MansuLi- Emcee Of The Month Aug 2023

Tuzo ya ishirini ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (Aug 2023) tumemkabidhi Mansu Li (Sinza Starr)

Mansu Li aka Killer Bee aka Sinza Starr aliachia EP yake mpya Sinza Starr tarehe 25.06.2025 baada ya kutupatia album yake Love Life mwishoni mwa mwaka jana tarehe 25.10.2022. Hili linaonesha wazi vile mwanetu yupo busy kutuandalia sie mashabiki wa muziki wa Hip Hop kazi nzuri.  Kama hujaipa skio hii EP ya Sinza Starr unapitwa na mazuri.

Kutoka kwa EP yake ya Sinza Starr ndipo ilipotoka kibao hichi kilichobeba jina la sio EP pekee bali pia aka yake, Sinza Starr. Kwenye track hii emcee huyu anaonesha kwanini anaipenda mitaa yake ya Sinza na vile amejitwika jukumu la kuilinda na kuiheshimisha. Ngoma hii ili tayarishwa na Mnyama Double kutoka kule studio za D Sounds, Dodoma.

Waswahili hawakukosea waliposema kua mcheza kwao hutuzwa na ndio maana leo tumemtuza emcee MansuLi na tuzo ya emcee bora mwezi Agosti 2023.

Hongera sana kwa Mansu Li kwa kujinyakulia tuzo ya ishirini ya mwezi wa August 2023 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.