
Kaa La Moto - Emcee Of The Month Mwezi Desemba 2022
Tuzo ya kumi na mbili ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (Desemba 2022) tumemkabidhi Kaa La Moto (Hoi, Kijana Mwafrika)
Baada ya kutupatia mradi wa kitofauti sana na mategemeo yetu Leso Ya Mekatilili na pengine manungu’niko yakamfikia bwana Kesi akaona isiwe tabu. Kabla mwaka haujaisha emcee huyu akatudondoshea ngoma mbili ya nguvu Hoi akiwa na Magaaa na Kijana Mwafrika aliomshirikisha emcee Kala Jeremiah kutoka Tanzania na mwimbaji Leghato.
Kwenye Hoi KLM katuletea wimbo mzuka sana ambao msingi wake ni mashairi yaliyokwenda shule, usaidizi kwenye kiitikio kutoka kwa bwana Magaa ambaye nakiri ndio mara yangu ya kwanza kumfahamu pamoja na video mzuka sana inayotuhimiza sisi tuthamini vya kwetu. Kaa La Moto anaonesha uwezo wake wa kuimba na kuchana kwa wakati mmoja. Bonge la ngoma
Kaa na Kala wanaunguana pamoja wakisaidiwa na Leghato kuongea na Kijana Mwafrika. Ngoma hii ilituvutia pia kutokana na vitu kadhaa; vijana hawakuchukua jukumu la kuongea na vijana wenzao kuhusu umuhimu wa kujithamini na kuthamini vya kwao. Juu ya mdundo wa Grandmaster Teknixx wawili hawa wanachora mistari kwa Kiswahili fasaha iliyo na mafunzo si haba. Jamaa wakaona isiwe tabu wakatupatia na lyrics video bomba sana inayokufanya ujiskie fahari kuwa Kijana Mwafrika.
Hongera kwa kazi hizi mbili ambazo zinazidi kumuweka Kaa La Moto kama mmoja wa washairi na wachanaji bora wa kizazi chake. Miradi hii pia ilikuwa utangulizi kutoka mradi wake mpya uliodondoka Desemba 2022, Mkanda Mweusi.
Hongera sana kwa Kaa La Moto kwa kujinyakulia tuzo yetu ya kumi na mbili ya mwezi Desemba 2022 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.
