Ngoma nilizozipenda: Mi Mmasai, Maneno Mbofu Mbofu, Fahahi Yako, Sitaki Pombe….kwa ufupi ngoma zote!
Mwaka jana 2021 mwezi April tarehe 29 niliandika hivi kuhusu marehemu Mr. Ebbo,
“Marehemu Mr. Ebbo alikuwa msanii wa kipekee mwenye style yake enzi hizo. Album yake ya Fahari Yako kwangu ni classic. Ni album yenye madini ndani ya ucheshi. Nashkuru kaka Evans Waihuini kwa kunipa hii albam na nyingine za hip hop toka bongo bure enzi hizo japokua ulikuwa unaziuza kule Mombasa. Nilithamini hii sana kaka, hujui tu.
Kwa Ebbo, hii album nikikumbuka nasema ulituachia fahari ya kweli mashabiki zako.”
Dizasta Vina wakati akihojiwa kuhusu kazi yake classic The Verteller alisema moja ya kazi alizokuwa akiziskiza sana wakati akiandaa album yake ilikuwa ni mradi huu wa Fahari Yako. Hapa ndio utajua umuhimu wa kazi hii kwani mpaka leo inazidi kuacha alama mioyoni mwetu.
Msanii huyu ambaye jina lake rasmi ni Abel Loshilaa Motika alizaliwa tarehe 26 Mei 1974 kule Arusha na kufariki December 1, 2011 kule Arusha baada ya kuugua saratani ya damu (leukemia).
Album yake ya kwanza Fahari Yako aliitoa mwaka 2002 ilikuwa na ngoma hizi;
- Mi Mmasai
- Maneno Mbofu Mbofu
- Fahari Yako
- Vipi Hatuoni?
- Sitaki Tena Pombe
- Mi Mmasai (RMX)
- Muwe Na huruma (Feat. Bad Gear)
- Nani Huyo? (Feat. Mwanafalsafa)
Mradi huu ulituhimiza kujipenda na kupenda vya kwetu na pia kuanza kuhoji elimu ya shuleni iliyotufunza kua sisi na vyote tulivyonavyo hapa viligunduliwa na mzungu, Maneno Mbofu Mbofu.
Shukran sana kaka mkubwa marehemu Mr. Ebbo. Mchango wako maishani mwetu na kwenye tasnia ya muziki sio tu ya bongo bali hata Africa Mashariki kiujumla ulikuwa ni mkubwa leo tumekukumbuka kupitia kazi yako ambayo sio tu fahari yetu ila ni Fahari Yako pia.