Leo nina mizuka ya kupita na kundi japo mimi napenda kuwaita familia MaKaNTA(Maskini Katika Nchi Tajiri) hii ni moja katika familia inayofanya vizuri sana katika underground Hip Hop katika zile nguzo zake zilizopo japo zingine bado hawajazigusa kwa sana.

Katika vitu vinavyofanya leo nipite nao ndugu zangu toka Mbeya kipande cha Sae ni ile project yao ya TMT (Tunavaa Machata Tu) ni moja kati ya project kubwa sana ambayo ilianza mwaka 2019 ikafanya vizuri na ikafanikiwa kuwaunganisha Emcee’s wengi katika huu utamaduni kwa kutoa nyimbo mbali mbali zikizungumzia TMT za nyumbani Tanzania, kilele cha project ya hii TMT kwa mwaka jana ilikuwa pale Msasani Club(Dar es salaam). Hii siku hii kitu ilifana sana.

Respect kwa brother ben Benedict Mbuya alijitoa lau kununua tiketi 10 na kuwapa watu wakatazame matunda ya TMT, pongezi ziende kwa Watunza Misingi  wao walisimama kwa upande wao kufanikisha hii kitu bila kusahau timu nzima ya MaKaNTa ilikuwepo pale kuanzia Lugombo Makanta, Momumo Machata, Jadah Makanta na wengine wengi toka MaKaNTa. Pia tukamkumbuka mwanetu mwenyewe Michael Mkolosai Makanta ambaye kalala usingizi wa kudumu.

Kwenye TMT ya mwaka jana nilivutiwa na mdundo ndio ilikuwa ya kwanza kabisa kuniumiza kichwa kwa mizuka ya ghetto. Cha pili ilikuwa ni chorus ya wimbo wa MaKaNTa. Wimbo ulionivutia zaidi ni ile ngoma aliyofanya Nikki Mbishi (Baba Malcom)  Kay Wa Mapacha pamoja na Moses Mfalanyombo. Hii kwa mwaka jana ni moja kati ya project kubwa sana ambayo iliunganisha watu na kuwapa mizuka ya kuvaa machata(nembo/label/logo) ya nyumbani toka kwa wabunifu wetu mbali mbali.

Mwaka huu 2020 project imekuwa endelevu na kikubwa zaidi ilikuwa tofauti na mwaka jana, kwa mwaka huu kabla mpango kuanza ilitangazwa kuwa kila producer ambaye anapenda mdundo wake utumike atume mdundo watu wachague. Sijajua wingi wa producer waliotuma mdundo ila bahati bado ikarudi kwa Patrino (kama sijakosea jina) aliyetengeneza mdundo wa TMT ya mwaka jana. Sijajua zaidi mchakato gani ulitumika katika kupata mdundo mpaka jamaa akashinda tena ilo naomba kwa leo tukaushie tubaki na TMT.

2020 sijapata sana bahati ya kusikiliza ngoma nyingi za TMT ya mwaka huu kutokana na kutofanikiwa kuzipata lakini sina shaka sana najua nitazipata tu kwa Gego Master, Iddy Mwanaharamu au account ya MaKaNTa kule YouTube.

Kilele cha TMT ya mwaka huu kilikuwa jana jijini Mbeya japo sikuwepo lakini matukio katika picha yamenifanya niamini na kuona kuwa TMT kwa mkoa wa Mbeya maniga wamepokea vizuri.

Nachokiomba na kukiona ambalo ni wazo langu mimi Beberu La Mbegu ni kwakuwa TMT ya mwaka jana ilitoka naweza sema ni Volume 1 TMT, na ya mwaka huu ni volume 2 TMTbasi  kama tukijaliwa uzima wa afya ya mwili na roho naomba TMT ya 2021 ifanyike tofauti kidogo na TMT zilizopita nikimaanisha kua utofauti wa TMT hii ianze kwenye mdundo kwanza, kwani wengi wetu kusikiliza wimbo japo ni tofauti kwenye mdundo mmoja inakuwa kama inawashinda wanabaki na hisia kuwa wanasikiliza wimbo ule ule aliosikiliza mwanzo wa wimbo uliopota.

TMT ya 2021 naomba kamati ya TMT ikae na ichague midundo japo mitano ambayo itangazwe kuwa ndio maalumu kwa TMT na atumiwe kila Emcee ambaye atataka kufanya TMT ili aweze kuchagua ni mdundo gani anaweza kunata nao na kuwakilisha machata yetu vizuri kupitia mic, baada ya kamati kufanikiwa kwa ilo naomba hii itoke kama album na wapitishe tena shindano la kutafuta cover kali ambayo itatumika kwenye album ya TMT 2021. Na kikubwa zaidi endapo album itatoka na kufanikiwa kuuza japo kwa kidogo wale wachanaji ambao watakuwa wamefanya kazi basi kamati iwapoze makoo kidogo kwa TMT 2021.

Much respect to MaKaNTa, nyie ni familia kwangu nitakuwa pamoja nanyi na tusimame katika hii “TUACHE UPENDO UTUONGOZE” kwa kila jambo kwenye maisha yetu chuki zisizo na maana hazina faida kwetu na mziki wetu kiujumla.