Adam Shule Kongwe -Nyumba Yangu

Msanii: Adam Shule Kongwe
Wimbo: Nyumba Yangu
Album: Fasihi Simulizi

Kama kawaida msomaji wa segment hii ya Nyuma Ya Pazia tunakutana tena na tena this time tuko na Adam Shule Kongwe na tutazungumzia kuhusu wimbo wake wa ‘Nyumba yangu’

Twenzetu…

Niaje Kongwe?

Fresh kabisa bro, lete habari…

Nyumba Yangu ni moja kati nyimbo zangu pendwa wa muda wote, ndio maana nikaona sio kesi bob tuizungumzie hii track ili nipate mawili matatu. Kwa kuanza, idea ya nyumba yangu ilikujajekujaje?

Nakumbuka nilikuwa geto (Singida) nikisikiliza midundo na ilikuwa midundo miwili niliyosikiliza sana siku hiyo ambayo ni Affirmative Action na People's Champ lakini niliishia kuurudia mdundo wa people's champ wa Apollo Brown na Oc, huku nikichana chana verse nyingi nyingi kuamsha mizuka.

Yap yap! Nakusoma bob, hebu tuendelee sasa hapo ndio mizuka ishapanda mzee unachanika mbaya, ikawaje mpaka ikaja Nyumba Yangu? Uandishi wake labda na issue ka’hizo?

Sasa wakati naendelea kukiamsha Ghetto alikuja mwanangu (Hamisi) nikatoka kumcheki baada tu ya salam nikamwambia kuna wimbo unaitwa Nyumba Yangu, nauandaa nikampa lines kadhaa nilizokuwa nimezichora tayari, akacheka akaniambia limalizie hilo P litakua noma, tukaendelea na story nyingine.

Kawaida huwa sipangi niandike nini ila huwa napitia mistari haswa ninayoandika mmoja mmoja au vipande kwenye simu sasa kuna mistari miwili nilikuwa nayo ambayo ni: “Nawakilisha wanangu wanamjua mtu wao/Nipo tangu na tangu si unajua mtu kwao? /” Nikaona hii niitafutie kitu, sasa hapo ndipo lilipokuja wazo la “Nipo tangu na tangu wapi? Underground!”

Lakini sitaki iende wazi wazi tu nikaitafutia njia isiyo ya moja kwa moja, nikaona sasa hapa niwakumbushe na watu niliowaaminia (waliokula hela zangu kwa namna yoyote ile kwenye muziki na utamaduni kwa ujumla, huenda ikapunguza hasira ya yale yaliyonipa mshangao wa wao kukacha njia sahihi).

Kwa MC akishapata pa kuanzia mara nyingi huwa ni rahisi kumalizia kilichobaki, hivyo ndivyo Nyumba Yangu ilivyojengeka bro.

Ni lini hasa wimbo huu ulirekodi na mzunguko mzima wa kuandaa mpaka kukamilika ulikuwaje?

Ni kati ya May 28 na 29 nilipoenda Dom kushiriki kwenye album ya Fasihi Simulizi mwaka 2016 na nilirekodi ndani ya masaa manne tu ila siku za kuandika ni kama 5 hivi, maana mizuka ya kuandika ikija huwa siandiki wimbo mmoja lakini mdundo huwa mmoja naweza andika ngoma hata 5 kutumia beat moja.

Vipi harakati za kurekodi na ushirikiano wa producer siku hiyo?

Producer ni Bin Laden (yule Laden kabla hajaanza kutekwa) aisee tulikua tunafanya beat selection usiku wa kama saa mbili sasa alipo play beat na kuifikia hiyo, LC(Lucas Malali) akaniambia hili beat linakufaa japo hata sikumwambia nafanya ngoma gani, nikaingia booth huku nikisema hii ngoma nayofanya itaitwa Nyumba Yangu.

Sikupata shida maana beat kama ilikuwa inaningoja mimi na nilipiga Take 1 tu kila ubeti, watu walikuwa wanacheka tu si unajua mizuka? So, ushirikiano wa producer ulikuwa mkubwa sababu huwa sisumbui booth.

Hii ngoma umefanya mwenyewe, haikukupendeza kumuweka mtu kwa collabo?

Unajua huu wimbo nilitaka niufanye nikiwa Singida na kuna mdogo wangu mmoja wa kitaa huwa anarap anaitwa Emmanuel au Wesa P, nakumbuka nilimpanga dogo Wesa afanye chorus sema akawa anachelewa chelewa kuleta chorus na alipoileta sikuipenda nikaona ntafanya mwenyewe tu.

Daah! ule mchorus ni baab kubwa aisee, uliichoraje choraje ile kitu ?

Nilipanga wimbo wangu uitwe Nyumba Yangu, nikatafuta nyimbo zenye maneno yenye nyumba yangu au kuhusiana na hayo nakumbuka nilipata :You Ain't Got No Wins In Mi Casa(Redman), House Of Hits (KRS One) na ile We In Da Houuuuse kwenye wimbo wa Roc Boys wa Hov) lakini hata hivyo hayakuwekwa, producer akaniambia nipige chorus ya kawaida ambayo niliipiga ilikuwa (Nipo ndani ya nyumba na nna nyumba ndani yangu/nyumba ya wachache hii sio nyumba ya kila mtu /Nawakilisha wanangu wanamjua mtu wao /nipo tangu na tangu si unajua mtu kwao/)

Huu wimbo unapatikana kwa albamu gani?

Upo kwenye album ya kundi langu DDC “Fasihi Simulizi” niliuweka humo sababu uliendana na title na maudhui ya album kwa hiyo ni wimbo wa kundi.

Nini hasa ujumbe wa wimbo huo?

Ujumbe ulikua ni kujivunia nilipo (mtu kwao) na kuwaambia wana bado tupo na tunawakilisha ukizingatia kilikuwa ni kipindi cha watu kuacha uhalisia au zile walizotuaminisha ni asili) na kuwakumbusha yaliyowakuta waliowatangulia kimuziki baada ya kuacha njia.

Mapokeo ya wimbo yalikuwaje?

Aisee kuhusu mapokeo watu wengi waliupenda japo wengine mpaka sasa hawajui niliongelea nini, criticism zilikuwepo ila nachoshkuru ni kwamba mistari iliyomo ilikuwa inamaliza utata.

MF Straton aliwahi kuandika "Nyumba kama haina kuta imara wala msingi na haijakidhi vigezo sio nyumba ni kiota cha ndege" nilimjibu akaniambia niangalie isiwekewe X, nikamwambia hilo sio suala jipya maana" wenye fitina walishakuja"

Hahahaaaa! Vipi kuhusu malengo? Tumeyafikia ama laa?

Lengo lilifikiwa mpaka wanangu wananiambia aisee hawa waliohama njia inabidi wasikilizishwe hii, maana wapo wanaojirudisha kiaina wakati "Kama ilikushinda hapo awali/raundi hii sipangishi hata ukitimba na dalali/

Kuna changamoto yoyote ulikutana nayo katika mzunguko mzima wa uandaaji wa hii ngoma?

Hakuna changamoto niliyoipata aisee maana wimbo ulikuwa kichwani, labda tu chorus ya kurap kuna namna haikukaa sawa mwanzo, na yale maneno ya kwenye ngoma za mbele kupigwa chini…Iliniuma ila sio kivile

Lolote la kumalizia?

Wasanii ambao wapo underground (au wanaoamini wapo underground) waangalie na kusoma vizuri walipo, huku hamna ubabaishaji wala kuyumba, wausome vizuri utamaduni, maana kuna madogo wanatumia hadhira ya underground kutafutia tagi kisha waende wanapojua wao, majina tunayo tunawaangalia tu.

Pamoja sana Kongwe…

Asante arif…

Pia mcheki Iddy Mwanaharamu mwandishi wa makala haya kupitia;

Facebook: Iddy Mwanaharamu