Uchambuzi wa Albam: Refraction
Emcees: The MC (Mukimala x Catalyst)
Tarehe iliyotoka: 12.06.2021
Nyimbo: 29 (Nyimbo 22 na Skits 7)
Watayarishaji: De La Funky, Abby MP, Ngwesa, Black Ninja
Studio: Digg Down Records

Ngoma Nilizozipenda: Idle, Idol, Kanabo Character, Kerosene/Kere Scene, Mtaa, Perscreativity, What You Are, Rebel/Label, Take Knowledge/Technology, Idea/I Dear

Catalyst x Mukimala

Refraction ni kupinda kwa mwanga (pia hutokea kwa sauti, maji na mawimbi mengine) inapopita kutoka kwa dutu moja ya uwazi hadi nyingine.

Kujipinda huku kwa kinzani hutuwezesha kuwa na lenzi, miwani ya kukuza, prismu na upinde wa mvua. Hata macho yetu yanategemea kupinda huku kwa nuru. Bila kinzani, tusingeweza kuelekeza mwanga kwenye retina yetu.

Mwaka jana kundi la jamaa wawili toka Dar wanaojiita The MC; Mukimala na mwenzake Catalyst walitumia hizi kanuni za sayansi za upinde na kutupatia album yao Refraction. Mukimala na Catalyst tukianza na kundi hili nilichokiona ni kuwa wao ni upinde wa mashairi yanayotoka kwenye speaker zetu. Kila mmoja kwa upindi wa kinasa anatuonesha rangi tofauti na mtazamo tofauti wa kitu kimoja kwa kupitia kinasa.

Mradi huu ambao umeundwa chini ya studio ya Digg Down Records umewashirikisha ma producer waliobobea kwa midundo ya boombap na kusheheni lofi Hip Hop kama vile Ngwesa, Black Ninja, Abby MP na De La Funky ambae aliandaa asilimia kubwa ya midundo kwenye mradi huu.

Single ya kwanza toka kwa mradi huu Mistari –Barz uliyoundwa na Ngwesa wakimshirikisha Dizasta Vina ambaye ni mmoja wa ma emcee waalikwa kwenye mradi huu. Wengine walioalikwa ni kama Jessy, Lyne, Hechi, Kamusi, Liyen, BinSimba pamoja na Nim Art.

Mtaa ndio single ya pili iliyoachiwa toka kwa mradi huu. Wimbo unaanza na gita zuri wakati Muki na Catalyst wakituelezea soga za mitaa wanayotoka na kuiwakilisha hadi kifo chao.

Skits ama maigizo yapo mengi kupitiliza kwa maoni yangu na yanakaa ki mamtoni sana na nadhani kwa waliozoea Kiswahili hizi zitakua zinapigwa forward fasta sana baada ya kuziskiza kwa mara ya kwanza.

Ila kando na hayo umahiri wa ma emcee unauona kwenye ngoma kama Ara Kati/Harakati, Free Wheel/Free Will, Glow/Grow, High Breed/Hybrid, Idea/ I Dear, Imagination/ Image Nation, Rebel/Label, Take Knowledge/Technology, Idle zinazoonesha upinde unavyo fanya neno moja kutoka na maana mbili. Kwenye Idle Mukimala anachana juu ya mdundo flani mzuka sana wa De La Funky akisema,

“First let’s get one thing straight I never stay idle/
Me and Mary Jane got a procession that is bridal/
If you don’t get it that means I’m high bro/
365 all 7/24’s/
Yes I’m one with the crows/
Playing Robin Hood/
As I heist for food up to no good for the greater good always misunderstood/
By the clan see I’m a simple man/
I detest followers but spread love to fans/
I keep it real how I feel never in the midst of those who squeal I chucked the red and blue pill/
And settled for fruits I peel/
So I chill and let nature takes its course/
Knowing I and I got the direct link to source/
It pity’s me of course/
How they force how to I’d all leaving me idle with inner wars/
Tryna balance the scores/
Like I’m surfing on a tidal/
Now you tell me if I am fit to be your idol..../”

Nilichokipenda kwenye mradi huu ki ujumla ni chemistry ya ma emcee hawa, mashairi yao, uwasilishaji pamoja na uchaguzi mzuri wa midundo waliotumia kwenye albam hii. Refraction ndio habari ya mjini.

Wacheki ma emcee hawa kupitia ili upate nakala yako ya mradi huu Refraction;

Facebook: The MC Crew
Instagram: themc_255
Instagram: mukimala1
Instagram: kelvin_catalyst