Tuzo ya Ishirini Na Tatu ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (Nov 2023) tumemkabidhi Elijah Moz (Dandora Cinema, State Of A Nation)
Elijah Moz sio emcee wa ma juzi juzi, ila kwa mashabiki wanaofuatilia sana wasanii wa mkondo mkuu inawezekana jamaa ndio kaanza kuskika kwao hivi majuzi. Elijah Moz amekua kwenye handaki la game la Hip Hop nchini Kenya kwa zaidi ya muongo mmoja, yeye pamoja na shemeji yetu wakijiita Soul Mates Music.
Baada ya ukimya wa mda mrefu Elijah Moz ameanza kurudi tena hewani kwanza kwakudondosha “Resistance” akishirikiana na producer Kunta Official Beats mwaka 2022 na kisha mwaka 2023 aliskika kwenye miradi ys emcee Oksyde DTP, “Strictly For My Hoodlums” pamoja na mradi shirikishi wa Micshariki Africa, Fedoo na Msito, “Mashariki Ya Fikra” kabla ya yeye binafsi kuachia compilation tape yake “Born Free” ambayo tutakuja kuichambua hapa hapa Micshariki Africa, stay tuned.
Mwezi jana emcee huyu alidondosha vichupa viwili kwa ajili ya ngoma zake ambazo zinaongelea uhalisia wa maisha ya mwananchi wa kawaidi nchini Kenya pamoja na changamoto wanazozipitia.
“Dandora Cinema” inawakutanisha tena Elijah Moz na producer ambaye hata The Teacher, KRS One anakubali midundo yake, Kunta Official Beats, kutoka kule Truce Label, Nairobi. Kwenye vinanda vinavyopiga taratibu emcee Moz anaongelea maisha ya kitaa chake na vitu anavyoviona kule, ni kama unaona cinema, yaani vitu huwezi amini vinafanyika in real life….
Kwenye “State Of A Nation” emcee huyu anaongelea majanga yanayowasibu wananchi wa Kenya kama vile kodi kuongezwa kiholela, mfumuko wa bei, ziari za rais, naibu wake na mawaziri kwenda nchini za nje bila kujali madhara yake kwenye uchumi wa Kenya. Kwenye mdundo wa Afro Hip Hop emcee huyu anasaidiwa na mwanaharakati Francis Gaitho pamoja na mwanasiasa wa South Africa Julius Malema ili kuweza kueleza vizuri na kwa uwazi hali ilivyozorota nchini Kenya.
Hongera sana kwa Elijah Moz kwa kujinyakulia tuzo ya ishirini na tatu ya mwezi wa November 2023 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.