Jomba Uncaly - Emcee Of The Month January 2024

Tuzo Ya Ishirini Na Tano ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (January, 2024) Tumemkabidhi Jomba Uncaly (Ghetto)

Jomba Uncaly ni mmoja wa emcees wa kizazi kipya ambaye anajituma na kuwekelea kazi. Nilianza kumskia kwenye cypher ya Door Knockers kwenye kipindi cha kwanza ambapo aliweza kujipima uwezo wa uchanaji wake na ma emcee kama P-Tah, Brima, Locs40, Tony Kings pamoja na Brima (Maovete).

Baada ya hapa mwana aliamua kutuonesha ana Akili Kichwani kwa kudondosha kanda mseto yake ya kwanza, The Lost Tapes kabla ya kuja na album yake rasmi ya kwanza Outta Ghetto ambayo pia ndio imetupatia wimbo wa Ghetto uliomuwezesha mwana kwenda na tuzo ya mwezi January 2024.

Ghetto ni wimbo ambao amemshirikisha mtayarishaji/mchanaji Buff G/Buff beats ambaye ndio kaandaa mdundo na pia kachana pamoja na mwana kwenye wimbo huu. Junior Uncaly ambaye ni mwanae Jomba nae pia alishirikishwa kwenye wimbo huu, mskie kwenye kiitikio.

Kwenye wimbo huu na kichupa kilichoachiwa mwezi jana jamaa wanaonesha na kuchana kuhusu uhalisia wa maisha yao ya kitaa. Jamaa wanakiri japokua maisha kule ni magumu na wanaweza ondoka ghetto ila vile wamepapenda ‘u ghetto’ haubanduki ng’o ndani yao kwani ndio maskani wanapopaenzi na kukumbuka kila kukicha.

Hongera sana kwa Jomba Uncaly  kwa kujinyakulia tuzo ya ishirini na tano ya mwezi wa January 2024 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.