Buff-G - Emcee Of The Month May 2023

Tuzo ya kumi na saba ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (May 2023) tumemkabidhi Buff G (Nipeni Maua Yangu)

Tarehe 19 April 2023 Buff G wa kundi la S.O.G (Space Of Gangstar) alitukumbushia kua bado yupo kwenye alipodondosha kibao chake kipya, Nipeni Maua Yangu. Tulikaa na kutulia na kuweza kuskiliza ngoma hii mpya aliyomshirikisha muimbaji Q Jay kwenye kazi maridadi iliyo simamiwa na G. Kifaa au ukipenda Ghost Kifaa wa Action Records.

Ngoma inapoanza tu inanasa hisia zako pale vinanda pamoja na sauti ya Q Jay zinapotoka kwenye speaker na kukwamba, “Sio msubiri mpaka mi nife…”

Kwenye wimbo huu Buff G anatukumbushia kua kifo ni lazima na hakuna mwenye uwezo wa kukizuia siku ifikapo ila kuna kitu tunaweza kumfanyia yeye au mtu yoyote yule tunae mthamini, kumpa maua yake kabla haja danja.

Kusema kweli hii ngoma inaelezea uhalisia wa maisha yetu; tunaishi, tunafanya vitu vingi vya msingi duniani, wengi wanaviona; mchango wetu kwa maisha yao, mchango kwa sanaa ya nchi yetu, mchango wa kisiasa,mchango wa kimazingira ila wanatupatia maua yetu baada ya sepa. Hivyo inabidi tujizoeze kuwathamani watu wakati bado wanaisha. Ngoma mzuka sana.

Hongera sana kwa Buff G kwa kujinyakulia tuzo ya kumi na saba ya mwezi wa May 2023 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards. Buff G, chukua maua yako.