Tuzo Ya Ishirini Na Nne ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (Desemba, 2023) Tumewakabidhi Wakazi (The Legacy)
Mwaka 2023 ulikua mwaka mzuri sana kwa Hip Hop ya Africa Mashariki. Wasanii wetu wa Africa Mashariki walitoa miradi zaidi ya mia mbili, ikiwemo beat tapes, ep’s, mixtapes na albums. Moja ya album nzuri zilizoachiwa mwaka 2023 ni “Beberu Declaration” ya emcee Wakazi ambayo ilitoka rasmi tarehe 28.11.2023. Album hii ambayo kabla ya ujio wakee ilikua imepigwa promo ya kutosha ndio ilitupatia singo ya “The Legacy” ambayo imemuwezesha emcee Wakazi kujinyakulia tuzo ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards, Desemba 2023.
“The Legacy” ni moja ya ngoma pendwa kutoka kwa album ya Wakazi ambayo mdundo umeundwa na mtayarishaji Black Beats aka Black In This ambae hii ni kazi yake ya pili aliyoiunda baada ya ile kazi ya “Price Up” kutoka kwa emcee Nikki Mbishi kushinda tuzo ya Micshariki Africa Emcee Of The Month baada ya Nikki kusepa na tuzo hii mwaka 2022 mwezi Desemba pia.
Kwenye mdundo mzuka wa Boom Bap, kaka Wakazi anaongelea “Legacy” yake au ukipenda kwa Kiswahili, urithi wake ambao yeye angependa kuuacha kwa ajili ya watu wake na mashabiki wake. Kaka Wakazi kwenye kazi hii anaeleza bayana kwa kua yeye ana imani na uwezo wake wakuchana na pia akiwataarifu ma mashabiki wake kua anachonuia kuwaachia ni miradi ya kudumu wala sio ngoma zinazo “hit” siku moja alafu zina sahaulika kesho yake.
Wakazi kwenye ngoma hii anaonesha alivyo master uwezo wa kuchana na kunata kwenye mdundo wakati akitupatia mashairi ya majigambo, mafumbo na tafakari kuhusu ni kiwe urithi wake kwa ajili ya mashabiki zake.
Hongera sana kwa Wakazi kwa kujinyakulia tuzo ya ishirini na tatu ya mwezi wa Desemba 2023 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.