Karibuni sana Micshariki Africa jukwaa la Hip Hop linaloangazia taarifa, habari na miradi ya wana Hip Hop kutoka Africa Mashariki. Leo tuko Dar. Karibuni ili tuweze kumfahamu Swanga The Concious ni nani na anajishughulisha na nini.
Karibu sana kaka Swanga. Kwanza kabisa tuanze kwa kufahamu unaitwaje majina yako rasmi, unatokea wapi na unajishughulisha na nini?
Kwa majina naitwa Louis M Mpapa ni emcee mchenguaji katika utamaduni wetu huu wa Hip Hop na muziki wa Rap. Kiasili mi ni mtu wa Sumbawanga, Rukwa. Natokea Nkasi huko kaskazini magharibi lakini nimezaliwa Dar Es Salaam.
NB: Kama ungepeda kuskiliza Podcast ya gumzo hili lipo mwishoni mwa makala haya.
Tueleze kidogo kuhusu historia yako ya nyuma ya muziki.
Yeah, ukizungumzia historia yangu ya nyuma ya mziki ni ya kawaida tu kwa sababu mimi kabla ya kuingia kwenye rap game nilikuwa mchoraji mzuri tu. Niliwakilisha shule niliyokuwa nasomea na nimewahi kufika kwenye haya mabaraza tofauti tofauti ya sanaa kwa sababu ya uchoraji.
Nakumbuka nishawahi kuwakilisha shule kwenye baadhi ya projects za kijamii zaidi ambazo nakumbuka mradi huu ulifanyika Pugu Secondary na sisi au mimi ni miongoni ya wanafunzi kati ya wale watano ambao walibahatika kuwakilisha shule. Nafkiri ilikuwa mwaka 2002, kipindi hicho bado naendelea kuchora.
Baada ya kutoka kwenye uchoraji niliingia kwenye tasnia hii ya rap game.
Hili jina lako Swanga The Conscious Mind lilikujaje na lina maana gani?
Kabla ya kutumia jina la Swanga nilikuwa natumia jina la Mo Smart lakini kadri ninavyokua na aina ya harakati ninazofanya unatakiwa utafute jina unique ambalo linaweza ku fit kile ambacho unachofanya.
Sasa nilipokuwa nikipata nafasi kukaa na familia ya wazee mara nyingi walikuwa watu wa ku complain, “Ninyi hasa vijana mliozaliwa Dar Es Salaam mnakua mnapasahau kwenu kwa nini? ...sasa msije mkapotelea huko Dar Es Salaam. Msipasahau kwenu”. Kwa hivyo msipasahau kwenu ilikua kama kilio kilichonifanya kutafuta kitu kitakachonisaidia ku maintain kwamba muda wote nitakapokuwa nipo, chochote nitakachokuwa nakifanya basi nitakuwa napafikiria nyumbani kwa mda mwingi sana ndio nikapata neno la Swanga.
Swanga ni neno ambalo limetoholewa kutoka kwenye neno Sumbawanga, baada ya kupunguza herufi kwenye Sumbawanga kwa ufupi kidogo ndio tukapata neno Swanga.
Swanga mpaka sasa una miradi mingapi, hapa naongelea EP, Mixtapes na albums. Mimi binafsi nafahamu na nina nakala za EP zako mbili, Safari na Acha Moto Uwake?
Mpaka sasa nina miradi miwili ambayo nimeiachia official lakini still kuna mradi wa album ambao upo njiani mda wowote kuanzia sasa. Nina mipango ambayo naifikiria ikikaa sawa rasmi, hasahasa kwenye swala la ki marketing zaidi mziki nitauachia rasmi. Kwa hivyo bado niko katika ku negotiate kwamba niachie kama hard copy (cd) au niachie kwenye hizi digital platform zinavyokwenda ili kuona kwamba biashara inafanyika vipi kwa sababu kama unavyojua haya maandalizi tunatumia muda ku invest kwenye kiasi kidogo cha fedha, kutumia mda mwingi kuandika mashairi, recording sessions kwa hiyo kuna vitu bado havijanikalia sawa kwenye upande wa ku release album. Nataka nikifikia huko basi nione kuna faida.
Swanga nimeona kwenye pita pita zangu kwenye mitandao ya kijamii kuwa wewe pia ni “Emcee, Event Planner, Host”. Tueleze kuhusu hizi mbanga.
Kuhusu kuwa host na maswala ya event planning, mimi nafkiria hizi ni other side of my talent sio kwamba ukafikiria mtu alikaa akaenda shule kusomea hivyo vitu hapana. Hivi vitu vimekuja kwa sababu mda mwingi huwa nimebahatika kuhusika kwenye matamasha mengi na kuhusika katika sehemu kubwa ya uandaaji wa baadhi ya matamasha watu huwa wanachukua sana ushauri kutoka kwangu katika kuendesha baadhi ya shughuli. Kwa hiyo nikaona why not, kwani mimi sometimes ninakuwa natumika sana kwenye baadhi ya mambo ya watu bila kupewa credit na ndio maana nikaamua nijiite Event Planner, kwa sababu naweza kuratibu jambo na kuweza kulisimamia na likawa kama vile tulivyolitarajia na kutaka kuwa.
Kuwa Host pia nafkiria ni upande wa pili wa talanta ambayo Mungu amenijalia kuwa nayo na ndio maana pia naifanyia kazi kwa kipindi hichi. Hivyo ni vitu vilivyo kwenye sehemu ya maisha yangu ya kawaida.
Pia kuna harakati unazojihusisha nazo kama “Watch Kama Ikulu” na “Knowledge & Movement Hip Hop Cypher”. Hizi harakati mbili zinajihusisha na nini?
Kuhusu Watch Kama Ikulu na Knowledge and Movement hii ni miradi yangu pia mikubwa miwili ambayo nilibahatika kuifanya na kuisimamia kwa nafasi yake lakini sikufikia malengo yake. Bado tuko katika hali ya kuendelea kupambania vitu hivyo kama tulivyovitazamia.
Hii Watch Kama Ikulu lengo lake kubwa nataka iwe taasisi ya mtu binafsi ambayo inajihusisha hasa na shughuli za kijamii kwa sababu sisi tunatoka katika hii jamii ya chini sana kwa hivyo ni vingi ambayo tunaviona, jamii inahitaji msaada. Kwa hiyo as an emcee ambae ana nafasi pia ya kuisimamia jamii yangu nilikua najaribu hili kwa wepesi zaidi, najaribu kuwa na mawazo chanya kuwa naweza nikafanya kitu ambacho jamii ikanufaika nacho na wakaja sema Swanga alikuwa anafanya hip hop ila kuna kitu alitufanyia sisi wanajamii hata kama sio katika eneo ambalo nililo zaliwa lakini jamii kiujumla.
Kuhusu Knowledge and Movement Hip Hop Cypher, hii basically iko katika kuishi na kuenzi utamaduni wa Hip Hop na kikubwa nikawa napambana kutaka kufikisha mambo chanya na kuondoa dhana potofu katika jamii kuhusiana na watu wanaoishi katika huu utamaduni wa Hip Hop. Lakini basically iko katika hii culture yangu ambayo naiishi na kuienzi.
That’s why katika hizi movement nilikuwa najaribu kutafuta vijana ambao wana mtazamo chanya na ambao tunaishi wote na ku focus kwenye jambo moja ili tufikishe mawazo yetu kwa hadhira. Na tulifanikiwa kufanya mradi mmoja. Focus ya hii Knowledge and Movement Hip Hop Cypher ni kila mwaka at least huwa inafanyika moja. Tunatafuta mada ama topic ambayo itakua na mlango chanya kwa jamii, tunaingia studio tuna record alafu then tunai release. Kwa hiyo kwa hii Knowledge & Movement ni mradi ambao utakuwa unatoka kila baada ya mwaka, hiyo ndio focus kubwa ya hii Knowledge & Movement Hip Hop Cypher.
Ni nini kinachomtofautisha Swanga The Conscious na emcee yoyote yule nje na ndani ya Tanzania?
Kinachonitofautisha zaidi na ma emcee wenzangu wa ndani na wa nje (ya Tanzania) naamini ni upekee, uniqueness ambayo Mungu amenijalia kua nayo, pia delivery, uandishi, flows, nafkiri hivi vitu vipo tofauti na vya baadhi ya wenzangu kwa sababu kikubwa mimi huwa naandika sana kwa hisia, mimi napenda delivery, lyrical delivery iwe kwa namna yoyote ile katika kufikisha ujumbe, katika bata hata katika flow za kibabe. Lakini kikubwa naweza sema ni upekee kwa sababu kila mtu alivyoumbwa na Mungu aliumbwa na nafasi yake, na utofauti wake, we are not equal. Yaani hicho ndio kitu ambacho ninaweza kusema.
Wana Hip Hop wa handakini wamekuwa wazito kidogo kuweka miradi yao kwenye digital platform za muziki. Wewe naona umefanikiwa kuweka miradi yako huko na ningeomba utueleze kidogo kuhusu changamoto, manufaa na hasara ya hizi platforms. Ni kipi kilichokusukuma kuweka muziki wako kule?
Ok, kuhusu hizi digital platforms nafkiri muziki umezidi kukua na muziki umekuwa biashara na kadri tunavyoendelea kukua na masoko ya sanaa yetu yanaendelea kutanuka zaidi. Kwa sisi wasanii ambao tuna audience ndogo ni vizuri mimi ningependa kuwashauri wasanii wenzangu wa invest kule na ku invest kule sio kwa matarajio ya kipindi kifupi kwamba uingize leo mwezi wa pili upate, hapana. Kwa sisi wenye audience ndogo unatakiwa kule una invest for years yaani unakua na matarajio ya miaka kadhaa mbele unaweza unakapata kile unachostahili.
Kwa hiyo mimi sioni tatizo kwa kule kwa sababu nitaendelea kujitangaza zaidi na kuwa free zaidi na pia kulingana na soko la muziki sasa hivi lilipo pia. Tunatakiwa kuwafikia hawa wafuasi wetu kwa wepesi zaidi kama wanavyofanya baadhi ya watu wa miziki mingine.
Kwa hiyo mi nafkiri kule kuna nafasi kubwa sana kutu push sana sisi artists na kutufanya sisi muziki wetu uende kwa wengi na mbali, that’s why kadri jinsi kunapokuwa kuna digital platform nyingi matokeo ambayo yanakuwa yanapatikana na yanakua yanatoa ajira mbadala kwa wasanii. Kwa hiyo mimi nachukulia kule ni kama upande wa pili wa ajira ya sanaa yangu.
Hasara ni changamoto za kawaida kwenye miradi na biashara, kwa hivyo siwezi kuongea. Hata hizi hard copy ( CDs) unakuta mtu unamuuzia CD na yeye anaenda anampa mtu anadurufu CD, we huoni hiyo pia ni hasara katika kazi? Kwa hiyo sasa kwenye swala la hasara kwenye zile digital platforms ninachukulia ni changamoto tu za kawaida kwa sababu huwezi ukawa unafanya mradi au biashara yoyote ukawa unaikwepa hasara. Kuna faida kuna hasara. Kwa hiyo mimi naonaga hasara ikitangulia sasa hivi unakua bora zaidi, japokua pia hasara ina cost yake kubwa sana. Hasara inaweza kukusababishia ukakata tamaa ukafanya kitu ambacho hukutarajia kufanya. Lakini pia hasara zinatufanya kuwa na funzo na kuwa bora zaidi ya wakati huo ya biashara uliyokuwa unaifanya.
Kwa hiyo digital platform kwa upande mwingine mimi naichukulia ni nafasi ya kujitangaza na ku link up na wasanii wenzangu nje pia ya dunia yangu ya karibu ambayo tunaishi ambao tunafanana mitazamo chanya.
Kando na mziki Swanga The Conscious unajishughulisha na kipi kingine ambacho kinakuwezesha wewe kuweka msosi mezani?
Hasahasa ni mjasiriamali ninae fanya shughuli zangu ndogo ndogo ambazo zinanipatia rizki zangu ndogo ndogo, before that nilikuwa assistant driver na tulikuwa tunavusha ma truck kutoka ndani kupeleka nje ya nchi kupeleka goods kule. Kwa hivyo tumefanya kazi hiyo for years na nilichokipata kule nikaona ngoja ni invest kwenye hizi biashara zangu ndogo ndogo.
Kuna dhana flani nilisoma sehemu kuwa wana handaki hawafai kuhojiwa redioni. Wewe naona umehojiwa na redio kibao. Hili unalizungumziaje?
Yaah, sasa hapo kuhusu kuhojiwa sijui walikuwa wana dhana gani na walikuwa wame focus kwenye nini lakini sisi kama wasanii ambao tunaishi kwenye rap game tunahitaji sana mapinduzi ya huu muziki wetu kwa hiyo radio inahusika kwa nafasi kubwa kuendelea kututangaza na kutufanya tuifikie jamii yetu kwa wepesi zaidi.
Vyanzo vya habari ni muhimu sana, hata hapa podcast yako hii ipo kwenye chanzo cha habari, sasa kama sitakiwi kuhojiwa na huku nahojiwa kwenye hii podcast kutafuta nini. Ndio utakuja kuona utofauti sana, sometimes uelewa pia ni changamoto, hivi hivi.
Kwa hiyo sisi baadhi ya wasanii tunahitaji pia kupata elimu juu ya hivi vitu kwa maana tusiishi tu kwa kukariri kuwa hichi kipo hivi basi tukifate hivi. Tuwe tunahoji na tunauliza kwa nini ili tuweze jua kwa nini kipo hivi na kwa sababu gani kipo hivi. Kwa hivyo nafkiria uelewa tunaukosa baadhi ya maarifa juu ya hivi vitu, lakini vyombo vya habari huwa ni vitu muhimu sana kwa kuendelea kukuza sanaa yetu na kutufanya tufikie karibu jamii yetu au wale watu ambao wako mbali na maeneo yaliyotuzunguka na ndio maana unaona kuna Facebook kuna Instagram, WhatsApp, Telegram. Hivyo vitu ni vyanzo vya habari ambavyo wasanii tunavitumia.
Wakati unapochagua mtayarishaji wa kufanya naye kazi ni vigezo gani unavyovizingatia?
Mimi kikubwa ambacho ninakizingatia kwa mtu ambaye ninayetaka kufanya nae kazi ni kwamba yeye mwenyewe awe na feelings na kile anachokifanya. Yaani producer akiwa na feelings ana delivery ya ala zake mimi huwa nafanya naye kazi, mimi huwa sichagui sana yaani sijui huyu braza sijui huyu nani, huyu ana jina hili. Mimi sichagui jina. Mimi naangalia napata nini kwa huyu ninayefanya naye.
Coz that’s why mimi nimeanza kufanya kazi na Patrino miaka ya nyuma kuanza 2013 alikuwa ananitumia ma midundo hadi leo hii niko naye kwa sababu nimeona huyu jamaa ana kitu. Kwa hivyo mtu akiona nafanya kazi na Patrino mtu anaweza dhania nimeanza kufanya naye kazi juzi kumbe hapana ni mda mrefu na si kwa sababu anatoka Sumbawanga, sio kwa sababu Patrino hapana.
Pia niko na mwanangu Tinie Cousin, unaona huyu jamaa anafanya na anafanya kwa nafasi yake, anatake naye sanaa yake ifike, kuna mahala ifike. Kwa hiyo ukikutana na watu ambao wana mitazamo chanya alafu wote mnafanana ideas basi mimi nafikiri kuna kitu kizuri sana.
Mimi huaga sichagui producer na huwa sina ile tabia ya kusema sijua kwa sababu ni flani ndio nifanye naye kazi, sinaga utaratibu huo. Mimi producer yoyote hata ambae anae tokea sasa hivi ambae naweza kupiga kazi na nikaweka shairi langu juu ya ala zake na nikafika kule ninapopataka basi mtu wa namna hiyo naweza kufanya naye kazi.
Pia tunatoa nafasi kwa ma producer namna hiyo pia kama wapo wanaweza waka link na mimi tukaangalia namna gani tunaweza tukafanya kazi.
Ni kipi cha mwisho ungependa kutuambia ambacho sijakuuliza kukuuliza?
Niwapongeze nyinyi kama Micshariki kwa kutumia mda na nguvu zenu ku invest kwenye hii rap game. Ila msisahau kuwaambia wanajamii, kuwatangazia wana jamii kuwa project ziko on. Nimetoa Project ya Safari na mradi wa pili huu wa Acha Moto Uwake lakini napenda kuwaambia wanajamii na mashabiki kuwa album ipo njiani au ipo katika maandalizi ya hatua za kati. Maandalizi yapo yanaendelea, tracks kadhaa zishakua recorded kwa hiyo hicho ndio kikubwa ambacho nataka niwaambie nyie jamaa ambacho hamkuwahi kuniuliza.
Shukran sana kaka Swanga kwa mda wako na asante sana kwa kukubali wito wetu wa kuja kwenye jukwaa letu la Hip Hop Micshariki Africa. Asante sana.
Shukran pia nyie wajamaa pia kwa kunipa mda wenu na kuamini kwamba Swanga pia na yeye anaweza aka share kitu katika page zenu pia. Nawapenda sana!
Mfuate Swanga The Conscious:
Instragram: swanga_theconscious_mind
YouTube: Swanga ConsciousMindtz