Toka kwa: Solo Thang
Wimbo: Miss Tanzania
Mradi: Single
Tarehe iliyo toka: 10.07.2012
Mdundo: Tongwe Records
Mchanganya Sauti na Mdundo: Roof Recordz

Beti Ya Kwanza

Baba yake alikua mkoloni kipindi huyu miss mwali/
Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari/
Sababu alikua busy kumlinda na geti kali/
Kumbe wenzake wanabinjuka kushtuka kakaa mbali/
Demu alikua na heshima kabla haijatangwazwa rukhsa/
Chukua chako mapema ukimkonyeza tu umegusa/
Ana kifua kimebetuka sio maziwa ni madini/
Kayaacha wazi watu wanashika hapo ndio anaponiudhi mimi/
Watu wanagonga tu ikulu tena kwa mitindo huru/
Kavu kavu bila kinga hajali vinavyodhuru/
Kawa shangingi na amedata hana uwoga wa kunguru/
Anapenda sana chapaa haimtoshi kodi na ushuru/
Ana kijungu matata laini kama nyanya masalo/
Anatingisha Afrika nzima na mzigo Kilimanjaro/
Usimchezee kwa vidani sio pete sio hereni/
Anamiliki tanzanite kama ardhi ya Mererani/
Sura dhahabu inaita kama amezaliwa Geita/
Tatizo ndio kicheche kila mwanaume ndio amepita/
Hata Benja hakutoka kapa huyu demu hajatulia/
Kama rushwa ndio kikwapa ananuka na kunukia/
Miss Tanzaniaaaa/

Kiitikio

Nakupenda ila hujatuliaa/
Vitendo vyako sitojivunia/
Sifa yako kubwa umefulia/
Miss Tanzania/

Beti Ya Pili

Bora angebaki kuwa modo kama Flavian Matata/
Ila demu amejiachia kisa anaendekeza bata/
Sitachoka kuwakilisha jinsi anavyoniacha hoi/
Juzi juzi kaopolewa na handsome boy/
Kabla hapo shoga zake wote kashawaona mabwege/
Sababu hawana dira na yeye ameshahongwa ndege/
Anafaa kua miss dunia maandalizi longolongo/
Tatizo anakula sana akijamba ni Songosongo
Mara ghafla kanenepa kumbe mimba B.O.T/
Kumbe demu aligawa EPA watu wamepiga hafu jii/
Alizugwa na akaunt hewa kuwadi bwana Bilal/
Mara mdomo nae kazimwa bila hata picha ya kaburi/
Kinachomponza huyu shawty utulivu sifuri/
Ila hakuna anaepinga kwamba huyu demu ni mzuri/
Mixer siasa na biashara demu ameshakua chotara/
Mishe za dar akimaliza mjengoni anakwenda lala/
Kadri miaka inavyokwenda demu anazidi fulia/
Kumbe weupe ni mkorogo ona mwili sasa umefifia/
Demu kazidi umalaya wacha mabwana wamteme/
Haogopi kuliwa mtungo kisa nagawa umeme/
Miss tanzaniaaaa/

Kiitikio

Nakupenda ila hujatuliaa
Vitendo vyako sitojivunia
Sifa yako kubwa umefulia
Miss Tanzania

Beti Ya Tatu

Wadaku walishamfuma anakula denda na Richmond/
Dowans akazidi kete akamvisha pete ya diamond/
Binti maskini akanasa bwana mshenga ndio Lowassa/
Shemeji hataki hata picha ndio tabia gani sasa/
Ndoa ilifungwa kwa vifijo vigogo wakala Pizza/
Keki nzima wale wao share yetu si ni giza/
Sio hayo demu ana mengi ya kuchukiza/
Mali ghafi ashazinadi forsale anajiuza/
Mtaani ilivuma rumor demu kawa mama huruma/
Uchumi umefungwa drip maemdeleo ndio kali homa/
Mali asili ndio kitasa kila ufungo ndio unapita/
Toka alipovunja ungo nusu karne imeshapita/
Mapenzi kafanya mradi anamegwa na mafisadi/
Amani kwa time bomb binti amekumbatia radi/
Vitendo vyake vibaya vinafanya adharaulike/
Tabia katiba sio msahafu ndio useme isibadilike/
Mikosi inayomkuta ndio kwanza anatabasam/
Hajali waliomzunguka kama nao binaadam/
Mbagala walimbaka mpaka akamwaga damu/
Na juzi Gongo la Mboto kaanza kujamba mabomu