Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (May 2022): Dizasta Vina
Tuzo ya tano ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (May 2022) tumemkabidhi Dizasta Vina kwa ajili ya ngoma yake Shahidi.
The Verteller kama anavyojiita emcee Dizasta Vina kwenye album yake iliyotoka mwaka juzi, anatupatia wimbo mzuka sana ambao umeandikwa ki tamthilia.
Tamthilia hii inatokea kwenye mazingira ya meli flani ambayo Dizasta anachukua nafasi ya Shahidi ambaye akiwa kwenye meli flani anaona mapema hatari kwenye chombo hicho cha usafiri na anafanya kila juhudi kuwahabarisha sio tu manahodha bali hata abiria waliopo mule ila hakuna anayetaka kumskia.
Anaangukia vicheko, matusi, kebehi na masimango hadi mwisho anaamua kuokoa nafsi yake kwa kushusha mtumbwi mdogo majini na kujiokoa. Akiwa kwenye mtumbwi ule anapata fursa ya kuwa Shahidi kwa mbali na kuona vile watu wanavyohangaika kuokoa nafsi zao ila wapi, wanakufa maji.
Wimbo huu pia ulikua wa kimapinduzi kwani emcee huyu alithubutu kutuletea wimbo kwa mtindo tofauti; video ilikuwa na michoro ya hali ya juu iliyowekwa pale kwa kusudi la kutuwezesha sisi kupata picha ya kile alichokipitia Shahidi na pamoja alichokiona.
Na ndio mashairi yalichanwa kwa hisia ilhali Ringle Beats mtayarishaji mkuu wa Dizasta alimuandalia mdundo mzuka wenye hisia emcee wetu hadi sisi tulihofu, tulipata majonzi na tulihoji kuhusu mkasa huu.
Hongera sana kwa Dizasta Vina kwa kazi hii ya kimapinduzi na pia kwa kujinyakulia tuzo yetu ya tano ya mwezi Mei 2022.