P-Tah - Emcee Of The Month April 2023

Tuzo ya kumi na sita ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (April 2023) tumemkabidhi P-Tah (Count Your Blessings)

Ujio wa Uviko19 mwaka 2020 ulikuja na changamoto zake na kila mtu alitafuta jinsi ya kukabiliana na changamoto hizi. Kwa waliokua wanaishi kule ughaibuni na baadhi nchi kadhaa Africa kama vile Uganda na South Africa changamoto moja ilikua nini mtu afanya pale lockdown ilipowekwa kama njia moja ya kuzuia usambazaji wa gonjwa hili.

Akiwa kule Uingereza, P-Tah au ukipenda P-Tah Wa Furu aliamua kuanza kuchana nyumbani kwake kule Uingereza kama njia moja wapo ya kuondoa kuboeka wakati akiwa lockdown. Hapa ndio safari yake ya kua msanii ilipoanzia.

Safari hii imemuwezesha emcee huyu kundodosha zaidi ya EP tano ikiwemo ya hivi majuzi kati OMC3. Kuongezea hili emcee huyu mwezi jana akaja na ngoma yake mpya aliyowashirikisha emcee Fikrah Teule na muimbaji Viquee Ofula kwenye kibao chake Count Your Blessings wimbo ambao unatuhimiza sisi kuhesabu baraka zetu zote, ndogo ndogo na kubwa kubwa kwa usawa.

Kwa hiyo kwa upande wa Hip Hop Uviko 19 japokua ilikuja na madhara hasi kibao, mathara chanya tunayaona kama hivi; P-Tah kuanza kuandika mistari yake na kuanza kuchana na miaka mitatu baada ya ujio wa gonjwa hili katukumbushia kua kwa chochote kile unachopitia usisahahu ku Count Your Blessings.

Hongera sana kwa P-Tah kwa kujinyakulia tuzo ya kumi na sita ya mwezi wa April 2023 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.