TMT Festival ya mwaka huu ilifanyika Dodoma ambayo ni kitovu cha nchi hii. Baada ya maandalizi na nyimbo kibao kuachiwa na wanaharakati wanaona unga mkono movement hii tamasha lilifanika kufanyika tarehe 27.11.2021.
Nilipata fursa ya kufanya mahojiano na DQ Nyuzi Tisini ambae ni mmoja wa waratibu wa tamasha hili ambae pia ni mwenyeji wa Dodoma akiwakilisha kikundi cha wana Hip Hop toka kule kiitwacho Chimbuka Na Hip Hop.
Karibu ili tuweze kuskia toka kwake ile tuweze kuona jinsi tukio lilivyo kua pamoja na juhudi gani walizo ziweka ili kufanikisha tamasha hili ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Karibuni.
Karibu sana Micshariki Africa kaka. Tueleze kidogo kuhusu maandalizi ya TMT yalikuwaje? Nini kilifanyika behind the scenes kuhakikisha zoezi hili linafanikishwa? Maandalizi yakianza lini, nani wahusika?
Maandalizi yalianza mara baada ya kuthibitishwa kwamba TMTFESTIVAL2021 itafanyika Dodoma papo hapo maandalizi yalianza kwa kutafuta mdundo ili watu wafanye ngoma kama ilivyokuwa kwenye misimu miwili iliyopita mwaka 2019 Dar es Salaam na 2020 mkoani Mbeya ambapo tulifanikiwa kupata mdundo uliopigwa na mtayarishaji JAX INK kutokea Hapa hapa Dodoma.
Maandalizi ya kuhakikisha tunafanikisha kufanyika kwa TMT mwaka huu Dodoma kwanza kabisa yalianza na CHIMBUKA NA HIPHOP kwasababu ndio tulipewa jukumu la kuhakikisha kwamba mambo yote yanakaa sawa kuanzia ukumbi, sound, jukwaa vina kuwa sawa kwa wakati na kwa uhakika.
Lakini licha ya CHIMBUKA kupewa hilo jukumu bado kulikuwa na kamati ya kuhakikisha kwamba pesa zinapatikana kwa ajili ya kuwezesha tukio zima kufanyika na kamati hiyo hiyo ndiyo iliyotoa maamuzi ya TMT kufanyika Dodoma mwaka huu ambayo inaundwa na wawakilishi kutoka kwenye majukwaa na makundi ya HIPHOP nchini ambao ni Lugombo MaKaMTa (MaKaNTa), Gego Master (AKILI 100 ASILI 100), Moses Mfalanyombo (Kiswahili Na Sanaa), Kella B (Wasadikaya), Ben Mbuya, Kay Mapach (MAUJANJA SAPLAYAZ), Nyeke Da Nyiki (Watunza Misingi), Kunene, Jadah MaKaNTa, Alex SigaNyox...
Maudhui ya TMT 2021 yalikuwa ni yapi?
Maudhui ya TMT 2021 yalikuwa ni kuimarisha umoja na upendo baina ya wana HIP HOP nchi kote na hata duniani maana licha ya kuhamasisha uvaaji ya bidhaa zenye chata zetu wenyewe ila tunapokutana angalau kwa mwaka mara moja ule umoja na upendo unakomaa zaidi maana baadhi ya watu tumekutana kwenye mitandao ila tunapokutana inakuwa mzuka zaidi maana hili ndilo party la wana.
Nyimbo za TMT 2021 ziliandaliwa kwa kupitia mfumo upi? Ngoma zinapatikana wapi kwa wale wanaozihitaji( Je kuna uwezekano nikazipata kwa ajilli ya kuziweka pale Micshariki Africa kwa ajili ya mashabiki kuzipakua?)
Nyimbo za TMT2021 ziliandaliwa kwa mfumo wa muendelezo kwa maana ya kuanzia Part One(1) na kuendelea (Uwezekano wa kuzipata upo).










Siku ya tukio ilikuaje? Japokua zoezi lilianza saa sita je ni maandalizi gani ya awali yaliyofanyika siku hiyo ya tukio kabla ya shughuli nzima kuanza?
Siku ya tukio ilikuwa ngumu ila ilikuwa siku poa sana. Siku ngumu kwasababu ndio siku ya tukio kwa hiyo inabidi kila kitu kiwe sawa hivyo mikimbizano inakuwa mingi sana ila ni siku poa kwasababu ndio siku ya kufurahi na wana mastori ya mipango, mapicha yaani fresh sana. Maandalizi ya awali ni kuhakikisha kila kitu kilicho hitajika kimepatikana hata kama bado hakija fika eneo la tukio lakini pia mapokezi ya wageni wa siku hiyo.
Chimbuka Na Hip Hop mlihusika vipi na tukio zima?
CHIMBUKA NA HIP HOP ndio tulipewa jukumu la kuandaa kila kitu pamoja na kulisimamia ili kuhakikisha TMTFESTIVAL2021 linafanyika. Hivyo TMT2021 lilifanyika kupitia jukwaa la CHIMBUKA NA HIPHOP kwa kushirikiana na majukwaa na makundi mengine ya HIP HOP ndani na nje ya nchi.
Je watu kutoka mikoa mingine walianza kufika lini? Je mikoa iliyo wakilishwa ni kama ipi? Je inakisiwa idadi ya watu walio hudhuria tamasha hili ni wangapi?
Watu kutoka mikoani walianza kuingia siku ya ijumaa siku moja kabla ya tukio ndio tulianza kupokea watu kutoka mikoani. Mikoa ilyopata wawakilishi ni Mbeya, Dar es Salaam, Songea, Arusha na Morogoro. Watu si chini ya 150 walihudhuria kwa makadirio.
Je kwa upande wa maankuli, vinywaji na malazi mlihakishaje kuwa wana waliosafiri toka mikoa mingine wanajiskia wako nyumbani mbali na nyumbani ?
Tunashukuru kwamba kila kitu kilienda sawa japo sio kwa asilimia 100 ila tulihakikisha hivyo pia vinakuwa sawa japo wengi walikuwa wamshaandaa sehemu za malazi kabla hata hawajasafiri kuja Dodoma.
Kiingilio cha tamasha kilikuwa nafuu kwa waliovaa machata ya nyumbani tofauti na aliyefika tamashani bila chata, kwa nini mliamua kufanya hivi?
Kama nilivyosema kuwa hii ni kampeni ya kuhamasisha watu kuvaa machata ya ndani kwahiyo kiingilio pia kinaweza kumpelekea mtu ahamasike kutafuta chata lolote la nyumbani kama hana ili alipe buku 3.
Pia lakini kiingilio ni kama uchangiaji wa gharama za uandaaji maana bajeti muda mwingine huwa haitoshi kwa asilimia 100 hivyo kile kinachopatikana tunajazia jazia palipopungua na ni kiasi kidogo ili mtu yoyote aweze kumudu na viingilio ni tofauti kulingana na maandalizi kila mkoa ukifatilia Dar, Mbeya na Dodoma.
Ila kwa upande wangu natamani sana hata watu wangekuwa wanaingia bure lakini ndio hivyo muda mwingine mambo huwa yana bana kunakuwa hakuna jinsi.
Wana Dodoma wenyewe walipokeaje TMTFestival2021 ukiangalia ndio mara yao ya kwanza ku host TMT?
Mapokeo yalikuwa mazuri japo kulikuwa na changamoto kidogo kwenye matangazo ila tunaamini wakati mwingine yatakuwa mazuri zaidi kwa kupitia TMT ya mwaka huu.
Tamasha lenyewe lilianza saa ngapi na kuisha saa ngapi? Hali ya hewa ilikuaje siku ya tamasha? Je ratiba ya kipindi ilikuaje toka mwanzo hadi mwisho?
Tamasha lilianza saa 10 kutokana na matatizo ya umeme siku hiyo na tulimaliza majira ya saa 6 usiku. Hali ya hewa ilikuwa zuri kabisa. Ratiba ilianza kwa
(i) Kukaribisha wageni na utambulisho
(ii) Muhusika kuelezea chata lake na upatikanaji wake
(iii) Kupiga picha za kumbukumbu huku tukisikiliza ngoma za TMTFESTIVAL2021
(iv) Kuwakumbuka waliotangulia/walitutoka katika utamaduni.
(v) Burudani/performance
Wageni waalikwa katika tamasha hili walikua akina nani?
MaKaNTa, Watengwa (Jcb), KiNaSa (Nash MC), Maujanja Saplayaz (Kay Mapacha), Vichwa Vya Habari (XP- Experience), RPGs (J Yank), Watunza Misingi, Kiraka Tosh (Viraka), BCP WaGe (Swahili Genge)
Ni ma emcee gani waliopata fursa ya kuchana na mapokezi ki ujumla yalikuaje toka kwa mashabiki?
(i) Face B na Abby The Brain (Ashunga)
(ii) Jcb Watengwa
(iii)Hk Midundo na Chad Boy (Chad Bronx)
(iv) Double Y na Sheby Mc
(V) J Yank, RPGs
(Vi) DDC, Adam Shule Kongwe na Miracle Moma
(Vii) Xp - EXPERIENCE (VCW)
(Viii) MaKaNTa
(ix)Nash Mc




Mapokezi yalikuwa na mizuka ya hatari sana, unajua party la wana linavyokuwaga noma.
TMT ni tamasha la kusherehekea machata yetu. Ni machata gani yaliyowakilishwa kule? Je bidhaa zipi zilikuwa sokoni pia?
Baadhi ya bidhaa zilizokuwepo ni T-shirts, pullovers, CDs na flash zenye albums, mix tapes na Ep’s.
Changamoto gani zilijitokeza na ni vitu gani tunaweza kuboresha kwa ajili ya TMT ijayo?
Changamoto ni maandalizi ya mapema mara baada ya kujua ni wapi TMT itafanyika, bajeti ijulikane mapema na pia kuwe na muda maalum wa kuanza na kumaliza kupokea michango kwa ajili ya maandalizi ili kuepuka mikimbizano ya mwishoni na kuhakikisha kila kitu kinalipwa mapema
Je mlikuwa na wafadhili ambao walifanya nanyi kazi ili kuweza kulifanikisha hili?
Tulipata ufadhili kutoka ILLEST HUSTLA ya Ghosta El Chapo kwa kutupatia pesa pamoja na Touch DJz (DJ Kaka pamoja na DJ C) hawa walihakikisha ngoma na midundo inalia kwa mpango mzuri




Shukran sana DQ kwa kutupatia ripoti nzuri kuhusu TMTFESTIVAL2021.
Shukran Micshariki Africa.