Nikki Mbishi - Emcee Of The Month Mwezi Januari 2023
Tuzo ya kumi na tatu ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (January 2023) tumemkabidhi Nikki Mbishi (Price Up)
Nikki Mbishi alikuwa busy sana mwaka jana, jamaa aliachia miradi miwili kwa ajili ya mashabiki zake; the critically acclaimed Welcome To Gamboshi na kisha baadae akaachia Kanda Mseto yake Kisirani Gubu Cha Unju (K.I.G.U).
2023 ndio hii imefika na jamaa kaamua kutubariki na kichupa freshi cha wimbo wake Price Up ambao unapatikana kwenye Mixtape ya K.I.G.U. Leo tupo hapa kusherehekea msingi wa uchanaji; nondo, mistari, punch lines, uwasilishaji, unataji wa midundo, flows, mafumbo, boombap beats, video ya kibunifu na yenye hali ya juu na pia no chorus. Vyote hivi matawi ya juu, bei imepanda, Price Up.
Hongera sana kwa Nikki Mbishi kwa kujinyakulia tuzo yetu ya kumi na tatu mwezi huu wa January 2023 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.