.M.B ya Wazawa The Ink hivyo ikanisukuma nifanye naye tena kazi kwa mara ya pili, ushirikiano ulikuwa mkubwa sababu ali appreciate kazi na ameisapoti sana.

Vipi kwa upande wa mapokeo na malengo kusudiwa?

Mapokeo yamekuwa makubwa kiasi cha kuniongezea mashabiki hata wa nchi jirani na ujumbe umefika ipasavyo hivyo hata lengo limefika kwa uzuri kabisa.

Kwa upande wa changamoto, kuna namna yoyote ile imekupata?

Changamoto zipo, kwanza kwa mashabiki, kwani wengi wao wanahisi wimbo unamhusu mwanamke.

Hii kwa upande wangu pia imenifanya nijue jinsi gani uandishi wangu umekua. Changamoto pia ni kuwa ilinibidi niiandike sehemu tulivu, kitu ambacho sijazoea. Kwenye kurecord hakukuwa na changamoto yoyote.

Kuna chochote cha kujivunia kuhusiana na track hii?

Sana tu, cha kujivunia kipo sababu baada ya kutoka Mke Dalali nimekuwa nikitafutwa na baadhi ya wasanii kwa ajili ya collaboration, pia imefanya baadhi ya emcees wanipe heshima yangu.

Namna hii ya kuelezea pesa kama mwanamke flani hivi asiyetulia ni so fantastic aisee!

Hahahahaha ndugu hii ni sanaa, nimechukua uandishi wa mgongo. Sikupenda kila msikilizaji anielewe kirahisi ndio maana nikaanza kama namuimbia binti mrembo kumbe wala!!

Mke Dalali ni wimbo wako wa ngapi?

Ni wimbo wangu wa tatu, ndio wimbo wa kwanza pia kuufanya bila kiitikio. Imeweka heshima yangu eneo langu na kunifanya niwe FINEST kweli (KOROGWE FINEST)..!!

Lolote la kumalizia…

Wadau watambue tu kuwa mke dalali inahusu pesa na sio mwanamke kama wengi walivyodhani...!!

Pia mcheki Iddy Mwanaharamu mwandishi wa makala haya kupitia;

Facebook: Iddy Mwanaharamu