Wimbo: Mzee
Toka kwa: Songa
Mradi: Mitaa Flani
Tarehe iliyotoka: 08.12.2023
Mtayarishaji: KTB
Mixing & Mastering: Mdach
Studio: Sound Garage

Songa

Kabla hujanipa mic mzee/
Kata simu kata simu niko site mzee/
Nianze kuzungusha lines kama bike mzee/
Na zote zinatick kama Nike mzee/
Mbele ya pesa wanangu washageuka maiti mzee/
Piga kazi usichoke wanao waishi mzee/
Kwakuwa hawafanyi unachofanya watahisi ni rahisi mzee/
Pambana leo golden chance haiji twice mzee/
Tunaishi ndoto zetu hatuoti night mzee/
Kwa kuwa maisha si mchezo wote tuna fight mzee/
Kuna muda mpaka ukitapika naona ni showoff bei za vyakula zilivyo tight mzee/
Jinsi Maisha hayako fair siku hizi mpaka yanantia hofu, wengine wana njaa wengine ni diet mzee/

Ukisubiri usikilizishwe kila ngoma utaskia mbovu, mziki mzuri inabidi uusachi mzee/

Jinsi maisha yapo moto ni kama supu mzee/
Ishakata mwaka watu hawajala hata kuku mzee/
Usishangae tunatoa sadaka buku mzee/
Umeme tumeupata utata luku mzee/

Wengine mpaka wanawaza washike mtutu mzee/
Maana hakuna hata pembejeo za ruzuku mzee/
Hali duni muda wa msosi ni chukuchuku mzee/
Vijana ajira yetu kubwa ni tukutuku mzee/
Tunacheka usoni moyoni ni dukuduku mzee/

Vyuma vimekaza hamna kutu mzee/
Yale makali yanayokata sa hii ni butu mzee/
Game bado ni mbichi na hatujafuzu mzee/

Kwenye utelezi tunalipishwa hadi busu mzee/
Kama una roho nyepesi hukai huku mzee/
Hupati kitu mazima ni mwendo wa nusu mzee/
Kabari chocho nyembamba usijitusu mzee/
Na kuna watu wana kamba usiruhusu mzee/
Wote vichwa vigumu wamekaza fuvu mzee/
Vijana taifa la leo tuunge nguvu mzee/
Kwa maana umoja ni mali tuache uzuzu mzee/
Sio mpaka tushtuke pako patupu mzee/
Tuache roho ya kukunja tuwe na utu mzee/

Yani mpaka dagaa nae kauzu mzee/
Ukijiona una dhambi kunae Mungu mzee/
Kwenye shida na raha anifaaye ndio ndugu mzee/
Nataka nije niwe taita design ya sugu mzee/
Pembeni pisi iwe kali isiyo na gubu mzee/
Ntabaki kuwa wa moto sio vuguvugu mzee/
Maisha ni zaidi ya kucheza ngoma za dufu mzee/
Na bado mpaka wenye power nao wana uchu mzee/
Kiukweli ninapambana niweze fuzu mzee/
Nami nije Nionje sukari hata ya Zuchu mzee/

Mzee Noma!