King Kaka - Emcee Of The Month Mwezi Februari 2023

Tuzo ya kumi na nne ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (February 2023) tumemkabidhi King Kaka (Asante, Wajionee, Umenibariki, Ray Chapter 1)

Kipindi nikiwa denti chuo kikuu mwaka wa pili mwaka 2002, emcee KRS ONE aka The Teacher aliachia mradi wake wa tano kwa jina Spiritual Minded. Mradi huu tuliupiga sana pale dormitory za chuo kwani kando na kutuburudisha ulitujenga kiroho na kutubadili mtazamo kuhusu muziki wa Hip Hop, jukumu lake na athari chanya kila kazi inaweza kuleta kwa jamii.

Miaka kumi baadae emcee King Kaka baada ya kupata fursa ya ‘kuzaliwa’ tena baada ya kupitia misukosuko ya ki afya iliyomfanya alazwe hospitali muda mrefu nae alikuja na mradi wake unaogusia maswala ya kiroho 2nd Life.

Mradi huu ndio umemuwezesha emcee huyu kutupatia video kadhaa ambazo zimemuwezesha emcee huyu mwenye uzoefu mkubwa kujinyakulia tuzo ya Micshariki Africa. Ngoma zilizomuwesha Kaka Sungura kusepa na tuzo ni;

Asante

Kwenye wimbo huu King Kaka alimshirikisha muimbaji mkongwe, Kidum na unapiga juu ya vinanda flani na ma violin pamoja na wana kwaya flani wakati yeye akitusimulia masaibu yaliyomkuta na jinsi alivyojinasua kutoka kwa mdomo wa kifo na kuweza kuishi tena licha ya madaktari kumwambia alikuwa na mda mchache sana wa kuishi.

Wajionee

Wuod Omollo ndiye mtayarishaji aliyehusika kwenye utayarishaji wa ngoma hii mzuka sana pamoja na nyingine kibao kwenye album hii kama sio zote na kusema kweli mdundo umeenda shule na umemuwezesha King Kaka kuchana mashairi yake kwa ajili ya mpenzi wake siku ya harusi yao huku akipata usaidizi mzuka kutoka kwa muimbaji Iyanii. Ooh na je ni King Kaka ndio kapiga ile “Alililiiiii…”? King Kaka na Iyani wanasheherekea upendo na mapenzi hapa, Wajionee

Umenibariki

Kwa kila unachopitia tusisahau kuwa mwenyezi Mungu katubariki, iwe kwa vingi au kwa vichache. Huu ndio ujumbe kwenye mgoma huu ambao ameshirikishwa mwimbaji wa injili Goodluck Gozbert kutoka Tanzania. Tuwe na uwezo wa kuona baraka tulizo pewa ndani ya mazingira yoyote yale tunayoyaishi au ndani ya msimu wowote ule tunaoupitia.

Ray Chapter 1

Wimbo huu nilipouskia mara ya kwanza ulinipa vibe ya wimbo wa Eminem akiwa na Dr. Dre, Guilty Conscience pamoja na wimbo classic toka kwa emcee Sticky Fingaz ambaye ni nusu ya kundi la Onxy kwenye wimbo Oh My God ambapo kwenye ngoma hizi zote ikiwemo hii ya King Kaka tunaingia kwenye akili ya mtu wakati anapopamba kujitafuta na inakuwa vita kati ya mema na mabaya. Ray nae ndio kafika kwenye njia panda hii, je atachagua njia ipi? Skia Ray Chapter 1

Hongera sana kwa King Kaka kwa kujinyakulia tuzo yetu ya kumi na nne mwezi wa February 2023 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.