Fivara

Hii itakua ni album yangu ya pili baada ya Fikra ni Vazi la Rap album yangu ya kwanza iliyotoka 2018 ikiwa na idadi ya nyimbo 13. Baada ya miaka kadhaa niliachia EP yangu iitwayo 259 EP yenye jumla ya nyimbo 6. Album yangu hii ya pili nilianza kuirekodi rasmi mwaka 2020 hivyo hadi mwaka huu itakapokua imetoka itakua ni jumla ya miaka mitatu katika maandalizi ya album hii.

Sababu za kuandaa hii album

Nikiwa ni msanii ambae mara nyingi naachia kazi kwa mifumo wa miradi yani albums, eps au mixtape hivyo mradi huu ni mwendelezo wa mkakati wangu kwenye huu upande wa kuachia miradi (catalog). Nadhani ni muda sahihi wa kutoa album ukizingatia kwamba katika miaka yote hii kuna mambo mbalimbali niliyojifunza, niliyoyaona na yamepelekea mimi kuandaa album hii. Nadhani mitaa na mashabiki zangu wanahitaji chakula hiki cha ubongo ambacho kitakua kwenye menu moja.

Ni album ambayo italeta mapinduzi kwenye tasnia ya muziki wetu hapa nyumbani kuanzia upande wa sanaa hadi biashara. Kupitia album hii najua nitaacha historia kubwa kwenye dunia kiujumla. Itaongeza thamani kwenye muziki wangu kwa sababu watu wataujua zaidi uwezo wangu na kunifahamu mimi ni mtu wa aina gani na nasimamia vitu gani.

Pia kazi hii itaonyesha ukuaji wangu katika nyanja tofauti za maisha yangu kuanzia mimi binafsi, sanaa yangu na kadhalika pamoja na kuonyesha inawezekana kuandaa mradi popote pale ulipo sio lazima kwenda jijini Dar es Salaam. Mradi huu utaongea na watu moja kwa moja kwenye rika zote haswa vijana wanaopambana kujikwamua

Watayarishaji wa hii album

Watayarishaji tofauti wamehusika akiwemo Wavoko, Odilla Beatz, Smokie, Sheem King, Black Ninja, Yas Lo, Aby Bangladesh, Slimsal, Daz Marley na wengine kibao.

Production na uchanganyaji

Album imerekodiwa kwenye studio ya B.I.G Records iliyopo jijini Mwanza ilhali watayarishaji Wavoko na Q The Don ndio wamehusika kwenye uchanganyaji (mixing) na umaliziaji (mastering).

Wasanii walioshirikishwa

Kwa asilimia kubwa album hii nimefanya mimi mwenyewe kuanzia uandishi, viitikio nk. Baadhi ya wasanii walioshirikishwa watakua ni surprise package na watu watawajua orodha ya nyimbo ikitoka.

Release date, artwork na tracklist

Album inatarajiwa kutoka kabla ya mwezi Juni mwaka huu 2023. Artwork na orodha ya nyimbo vitatangazwa kupitia vyanzo vyangu vya mawasiliano. Idadi ya nyimbo itajulikana pia kwenye kava la nyuma au orodha itapotoka (31.05.2023)

Mfumo wa upatikanaji

Album itapatikana kwa mifumo miwili yani soft copy na hard copy. Soft copy itakua kwa mfumo wa WhatsApp document, Telegram au email ambapo mnunuzi atachagua yeye. Hard copy itakua kwa mfumo wa USB flash ambazo zitauzwa kwa bei tajwa baada au kabla ya album kutoka.

Bei ya album

Album itapatikana kwa kiwango chochote unachotaka wewe mnunuzi ila isiwe chini ya sh 25,000.

Bidhaa ambatanishi

Album itatoka na bidhaa nyingine za kuipromoti ambazo zitatangazwa upatikanaji wake.

Show, promotions na ziara

Natarajia kufanya show mbalimbali kuanzia za uzinduzi, za kuskiliza, kuchambua na kuipromoti album kwenye mikoa tofauti Tanzania na ikiwezekana nje ya nchi

Matarajio

- Album ipokelewe vyema na mashabiki zangu, wadau na wapenda muziki wote duniani

- Watu wameng’enye kilichopo kwenye album na kiwasaidia kupiga hatua moja kwenda nyingine

- Iwe moja ya album bora iliyowahi kutoka kwenye muziki wa Rap na mahadhi mengine kiujumla hapa Tanzania

- Iishi vizazi na vizazi

- Iwe album bora ya mwaka kwa mahadhi yote kuanzia rap hadi muziki wa kuimba

Cha kusisitiza

Watu wakae karibu na vyanzo vyangu vya mawasiliano haswa mitandao ya kijamii ili kupata taarifa zaidi kuhusu ujio wa album hii;

Instagram:@fivara
Twitter: @fivara_
Facebook: @fivara
YouTube: @fivara
TikTok: @fivara

Asante!!