Toka kwa: Trickson Knowledge ft Nala Mzalendo
Wimbo: Mateka
EP: Akili Kichwani EP
Tarehe iliyo toka: 01.09.2021
Mtayarishaji:Wise Genius
Studio: AMG Records

Beti Ya Kwanza – Trickson Knowledge

Tumetekwa sio/
Washenzi wametekwa na Instagram ku post makalio/
Tumetekwa na misingi ya dini/
Tumetekwa na rules mpaka tunashindwa ku wini/
Kisa maslahi sasa/
Wasomi wanaawacha kazi and then wana engage kwenye siasa/
Familia ilikufa maskini kwasababu mzazi alitekwa na anasa/
Hii dunia imetekwa na amani batili/
Kahaba amatekwa na biashara ya mwili/
Lisipo kuteka lile utatekwa na hili/
Tumetekwa na wazungu mpaka tunaikacha asili/
Tunazidi kutekwa siku hadi siku/
Maana hatubagui, wajinga tunabeba kila kitu/
Kitu tunatakiwa tafatuta ni pesa sijatekwa na usingizi/
Trickson nimetekwa na kukesha/
Na nikisema tumekwa sio uongo/
Matozi wametekwa na mademu sio mchongo/
Masela wametwa na sembe/
Hawataki kufanya kazi wametekwa na uzembe/

Kiitikio – Nala Mzalendo

Mateka tumetekwa/
Hata tukiachwa huru tunashindwa kusepa/
Mkija kutukomboa tutawakwepa/
Namkijua kilichotuteka mtatucheka/

Beti Ya Pili – Trickson Knowledge

Tego hatari baba kijani noma/
Tekwa na kahaba baba udate upate ngona/
Kutekwa sio issue maze/
Akitekwa ndama basi katekwa na pedegee/
Ukitekwa wewe jiuleze watakufanya nini? /
Usiniteke maana hua najiteka mimi/
Niki rap nawateka mashabiki/
Hip Hop imeniteka hii ni zaidi ya mziki/
Skia tumetekwa ufahamu mpaka basi/
Wanachukua ardhi wanatupa kazi/
Kwasababu walitekwa na pesa/
Sio sisi ni viongozi walarushwa ambao ukidai haki unaswekwa ndani/
Na ukitahamani tu unajikuta mahakamani/
Unafgungwa kifungu hakijulikani/
Mpaka unasahau kua utatoka mwaka gani/(inasikitisha)
Na hiyo ndio misingi ya uongozi/
Imetuteka till now kila jicho chozi/
Nadhani maskini wananielewa/
Tunavyonyimwa haki tunteswa na kuonewa/

Kiitikio – Nala Mzalendo

Mateka tumetekwa/
Hata tukiachwa huru tunashindwa kusepa/
Mkija kutukomboa tutawakwepa/
Namkijua kilichotuteka mtatucheka/

Skiza wewe bwege/
Akili fupi umetegwa kwenye tundu/
Akili za ndege/