Professor Jay

Ukiniambia nikutajie album nzuri za muda wote za muziki wa kizazi kipya (rap) sintosita kutaja ‘Machozi Jasho Na Damu’ kuwa ni miongoni mwa album bora kabisa kwa karne ya 21 kwa muziki wa nyumbani Tanzania.

‘Machozi Jasho Na Damu’ ndio ilikuwa album ya kwanza kabisa toka kwa mtu mzima Prof Jay kama msanii wa kujitegemea hii ni baada ya ile album yao ya kundi la HBC ndipo akaja na solo project akaipa jina ‘Machozi Jasho Na Damu’.

Kwenye hii album kulijaa nyimbo nyingi kali na za 🔥 kusikiliza, yani wimbo ukimalizika ukafuata mwingine unasikia huu unaosikiliza baada ya ule uliokwisha ni mkali kuliko uliopota.

Huyu ndio Jay asikwambia mtu, mkali wa kukaa kwenye topic katika tungo zake mwanzo mwisho, mkali wa kukupa simulizi mwanzo mwisho kupitia rap na ukaelewa anachosimulia huku ukibaki na picha nyingi kichwani mwako juu ya simulizi aliyokupa.

‘Machozi Jasho Na Damu’ ndio album ambayo alikuja nayo ikiwa na jina lake jipya kabisa kutoka Nigger Jay mpaka kuwa Professor Jay. Yani mitaa ilishaona huyu sio nigger ni professor wa huu mziki.

Album ilibeba mawe mengi makali, mawe ambayo wale waliopata bahati ya kushiriki wakikupa simulizi juu ya kushiriki kwao kwenye hii album, unasema YES hii kweli ni miongoni mwa album bora za muda wote.

Ukisikiliza wimbo kama ‘Jina Langu’ unasema huu ni wenyewe kabisa, ukaja tena kusikiliza ‘Bongo Dar Es Salaam’ unabaki kuguna tu ubaki na ipi? Ukiwa unawaza unajikuta ‘Ndio Mzee’ hii hapo unajikuta mdomo unafunguka kwa kushangaa na maswali kibao ukiwaza huyu jamaa anawaza nini kabla ya kuandika.

Unasogea kidogo unakutana na ‘Niamini’ humu unawasikia ndugu zake wa HBC unakosa la kusema maana ujumbe umepata wa kutosha kabisa kuomba msamaha kwa baby mama, ukija PIGA MAKOFI nayo unaona ni moto.

Ukizidi kutega sikio unakutana na ‘Nawakilisha’ humu kila aliyepita alikamua mbaya unaweza kusema jamaa walikuwa wanafanya wimbo kama kutuaga vile sasa watupe zawadi ya beti kali kila aliyeweka sauti.

‘Salamu Bibi Na Babu’, ‘Na Bado’, ‘Yataka Moyo’, ‘Machozi Jasho Na Damu’ mpaka unatua kwenye ‘Tathmini’  unasema YES hela yangu nimelipa kihalali kabisa sijaibiwa na simdai mwenye album mpaka walioshiriki.

Kwangu mimi wimbo bora wa mda wote kwenye hii album ni ‘Tathmini’ akiwa na mtu mzima Jay Mo huu wimbo kwangu ni bora sababu vile vilivyoimbwa mpaka leo hii tunaviona kwa wasanii wetu.

Ubeti wa kwanza alianza Prof Jay mwenyewe,

Naahidi kuwa makini mpaka siku nafukiwa chini/
Na Mungu aliye hai bado yu pamoja na mimi/
Emcee shika vizuri karibu tawi linakatika/
Na kwa wote mliopo juu na chini sauti itafika/

Ukisikiliza mistari michache tu hapo unapata picha kuwa Jay yupo makini kwenye kila kitu chake huku imani yake kwa Mungu akiamini yupo nae kwa kile anachokiamini. Pia akatoa angalizo kwa emcee ambaye yupo mainstream na underground pia kuwa watamsikiliza na sauti yake itawafikia kwani hali ya game sio salama ki vile mda wowote upepo utabadilika.

Na kweli upepo umebadilika now Amapiano na Singeli zimeshika sehemu kubwa ya masikio ya wengi na kila msanii mpya anawaza kutoka kwa kuimba Singeli au Amapiano ikiwa zama zile walitoka kwa kurap.

Kazi na dawa ndani ya uswazi kazi ni kazi/
Na nipo radhi kutoa tathmini ngazi kwa ngazi/
Rap si lelemama kama wengi mnavyodhani/
Fasihi iliyo hai kuitoa jamii gizani/

Watu wengi waliamini rap ni kitu chepesi sana yani ukiweza kutamka(kuongea) basi unajiona unaweza kurap lakini Jay akawapa onyo kabisa kuwa rap sio lelemama, rap inataka watu smart ambao wanaweza kujaza knowledge kwa jamii kuwatoa kwenye giza la kile wasichokijua na sio kingine.

Miaka ya 80 Hip-Hop bongo ilichipua/
Na nadhani wakongwe wa rap hii mnaitambua/
Hali ilikuwa mbaya miaka ya 89/
Watu hawakutaka kuelewa rap kabisa/
Miaka ya 90 Hip-Hop Bongo imekubalika/
Wenye nia nzuri na rap tunawajibika/

Prof kaona ili jamii tumuelewe atupe kastory kidogo kuhusu Hip-hHop ilivyoanza na kuingia Tanzania, kuonesha msisitizo akawagusia wakongwe kuwa wanatambua hilo, kuna muda nikisikiliza mistari hii nasema Jay andika kitabu cha maisha yako.

Kufika miaka ya 90 naona sasa watu wakakubali kuwa Hip-Hop ni zaidi ya mziki japo 89 kuna tabu kidogo zilitokea. Anasisitiza wenye nia nzuri na rap wao wanawajibika yani wanawajibika kufunza jamii kupitia rap na sio kingine.

Rap ni wito yataka utashi na ufahamu/
Wasanii wenyewe wabongo wanafanya tudharauliwe/
Watu vibongo kidogo hawataki washauriwe/
Wanaongea blah blah vijina viwe/

Anakwambia kufanya rap ni wito ambao unatoka ndani ya moyo na sio ile kukaa maskani umekula mpepe au tungi ukaimba vijimbo vya watu basi ukajiona unaweza kufanya rap (mchanaji), kisha anakwambia wasanii wenyewe ndio mnatengeneza mazingira ya kudharauliwa.

Vitu vinavyofanya mtu akudharau ni viwili, muonekano wako na kile unachokiwakilisha, je vinaendana au vinapishana, unakemea kuhusu bangi na pombe cha ajabu wewe unayekemea muda wote upo ndumu na pombe hapo jamii itakupa respect vipi?

Watu wanaona kuwa wachanaji ndio kujua kila kitu kitu ambacho sio kweli ndio maana Jay akawaambia watu vibongo kidogo yani watu akili ndogo bado wanabisha au kukataa kuelekezwa na kupewa ushauri, watu wa hivi mwisho wa siku sonona inawatesa wanabaki kutoa lawama.

Na wanaovunja hata miko ya rap waheshimiwe/
Wengine watatumia kivuli cha rap kufanyia uhuni/
Hii ni sawa na kupanda ngazi kuelekea mbinguni/
Tathmini ya kweli yatia majaribuni/
Na mnaovunja miiko ya Rap jihukumuni/

Ubeti wa kwanza Jay kamaliza kiungwana kabisa na kiutu uzima, kuna watu wanatoka nje ya misingi ya Hip-Hop nao wanataka tuwape heshima katika Hip-Hop hii sio kweli, wengine wanaona rap (Hip-Hop) ni sehemu ya kufanya ujinga wao na harakati zao za kihuni ili lawama ipewe Hip-Hop.

Mwisho anasema wote ambao mnajua mnachokifanya sio sahihi jipeni hukumu wenyewe kabla ya kupewa hukumu na wadau, mashabiki n.k.

Ubeti wa Prof J,

Naahidi kuwa makini mpaka siku nafukiwa chini/
Na Mungu aliye hai bado yu pamoja na mimi/
Emcee shika vizuri karibu tawi linakatika/
Na kwa wote mliopo juu na chini sauti itafika/
Kazi na dawa ndani ya uswazi kazi ni kazi/
Na nipo radhi kutoa tathmini ngazi kwa ngazi/
Rap si lelemama kama wengi mnavyodhani/
Fasihi iliyo hai kuitoa jamii gizani/
Miaka ya 80 Hip Hop Bongo ilichipua/
Na nadhani wale wakongwe wa rap hii mnaitambua/
Hali ilikuwa mbaya miaka ya 89/
Watu hawakutaka kuelewa rap kabisa/
Miaka ya 90 Hip Hop Bongo imekubalika/
Wenye nia nzuri na rap tunawajibika/
Rap ni wito yataka utashi na ufahamu/
Elimu ya mtaani kujituma pia nidhamu/
Wasanii wenyewe wa Bongo tunaofanya tudharauliwe/
Watu vibongo vidogo hawataki washauriwe/
Wanaongea blah blah, vijina viwe/
Na wanaovunja hata miko ya rap waheshimiwe! /
Wengine watatumia kivuli cha rap kufanyia uhuni/
Hii ni sawa na kupanda ngazi kuelekea mbinguni/
Tathmini ya kweli yatia majaribuni/
Na mnaovunja miko ya rap jihukumuni/

Kiitikio pia kasimama Prof Jay mwenyewe.

Hii ni tathmini kwa wote juu na chini/
Yoh emcee zunguka nyuzi 360/
Umeona nini? Mwana mpotevu rudi kundini/
Fani ni uwanja mpana na jua lipo utosini/

Kiitikio tu kinakupa picha kuwa ni sahihi kabisa Jay kuwa Professor wa huu mziki kwa tathmini aliyotupa kupitia ubeti wa kwanza na kiitikio chake.

Ubeti wa pili kasimama mkali Jay Moe nae mkali wa kukaa kwenye topic pia mkali wa kutupa simulizi kwa njia ya rap akaeleweka vizuri tu bila kupata walakini.

Yoh! Mawazo ya Jay Moe usiku mchana yalikuwa wima/
Ingawa sikujua usiku ukiisha asubuhi itakuwa neema/
Kwani baba na mama miaka ile kipindi cha nyuma/
Waliamini rap ni kuimba yale yasiyokuwa mema/

Mwamba kabisa naye kama anatuambia ile miaka ya ‘89 ambayo Hip-Hop kwa Tanzania ilipata misukosuko hii tuliambiwa na Jay kwenye beti yake ya kwanza ‘89 watu hawakuelewa kabisa kuhusu Hip-Hop.

Jay Moe anasema baba na mama waliona rap sio muziki mzuri waliamini kitakachoimbwa sio kile ambacho jamii inatakiwa kuimbiwa hivyo wakae wasome watulie.

Haina noma wakwezi tulipomaliza kusoma/
Mistari iliandikwa ujumbe ukashuka ukakubalika/
Ndio ilikuwa bado wenye hisa kutolea macho/
Walithamini Bolingo, ambacho kimewachosha Bongo/
Wahisani waongo walidhani tungedorora/

Ikabidi kwanza wakomae na shule wasimuache elimu walipomaliza sasa ndio wakaja kwenye game Hip-Hop ambayo mwanzo wazazi waliona sio kitu cha kawaida kwa kijana kukifanya. Moe anakwambia watu wakaandika kuwa prove sivyo wale ambao waliona ni uhuni.

Wadau wa muziki waliwaza kuwa huu mziki wa kitoto hauwezi kukesha mziki wa kikubwa ni Bolingo, kumbe wadau hawakujua Bolingo vijana wengi imewachosha sasa wanataka rap na sio kingine.

Wameingia mitini ‘Chemsha Bongo’ ilipoingia redioni/
Kama wametawala ikafika walio Bungeni/
Watu wakazinduka, yaani wakashtuka wataongea nini/
Watu na Bongo Fleva kingine wanasema uhuni/
Taarabu imeingia nuksi, Bolingo inafuka moshi/

Moe anamaanisha wadau waliposikia ‘Chemsha Bongo’ wakajua vijana kuna kitu wanacho tuwazingatie tuwape sikio la ziada. ‘Chemsha Bongo’ ni miongoni mwa nyimbo ambazo zimeleta mageuzi makubwa sana kwenye huu muziki Tanzania respect to HBC.

Wadau ambao waliona ni uhuni wakaanza kusepa mdogo mdogo wakajua cha kuongea hakipo tena na muziki ukabatizwa jina kuwa Bongo Fleva zile zilizotamba zote tupa kule sio Taarabu wala Bolingo zama na Nasma na Khadija zikazimwa.

Sasa Wahisani tapeli hutoboa wenye mistari/
Kila mtu anakuja na uongo ili mradi tukubali/
Na ma producer wa sasa wanashtuka kwamba tunauza/
Wanashtuka kwamba walicheza Hip-Hop ina fedha/

Mapinduzi ya kimaandishi kutoka kwenye wimbo wa ‘Chemsha Bongo’ ndio kuliwastua wadau wahisani na kuona Hip-Hop kuna pesa pale ngoja tuzamie meli yao japo tuliwabeza ni uhuni lakini ndio generation yao inataka na wanaelewa ngoja twende nao tu.

Jay Moe mbakiaji sasa nahitaji umaskini ubounce/
Shori mzuri, gari, pamba, fedha kwenye bank account/
Labda tatizo liwe kwa Emcee asiye na elimu/
Eti afanye nini? Mi nadhani bora akauze ndumu/

Moe muhuni sana kuna swali mwishoni kafanya kama anauliza kisha anajibu "bora akauze ndumu"

Elimu ni muhimu kwa kila kitu ndio maana Moe akaliona hilo huu utamaduni unataka uwe na elimu juu ya huu utamaduni na kama ukiwa nao ubishani wa kijinga jinga nani Hip-Hop na nani sio Hip-Hop kamwe hauwezi kuwa nao. Ubeti wa Moe ukafunga hapo kiutu uzima.

Ubeti wa pili Jay Moe.

Yoh! Mawazo ya Jay Moe usiku mchana yalikuwa wima/
Ingawa sikujua usiku ukiisha asubuhi itakuwa neema/
Kwani baba mama miaka ile kipindi cha nyuma/
Waliamini rap ni kuimba yale yasiyokuwa mema/
Haina noma wakwezi tulipomaliza kusoma/
Mistari iliandikwa ujumbe ukashuka ukakubalika/
Ndio ilikuwa bado wenye hisa kutolea macho/
Walithamini Bolingo, ambacho kimewachosha Bongo/
Wahisani waongo, walidhani tungedorora/
Mara ngoma ika-change na nyota ya rap ikang’ara/
Wasambazaji habari ya kwamba Hip Hop uhuni/
Wameingia mitini ‘Chemsha Bongo’ ilipoingia redioni/
Kama wametawala ikafikia walio bungeni/
Watu wakazinduka, yaani wakashtuka wataongea nini/
Watu na Bongo Flava kingine wanasema uzushi/
Taarabu imeingia nuksi, Bolingo inafuka moshi/
Sasa wahisani tapeli hutuboa wenye mistari/
Kila mtu anakuja na uongo ili mradi tukubali/
Na ma-producer wa sasa wanashtuka kwamba tunauza/
Wanashtuka kwamba walicheza, Hip Hop ina fedha/
Jay Moe mbakiaji sasa nahitaji umaskini u-bounce/
Shori mzuri, gari, pamba, fedha kwenye bank account/
Labda tatizo iwe kwa emcee asiye na elimu/
Eti afanye nini? Mi nadhani bora akauze ndumu/

Tufunge na kumaliza na ubeti wa Prof Jay mwenyewe ambao nao umeshiba sana.

Yule yule ni Jay na Jay ni yule yule/
Wanga wekeni kikao kisha mnifanye msukule/
Domo langu ni hela linatoa ushauri wa bure/
Ila ma-emcee wengi wa Bongo hampendi kwenda shule/
Kumbuka hii ni rap ndani ya karne ya 21/
Nilazima uchangamshe Bongo kwenye mchanganuo wa hoja/

Jay anaamini mpaka alipofika pale yeye kashakuwa hela na so anachozungumza kuhusu jambo la ushauri na utaalamu inabidi apate pesa lakini kwa kuwa anajua changamoto zilipo yeye anatoa ushauri bure ukitaka pokea, hutaki usipokee na hii kakukumbusha ni karne ya 21 karne ya watu ambao ni wadadisi na wanaopenda kuhoji kila jambo na wanataka majibu sahihi.

Nafurahi kuona emcees ni wengi kama utitiri/
Kinachoniudhi wengi wanarap bila kutumia akili/
Rap ya Bongo imegawanyika katika makundi mawili/
Na kuna ma emcee kamili na emcee waliobatili/

Kiukweli kukosa kwa elimu juu ya Hip-hop ndio kimefanya kuwa na makundi na ubishani wa nani ni Hip-Hop na nani sio Hip-Hop na hapo ndipo unakuta kwa wale ambao wanajiona ni Hip-Hop kumbe ndio mawaki wakubwa na wale ambao wanaonekana sio Hip-Hop ndio wanaweza kuishi katika utamaduni wa Hip-Hop.

Ebwana nasema hivi kama kuna uwezekano huyu Prof Jay anatakiwa kutupa zawadi ya kitabu kuhusu maisha yake, muziki wake na upande wa siasa Jay ni mgodi unaotembea unapaswa tulinde na tutunze kazi zake.

Beti ya tatu ni kama hii

Yule yule ni Jay na Jay ni yule yule/
Wanga wekeni kikao kisha mnifanye msukule/
Domo langu ni hela linatoa ushauri wa bure/
Ila ma-emcee wengi wa Bongo hampendi kwenda shule/
Kumbuka hii ni rap ndani ya karne ya 21/
Ni lazma uchemshe bongo kwenye mchanganuo wa hoja/
Nafurahi kuona emcees ni wengi kama utitiri/
Kinachoniudhi wengi wana-rap bila kutumia akili/
Rap ya Bongo imegawanyika makundi mawili/
Na kuna ma-emcee kamili na emcee waliobatili/
Emcee mwenye hekima anafikiri kabla ya ku-rap/
Na emcee mpumbavu ana-rap apate nyapu/
Natumia lugha kali tafsiri unavyoweza/
Napunguza tafsida maneno yanajieleza/
Watu viwango vidogo wanaleweshwa na sifa/
Ni lazma mjikongoje kwenye level za kimataifa/
Wengi hampendi kuchambua tamathali za semi/
Na matokeo ndo vile ngoma zenu mwali hanemi/
Watu wanavaba mic na ku-rap kama majuha tu/
Katikati ya bahari mnapanda boti za mabua/
Msilete utani, hii ni fani yenye ushindani/
Jiulize waliovuma wangapi wamebaki gizani/
Ninaowaudhi, hii naifanya makusudi/
Ili mpate ghadhabu na kuongeza juhudi/

Muandishi
Beberu La Mbegu(Logo Ya Dunia)