Snaidah Don Dada

Anajiamini kuwa msanii hodari kwa sababu ya uwezo wake wa kutamba na kuwa mbunifu juu ya aina yoyote ya mdundo. Hili linaonekana katika nyimbo kama vile Can Gerrit (prod. by Motif Di Don), Madiba na Najiskia (prod. by Kingpheezle ).

Pia ameshiriki katika miradi mbalimbali kama vile Door Knockers Cypher Episode 3, Female Hip-Hop Edutainment Cypher pamoja na kufanya kazi na wasanii tofauti.

Hivi majuzi aliachia 'Black Whisper' EP ambayo inapatikana kwa urahisi kwenye majukwaa yote ya uuzaji wa muziki wa kidijitali na nyimbo zake nyingine nyingi zinaweza kupatikana kwenye chaneli yake ya YouTube.

EP yake ya 'Black Whisper' ina nyimbo tano:

  1. Kulala
  2. Ushuhuda
  3. Female Mcees
  4. Wakatae
  5. Kanyamo

Akiongelea mradi wake wa hivi majuzi, BLACK WHISPER EP, anasema alichagua hilo kama jina la EP yake ili kuonesha mwanga kuhusu matatizo ya kiakili aliyokuwa akipambana nayo baada ya kumpoteza babake. Hii imeoneshwa kwenye wimbo wake 'Ushuhuda.'

Mradi wa Black Whisper umejaa uhalisi ambao hauwezi kughushiwa. Hizi ni nyimbo zinazosaliti tishu za kovu. Nyimbo za kutafakari na za utambuzi. Kunaweza kuwa na minong'ono ya giza, lakini Snaidah anakuonesha na kukuelewesha kwamba hauwezi kushindwa. Kuna hasara nyingi sana na hakuna faida ya kutosha, lakini maadamu kuna imani juu ya kujiamini na kitu cha kina na uwezekano wa kitu bora zaidi, tumaini linabaki hai.

Kwa hivyo Snaidah Don Dada huunda muziki unaogusa mioyo, kuibua hisia na hisia fiche ambazo zitawatia motisha na kuwatia moyo wasikilizaji wake.

Karibu Micshariki Africa, Snaidah Don Dada. Majina yako rasmi ni yapi na unafanya nini?

Majina ni Mutswenje Snaidah Tsiavoka. Mimi ni Femcee na mwalimu kwa taaluma.

Tuambie kuhusu jina lako la kisanii Snaidah Don Dada, lilikujaje na linamaanisha nini?

Don katika kamusi ya kiingereza lina maana ya mhadhiri wa Chuo Kikuu... Nilisomea elimu hivyo nikachagua Snaidah Don Dada kuashiria kuwa mimi ni mwalimu wa sauti.

Tupitishe safari yako ya muziki, ulianzaje na safari imekuwaje hadi sasa?

Nilishiriki kwenye shindano (challenge) ya Motif Di Don 'Cangerrit ' na kwa bahati nzuri nilishirikishwa kwenye wimbo rasmi wa Motif Di Don... Huu ulikuwa mwanzo mzuri kwa safari yangu ya muziki. Safari imekuwa na heka heka lakini mapenzi na usanii wangu yananifanya niendelee. Kufikia sasa ni nzuri sana kwani mrejesho kutoka kwa mashabiki wangu yananikaribisha na hapo hapo yananifanya niendelee.

Tuambie kuhusu tukio lako la kwanza la kurekodi, ni wimbo gani ulirekodi kwanza? Kazi ile iipokelewaje na wale walioisikiliza?

Wimbo wangu wa kwanza ulikuwa wimbo unaoitwa Fresh na nilifurahi sana nilipoingia booth ya studio na kwangu ilinipa hisia ya kipekee kwani ilikuwa mara ya kwanza kusikia sauti yangu kwenye beat. Nilishindwa kujizuia kuweka wimbo uchezwe tena kama mara mia 😂🤦 ‍ ♀ ️.Majibu kutoka kwa mashabiki yalikuwa chanya kwa hiyo nilijihisi matawi ya juu na nilizidi kujiamini zaidi kama kama msanii chipukizi na wa kike.

Hip Hop ni Utamaduni wenye vipengele tofauti ndani yake. Kwa nini uliamua kujiunga na Utamaduni huu na ni nini kilikusukuma kuwa mchanaji wa Hip Hop?

Uhuru wa kujieleza ulikuwa ajenda kuu mezani. Mimi ni mtu mwenye mengi ya kusema kwa hivyo nilichagua kuwa mchanaji wa kike katika Hip Hop ili tu mtu yeyote asiwahi kuninyamazisha sauti yangu au kuigeuza kuwa mwangwi. Kuweka hekima katika akili za wasikilizaji wangu lilikuwa lengo ndiyo maana nilichagua femceeing .

Muziki wa Hip Hop ni mgumu sana kwa wanaume na wanawake kupenya lakini ni mgumu zaidi kwa wanawake. Ni nini kinachokusukuma kuifanya badala ya kufanya aina nyingine kama RnB na Afro Pop?

Nilikuwa naishi kati ya ndugu zangu wawili ambao ni wa kiume...Kwa hivyo kukua karibu nao kulinifanya niwe ngangari pia... Unaweza kusema ni upendo mgumu wa kaka na dada... Kwa hiyo hurahisisha kunyumbua mapigo katika hali ngumu na kuwa na moyo huo mgumu na mawazo ya kuwa na subira, kudumu na kuweza kuhifadhi changamoto zote zinazoletwa na kuwa mwanamke. Hip Hop inanipa uhuru wa kujieleza kwa kuwa ni vuguvugu la akili, ndiyo maana nilichagua kufanya kazi yangu ya muziki kama msanii wa Hip Hop na si kama msanii wa Afro Pop au Rnb .

Je, ni akina nani baadhi ya wachanaji wa kike nchini Kenya na ulimwenguni kote ambao hukupa motisha ya kuwa mchanaji?

Nchini ni Nazizi, Stellah Mwangi (STL), Petra, Femi One… mamtoni ni Rapsody, Young M. A, Nicki Minaj, Beanz, Savannah Hannah, Lady Leshur na Latto .

Je, ni changamoto zipi kuu ambazo umekumbana nazo katika safari yako kama mwana Hip Hop na umewezaje kuzishinda?

Kuvunja kikwazo cha Wakenya kufurahia muziki wa Hip Hop ni vigumu kwa kuwa wengi wamenaswa na kelele nyingi na muziki usio na maudhui.

Kwa hivyo kwa sasa ninafanya kazi ya kutangaza nyimbo zangu za Hip Hop kibiashara ili wasikilizaji wangu wa Kenya waweze kuzisikiliza na kuburudishwa.

Unyonyaji wa kijinsia. Ninachagua kuwa thabiti na mwenye kanuni kama msanii wa kike na kukataa kwa mnyanyasaji yeyote wa ngono ambaye anataka kuniwinda kwa jina la kuinua talanta yangu.

Vikwazo vya kifedha. Lazima nishughulikie ili kupata pesa za kuwekeza kwenye sauti na video zangu. Au nyakati fulani watu wanaonitakia heri hufadhili miradi yangu ya muziki.

Ukosoaji na hukumu. Kuna watu wamekuwa wakihisi kama vile mimi ni msagaji. Hili linatoka na mimi kuchana kwa nguvu kwenye midundo hadi mtu anaweza dhania nina nguvu za kiume 😂. Kwa hivyo nilichagua kubaki kiziwi kwa hukumu na ukosoaji wa watu na hiyo inanifanya niendelee.

Masoko. Ni ngumu kwa upande wangu kufanya nyimbo zangu zifikie umati mkubwa kwa vile pesa zinahitajika hivyo nimekuwa nikitafuta majukwaa ya kutumbuiza ili tu nipate kukuza idadi ya mashabiki wangu na wakati mwingine huwa ni kazi ya kanisa kwa sababu huwa silipwi 🤦 ♀ ️

Tuambie kuhusu katalogi yako ya muziki, umetoa miradi gani hadi sasa?

Nimeachia nyimbo sita kamili kwenye chaneli yangu ya YouTube: Kulala, Testimony Female mcees, Wakatae, Kanyamo na Fresh .

Pia nilishirikishwa kwenye nyimbo mbili za Kingpheezle (Madiba na Najiskia) na Motif Di Don akanishirikisha kwenye Challenge yake ' Cangerrit ' .

Tuambie kuhusu EP yako uliyotoa hivi majuzi, Black Whispers . Ilikuwa inahusu nini na ni nani walikuwa watayarishaji na wasanii walioshirikishwa kwenye mradi huo? Je, ilikuwa ni hatua gani muhimu kwako kutoa EP hii?

Kutoa EP kumenifanya niwe na mtandao wa watu wengi wenye mapenzi mema ambao wako tayari ku support muziki wangu hasa baada ya kusikiliza EP yangu. Black Whispers inajumuisha nyimbo tano Kulala, Testimony, Female Mcees , Wakatae na Kanyamo ). Hizi zote ni nyimbo zinazozungumzia matatizo yangu ya kiakili baada ya baba yangu kuchomoa betri. Nilipata msongo wa mawazo ila muziki ndio ulinifanya niendelee. Kwa hivyo nilitaka kugusa roho za watu kupitia muziki wangu kwa hiyo kuungana na wasikilizaji wangu kupitia wimbo wangu wa maneno kwa kuwaambia ukweli wangu kwa rangi nyeusi na nyeupe (black and white) kwa hivyo nilitengeneza EP ambayo iliweka kila kitu bayana bila ya kuficha chochote. Hakukuwa na wasanii walioshirikishwa kwenye EP na watayarishaji ni Motif Di Don, Cobra, Buju Da Beast na Brouser .

Ulishiriki katika kipindi cha 3 cha Door Knockers Cyphers. Je, uzoefu wako wa kufanya kazi na wasanii tofauti kutoka eneo hili ulikuwa vipi na cypher ilikuwa na athari gani kwenye kazi yako kama msanii?

Kipindi cha 3 cha DKC kilikuwa tukio la kujifunza. Ilinifanya kuwa na mawazo huru na kupata kujifunza jambo moja au mawili kutoka kwa wasanii wenzangu kutoka mikoa mbalimbali na ndio nilipata mtandao na kujitangaza na kwa sasa kwa hisani ya Door Knockers Cypher Episode 3 nilipata maombi ya ushirikiano kutoka kwa wasanii kutoka Uganda, Tanzania na Diaspora.

Je, una ushauri gani kwa rappers wajao haswa wanawake wanaojaribu kutafuta njia ya kutoka katika tasnia ya muziki?

Kinachohitajika ni uvumilivu, uvumilivu, uvumilivu, shauku, maombi na kujiamini kama msanii. Na jambo lingine ni kutowahi kuruhusu mtu yeyote kukufanyia unyonyaji wa kingono kwa jina la kukusaidia kuinua talanta yako ya muziki. Mwishowe, ili uwe mtangazaji mzuri, sikiliza magwiji ambao watakuweka sawa kama msanii.

Wasomaji wetu wanaweza kukupata wapi kwenye mitandao ya kijamii?

YouTube: Snaidah Don Dada
Instagram: @snaidah_don_dada
Facebook: snaidah Don Dada
TikTok: snaidahdondada
Twitter: Snaidah Don dada

Mawazo ya mwisho na shukran kwa yoyote yule?

Shukran zangu ziwaendee nyie Micshariki Africa kwa kumtambua Snaidah Don Dada. Mahojiano haya yana maana kubwa kwangu na ninahisi kuheshimiwa na kunyenyekezwa hwa hili. Kwa hivyo Micshariki Africa, jisikieni kuwa mmethaminiwa.