Toka kwa: Sosa (Watema Nondo)
Nyimbo: Uhuru Wa Manyani
Album: Nondo
Tarehe iliyotoka: 09.08.2020
Muunda mdundo: Sigger
Studio: Paradise Apple

Kwanini watu wanateseka, hofu na pressure? /
Siri wasioijua duniani kutatua hekaheka/
Mungu yupo au ujinga una ogopa kucheka/
Hauwezi pinga money money kinga inayo ogopesha/
Unafunga una sali mbona Mungua hakujibu/
Unaumwa Mungu hajali kachuna wala hakutibu/
Unakufa na maswali ni hali isiyo na majibu/
Waovu wanafanya dhambi na Mungu hawaadhibu/
Mungu ni nani? Au nakufuru kiimani niache? /
Mungu ni nini? Ni mtego kichwani ulio pahala pake/
Kuhusu kumjua Mungu nadharia chungu za wachache/
Mungu mwenye hekima binadamu wote si wa kwake/
Unaumizwa unasamehe kisha unamuachia Mungu/
Unajiumiza aliyekuumiza mzee hamuogopi Mungu/
Mafungu ya adui yanawindana kama Chui na Nyumbu/
Visasi mpaka siku ya kiama mpaka roho ina ukungu/
Kuamini Mungu hayupo kiini cha kukata tamaa/
Haujapata ulichokiomba, labda unateswa na njaa/
Unachoona wajanja wanamtumia Mungu kukuhadaa/
Au rizki kwa mafungu tu Mungu huziandaa/
Watu wanachinja kesi wanashinda wanyonge wana dinda/
Huanzi vita wanapochoka kudhani Mungu atawalinda/
Wanaosema mtegemee Mungu wanakufanya mjinga/
Waendelee kukunyonya kukutawala wao wanashinda/
Anajilipua kisa ahadi peponi atabarikiwa/
Anaaminishwa furaha yake siku kanisa kunyakuliwa/
Sadaka ya maskini ndipo babake inapoliwa/
Akihoji na ile imani yake dhahiri inakadiriwa/
Shetani ni picha ya kiakili haudhan/
Jua hili anatumiwa ili wenye imani wasitoke gizan/
Shida ziko palepale kitaani bado hakuna aman/
Unahoji hivi Mungu ana mamlaka gan/
Kutegemea maajabu ni tumaini la mnyonge/
Alie tafsiriwa vitabu aviombe hadi tabu zisonge/
Akiamka babu hakuti dhahabu hata nusu kikombe/
Huku wajanja wanapeana madili wanawini kwenye pombe/
Vyovyote unavyo aminisha nafsi yako hua na nguvu/
Ukishawishi akili na utashi unaishi kwa nguvu/
Kama Mungu yupo ndani yako thibitisha kwa utukufu/
Njia za kusaka ukweli na picha za kuunga unga mkufu/
Kujadili kama tuko wawili na roho ya Dalai Lama/
Usiku mchana nasafiri kama maili za Vasco Da Gama/
Utakiri huenda Mungu unaemfikiria wewe si kama/
Mungu wa dini na Mungu wa njia za imani na kila namna/
Firauni hajaoza akiwa Kush waongoza uzush/
Waliotozwa kwa Jehovah matusi waliwaponza watu weusi/
Ujinga mahususi umewaponza kwa nyaraka za kugushi/
Hekima ya Mungu imetuwacha maskini mbumbumbu weusi/
Tulifanywa bidhaa tukauzwa na Mungu hatukumbuki/
Taharuki babu zetu walikua nyani si kwa chuki/
Leo mikia yetu mbona haionekani wale hairefuki/
Mbona imani zipo nyingi hata ukiwa mpagani haufi/
Mungu wa Biblia Yesu alizaliwa wakamtoa sadaka/
Wayahudi wakamuaharibia akalia “Mungu mbona umeniacha?”/
Bado hakumsaidia na vipi Mohammed akafa/
Pamoja na vita zote alizo pigana jihadi akiwa Mecca/