Tuzo Ya Ishirini Na Sita ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (February, 2024) Tumemkabidhi Fivara (Barua 2, Wakala)
Nikiulizwa ni nini kinachomfanya emcee Fivara azidi kukua kila mwaka nitatumia neno la kiingereza kujieleza na kusema consistency. Consistency ndio imemfikisha emcee huyu pahali alipo na kwa emcee yoyote chipukizi anayetaka role model wa kujifunzia msome mwana.
Consistency miaka hii miwili ya nyuma imemfanya mwana atubless na EP, 259 videos kadhaa, freestyle videos, singles kibao zisizohesabika, makala za kuelimisha wasanii wenzake na album yake ya pili iliyodondoka mwishoni mwa mwaka jana Tegemeo.
‘Tegemeo’ ambayo ilikuwa miongoni mwa album zangu bora za mwaka jana ni album nzuri ambayo inaonesha dhahiri vile emcee huyu anajali sana mashairi kabla ya chochote kile. Ndio maana kwenye single na video ya kwanza rasmi kutoka kwa album hii Barua 2. Kwenye ngoma hii emcee Fivara anamuandikia marehemu baba yake barua akimwambia vile yeye ndio amempa motisha ya kuzidi kuendelea kupambania familia yao na ndoto zake pia. Barua hii ni kama shukran za dhati kutoka kwa Fivara kwenda kwa mwalimu wake wa kwanza, baba.
‘Wakala’ ndio single ya pili kutoka kwa album hii. Kwenye ngoma hii Fivara anatuelezea kisa cha jamaa flani ambaye mambo yalikuwa yanamuendea mrama mpaka pale salio lake likaongezeka ghafla na kumpa tabasamu kuwa walau hiyo siku itaisha freshi. Jamaa akatimba kwa wakala ili kuweza kutoa hela na hapo ghafla mambo yakarudi kule kule kwa hali ngumu alipokosea kuweka namba za wakala kwenye simu yake.
Story hii lazima utaielewa kama ushawahi kutoa pesa kwa wakala ukakosea namba kisha baada ya kupiga simu customer care ukaambiwa usubirie masaa 48, daah! Kwenye mdundo wa goma hili alikuwepo Odilla Beatz ambaye pia aliskika kwa video ya tatu ya mradi huu kwa jina ‘Utulivu’ ambapo ameshirikishwa mwimbaji Ivo Ivory.
Hongera sana kwa Fivara kwa kujinyakulia tuzo ya ishirini na sita ya mwezi wa February 2024 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.